Wahisani wapunguza fedha bajeti ya serikali ya 2010/2011 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wahisani wapunguza fedha bajeti ya serikali ya 2010/2011

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Luteni, May 12, 2010.

 1. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #1
  May 12, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  WAHISANI wamepunguza mchango wao kwenye bajeti ya serikali kwa mwaka 2010/2011 kwa sababu mbalimbali, ikiwamo kasi ndogo ya serikali katika kutekeleza mageuzi katika sekta za umma.

  Taarifa ya Wahisani hao iliyotolewa jijini Dar es Salaam jana, imesema katika mwaka huo watatoa Dola za Marekani 534 milioni sawa na (Sh721bilioni), ambazo ni pungufu kwa Dola za Marekani 220 milioni (sawa na Sh297 bilioni) walizotoa mwaka 2009/2010.

  Wahisani wa bajeti ya serikali ni Benki ya Maendeleo Afrika (ADB), Canada, Denmark, Jumuiya ya Ulaya (EU), Finland, Ujerumani, Ireland, Japan, Uholanzi, Norway, Sweden, Uswisi, Uingereza na Benki ya Dunia (WB) ambao mwaka jana walichangia Sh1.9 trilioni katika bajeti ya serikali kupitia miradi ya maendeleo na mifuko ya kisekta.

  Katika bajeti hiyo ya mwaka 2009/2010 Sh milioni 968,028 zilitokana na mikopo ya ndani na sehemu ya mchango wa wahisani hao kupitia misaada ya kibajeti.

  ADB ambayo ndiyo mwenyekiti wa wahisani hao jana, ilieleza katika taarifa yake kwa vyombo vya habari kuwa uamuzi wa kupunguza fedha za kusaidia bajeti ya serikali, umetokana na mambo mengi, ikiwemo serikali kushindwa kufikia malengo kadhaa ya maendeleo.

  Taarifa hiyo ilitaja maeneo ambayo serikali ilishindwa kufikia malengo kuwa ni mabadiliko ya haraka katika menejimenti ya sekta ya fedha za umma, mategemeo ya kuboreka kwa hali ya mazingira ya uwekezaji na uwekezaji na uboreshaji wa huduma kwa kutoka sekta za umma.

  Hii ni mara ya nne kwa wahisani hao kuiwekea ngumu serikali katika kuchangia bajeti yake kila inapofikia mwisho wa mwaka, kwa kushindwa kutekeleza mambo yanayowavutia kutoa fedha.

  Mwaka juzi wahisani hao waligoma kutoa fedha baada ya serikali kusuasua kuchukua hatua dhidi ya watuhumiwa wa ufisadi wakiwemo wa fedha za EPA mpaka zilipofunguliwa kesi kadhaa ambazo mpaka sasa zinanguruma mahakamani.

  Akizungumza katika mkutano huo, ambao ulihusisha nchi wahisani na taasisi za kimataifa, Mwenyekiti wa Nchi Wahisani wa Bajeti ya Serikali (DPG), Peeter Dorst alisema nchi wahisani zinaamini kuwa ni muhimu kwa serikali kuonyesha wanachukua hatua katika suala zima la rushwa zikiwemo rushwa ndogo na kubwa.

  Alisema hali hiyo inatokana na habari za hivi karibuni kuonyesha kuwa Tanzania imeshuka nafasi 24 katika suala zima la uwazi katika mapambano dhidi ya rushwa.

  Source: Gazeti la Mwananchi
   
 2. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #2
  May 12, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Mimi nafikiri ni wazo zuri tu kwa kupunguza mchango wao
   
 3. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #3
  May 13, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  IMO, the most interesting part inasomeka kama hivi:

  Kaa kila siku tunavosema humu., hakuna free lunch chini ya jua..lakini wachache wanaoelewa hili kwa mapana yake. DIrect translation ya hii statement ni kwamba kaa nguvu za kibeberu zikishindwa 'kuwekeza' sahauni 'misaada'. Kwa namna nyingine wanauma na kupuliza, ila wakiona mnaresist nguvu za kibeberu zinakwamishwa nadhani WATAUMA MOJA KWA MOJA. Lakini wakipunguza hivi huenda ikawa ni wake-up call kwa hii mibwenyenye ilokosa dira na mwelekeo.
   
 4. Cynic

  Cynic JF-Expert Member

  #4
  May 13, 2010
  Joined: Jan 5, 2009
  Messages: 5,154
  Likes Received: 628
  Trophy Points: 280
  Huku kwao wana'downsize' matumizi ktk kila kitu.. sembuse misaada kwa 3rd world countries?
   
 5. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #5
  May 13, 2010
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Afadhali hata hiyo misaada ingefutwa kabisa tujue moja. Ardhi tunayo, dhahabu tunayo, mafuta tunayo, kinachotushinda nini?
   
 6. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #6
  May 13, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Samahani kidogo, kuuliza si ujinga.

  Hivi hawa wanaoitwa ADB ndio wakoje wakoje? Ni nini haswa chanzo cha fedha cha hawa watu? Wamiliki ni akina nani?
   
