Wahitimu chuo cha kodi ITA wanaajiriwa wapi?

Wahitimu chuo cha kodi ITA wanaajiriwa wapi?

cj21125

JF-Expert Member
Joined
May 12, 2013
Posts
3,588
Reaction score
3,521
Ni wapi wahitimu wa shahada ya kodi wanaweza kupata ajira kama TRA wameamua kuwatosa katika interview iliyopita. Je, hiki chuo kinatambulika na kimesajiliwa? Mwenye wazo lolote kuhusu hiki chuo na upatikanaji wa ajira kwa wahitimu wake atujuze tafadhali.
 
tupo hapa alumn wa ITA,yaani pale ni mgodi wa kutoa tax consultants in tanzania
 
Hata wale wa Lushoto Institute of Judicial Administration, mahakama isipo waajiri huwa wanaenda wapi? Kuna tatizo pia kwa vijana wa JKT,au hawa ndio mgambo wa manispaa nchini.
 
JKT sio issue sana wanaweza wakaenda hata kampuni binafsi za ulinzi km Kenya Kazi au ULTIMATE
 
Kwani unadhani kila anayesoma ITA lazima afanye kazi TRA? Tax consultant's TZ mtawatoa wapi
 
Mbona huyo jamaa hajasoma ata hiyo ugali dagaa.. UD..
 
Kama mtu hajafanya usahili vizuri akafaulu unataka achukuliwe tu ilimradi kasoma chuo hiko ,basi kusingekua na haja ya kufanya interview wangechukuliwa direct toka huko
 
mkuu haukua na mkataba wowote ule kwamba ukimaliza ITA basi utapelekwa TRA moja kwa moja...au registration form yako ilisema ivyo?? inamaana hata wale walio vyuo ambavyo viko chini ya wizara ya fedha wakimaliza tuu wabebwe huko wizarani???ulitakiwa kufaula usahili, inamaana darasa zima mlioomba mmefeli usahili huo???basi kuna matatizo ya mlichofundishwa chuo mnashindwa kucompete na labour market...
 
Kuna jamaa zangu walisoma chuo cha azania college of management kipo upanga kinatoa sheria ngazi ya cheti na stashahada walikuwa kwenye usahili na watoto wa ija tume ya utumishi wa mahakama lakini walibahatika kupata kazi huko na hao wa ija walitoswa . Cha msingi ni kujieleza na kupita kwenye usahili tu haya mambo ya chuo kipo chini ya wizara hakuna kitu. Kama usahili ukifanya vibaya ndo basi tena.
 
Hata wale wa Lushoto Institute of Judicial Administration, mahakama isipo waajiri huwa wanaenda wapi? Kuna tatizo pia kwa vijana wa JKT,au hawa ndio mgambo wa manispaa nchini.
sidhani kama jina la chuo ndo kigezo cha kupata kazi..Hao wana Ija wapo wengi kazini na sio mahakamn tu kana udhaniavyo
 
Kuna jamaa zangu walisoma chuo cha azania college of management kipo upanga kinatoa sheria ngazi ya cheti na stashahada walikuwa kwenye usahili na watoto wa ija tume ya utumishi wa mahakama lakini walibahatika kupata kazi huko na hao wa ija walitoswa . Cha msingi ni kujieleza na kupita kwenye usahili tu haya mambo ya chuo kipo chini ya wizara hakuna kitu. Kama usahili ukifanya vibaya ndo basi tena.
well said!!hata Rita walikuwepo wengi wa Azania na Ija but kupata kazi kunatokana na ww na juhudi zako jina la chuo halikusaidii lolote pale ni ww na uwezo wako..
 
Back
Top Bottom