Wahisani wapunguza kuchangia bajeti ya serikali | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wahisani wapunguza kuchangia bajeti ya serikali

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by BabuK, May 14, 2010.

 1. BabuK

  BabuK JF-Expert Member

  #1
  May 14, 2010
  Joined: Jul 30, 2008
  Messages: 1,847
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  VIONGOZI WIZARA YA FEDHA WAITISHA KIKAO CHA DHARURA
  [​IMG]

  Rais Jakaya Kikwete

  UAMUZI wa wahisani kupunguza fedha wanazochangia kwenye bajeti ya taifa kila mwaka, umeishtua serikali ambayo jana ilikaa kikao cha dharura kujadili taarifa hiyo.

  Wahisani wamepunguza mchango wao kwenye bajeti ya serikali kwa mwaka 2010/2011 kwa sababu mbalimbali, ikiwamo kasi ndogo ya serikali katika kutekeleza mageuzi kwenye sekta za umma.

  Taarifa ya wahisani hao iliyotolewa jijini Dar es Salaam juzi, inaeleza kuwa mwaka huo wa fedha, watatoa dola za Marekani 534 milioni sawa na Sh721bilioni, ambazo ni pungufu kwa Dola za Marekani 220 milioni sawa na Sh297 bilioni walizotoa mwaka 2009/2010.

  Wahisani wa bajeti ya serikali ni Benki ya Maendeleo Afrika (ADB), Canada, Denmark, Jumuiya ya Ulaya (EU), Finland, Ujerumani, Ireland, Japan, Uholanzi, Norway, Sweden, Uswisi, Uingereza na Benki ya Dunia (WB) mwaka jana walichangia Sh1.9 trilioni katika bajeti ya serikali kupitia miradi ya maendeleo na mifuko ya kisekta.

  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Uchumi, John Haule jana aliliambia gazeti hili kuwa baada ya kupata taarifa hizo walijadili kwa dharura ili wampe waziri taarifa ambayo ataitoa baadaye kama tamko la serikali.

  "Tulikuwa tunaijadili taarifa iliyotolewa na wahisani. Tulijadiliana ili tumpe waziri aitoleee tamko," alisema Haule.

  Haule alifafanua kuwa pamoja na taarifa ya wizara yake, waziri Mustafa Mkulo ambaye sasa yuko safarini nje ya nchi atatakiwa pia kuzungumza na vitengo vingine vya serikali na kupata maoni yao kabla hajatoa tamko hilo.


  ADB ambayo ndiyo mwenyekiti wa wahisani hao ilieleza katika taarifa yake kwa vyombo vya habari juzi kuwa uamuzi wa kupunguza fedha za kusaidia bajeti ya serikali, umetokana na mambo mengi, ikiwemo serikali kushindwa kufikia malengo kadhaa ya maendeleo.

  Taarifa hiyo ilitaja maeneo ambayo serikali ilishindwa kufikia malengo kuwa ni mabadiliko ya haraka katika menejimenti ya sekta ya fedha za umma, mategemeo ya kuboreka kwa hali ya mazingira ya uwekezaji na uboreshaji wa huduma kwa kutoka sekta za umma.

  "Serikali na wahisani wa maendeleo wamekubaliana kuwa wanahitaji kufanya kazi kwa pamoja kuzifanyia kazi, sera na kuchukua hatua ambazo zitaleta matokeo mazuri ya kuwa na maendeleo, pamoja na kufikia malengo ya kupambana na umaskini kwa faida ya Watanzania. Matokeo mazuri yatasaidia kuzuia upungufu wa fedha za wahisani siku za mbele," inaeleza sehemu ya taarifa hiyo.

  Hii ni mara ya nne kwa wahisani hao kuiwekea ngumu serikali katika kuchangia bajeti yake kila inapofikia mwisho wa mwaka, kwa kushindwa kutekeleza mambo wanayofikiria wao kuwa ni muhimu zaidi katika maendeleo ya nchi.

  Mwaka juzi wahisani hao waligoma kutoa fedha baada ya serikali kusuasua kuchukua hatua dhidi ya watuhumiwa wa ufisadi wakiwemo wa fedha za EPA mpaka zilipofunguliwa kesi kadhaa ambazo mpaka sasa zinanguruma mahakamani.
   
 2. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #2
  May 14, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Wamechoka na upotevu wa pesa za umma through ufisadi ulioikithiri ndani ya utawala wa JK na wahusika wakuu kuachwa.
   
 3. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #3
  May 14, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Bila shaka Zak. Nadhaniu hatua hii kwa kiasi kikubwa imesukumwa na kitendo cha JK kuwatukana wafanyakazi walipoomba sehemu halali ya keki ya taifa inayopikwa kwa mchango mkubwa na wahisani hao.
   
 4. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #4
  May 14, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  Wake up call; ifikie mahala waondoe kabisa hiyo michango! sasa kama ni only 35 percent ya watoacho ndio kinawafia walengwa si bora ikosekane kabisa!

  Nafikiri ndipo akili ya kusimamia na kukusanya mapato ya ndani itatujia
   
Loading...