 7. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #7
  May 13, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Mzee Nkapa alikuwa anasema tunalipa madeni ili tuwe taifa linalokopesheka. Manake ni kwamba hakuna mkakati mbeleni wa kujitegemea, kila kitu mpaka washikiwe remote control na kubonyezewa kabisa!.
   
 8. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #8
  May 13, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Thanks for the obvious.
   
 9. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #9
  May 13, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Good point my friend. Their own governments are downsizing and their own governments are in need of money so why should they aid Africa? Their governments are also now in debt so why should they borrow to countries with little hope of paying back? Why should they lend when they are now also borrowing? Nadhani ni attitude yetu sasa na tuna dhani "misaada" ni haki yetu.

  Another point I'd like to add is that "aid" to Africa is not really aid per say. They are investments the West are making in order to gain something in return whether it is influence or favoritism when it comes to investment opportunities. Like any investment the investor would like to minimize cost and maximize profits. So when the costs increase and profits decrease the investment is no longer worth it. So ukiona nchi za magharibi zina punguza misaada ni dalili ya mambo mawili....1)Your government is bold enough to not be pushed around or 2)You are use to them has decreased.
   
 10. K

  Keil JF-Expert Member

  #10
  May 13, 2010
  Joined: Jul 2, 2007
  Messages: 2,214
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Watembelee kwenye site yao hapa chini: www.afdb.org
   
 11. Abunwasi

  Abunwasi JF-Expert Member

  #11
  May 13, 2010
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 3,166
  Likes Received: 1,061
  Trophy Points: 280
  Maoni yangu ni kuwa hali hii kama tutaichukulia kama challenge [badala ya kulalamika kukosa pesa za bure] hali hii inaweza kuwa blessing in disguise. Hawa jamaa wanapenda turegeze masharti ya uwekezaji ili wavune kiurahisi na kuwafaidisha share holders wa mabenki ya uwekezaji ya kwao na kunenepesha uchumi wao na sisi watuwache kama manamba omba omba na kuitana mafisadi.

  Hata hivyo serikali inaweza kuraise hiyo short fall kwa kupunguza mianya ya kodi pamoja na viwango lakini kupanua wigo kwa sana [ili kusiwe na sababu ya kutolipa kodi-by highly penalising defaulters-
  Siyo siri kuwa viwanda vingi vya uzalishaji vinakwepa kulipa kodi stahili kwa kuhonga [angalia mali zinazohodhiwa na baadhi ya wakusanya kodi] kwa vile viwanda vingi viko mijini ninadhani hazina ingefungua kitengo independent of TRA ku audit kodi inayotakiwa kukusanywa against actual kodi inayokusanywa by TRA.

  Vilevile serikali iikubalie TRA kuwamotivate zaidi wakusanya kodi ili kadiri wanavyokusanya basi nao motisha yao iendane na kazi za individuals involved.

  Na mwisho serikali iongeze makali kwa sana katika kuhakikisha kuwa matumizi hasa kwenye halmashauri na mikoa yanaendana na mipango iliyopangwa na value for money na tuanze kufukuzana kazi /kupelekana mahakamani kwa ubadhirifu/uzembe wa mali za umma.
   
 12. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #12
  May 13, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Nimekusoma.

  Kule kwene web yao kuna info kaa thesis mbili za PhD za ungwini....na naskia uvivu kwenda kupekua..Nilikuwa natafuta ntu anayejua tu kidogo tu-hint tuwili tutatu..ili nikipata wasaa nijue pa kuanzia.
   
 13. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #13
  May 13, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  I second you for this point, kwa wazungu hakuna msamiati wa neno AID kwao ni INVESTMENT/BUSINESS kama ulivyosema ukiona wanapunguza misaada jua kuna kitu wameona hakiendi vizuri kwa upande wao na si upande wetu, wanaposema wamepunguza kwa sababu serikali haijaboresha mazingira bora ya uwekezaji maana yake serikali imeanza kuwabana sehemu hizo rejea sera ya madini.
   
 14. Technician

  Technician JF-Expert Member

  #14
  May 13, 2010
  Joined: Mar 30, 2010
  Messages: 843
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0


  Mambo yameanza kuwaendea kombo,tumeanza kuwashtukia,kizazi kipya limeanza kukamata wazungu pabaya.wataanza uhusiano na vijana kizazi kipya ili kuweka mambo yao vizuri,wameanza kuweka waziri mkuu kizazi kipya ili kuweza kuunganisha vijana wengi na kuwalobby,kama huamini muda si mrefu waziri mkuu Cameron atakuja Tanzania kumtembelea JK na utasikia kaja kutoa msaada wa mabilioni,ukiuliza utaambiwa kwa ajili ya wahanga wa mafuriko kule kilosa kumbe wamekuja kusaini mkataba wa kuchukua madini yetu kule Buzwagi na bulyanhulu kama sio Kahama mining wakisimamiwa na waswahili wenzetu pale kama wakina Deo na Malogo wakidanganywe na visafari vya mara kwa mara Ughaibuni ili wasahau utanzania wao wajue maisha yako ulaya tuu na sio Tanzania.
   
 15. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #15
  May 13, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,944
  Likes Received: 2,091
  Trophy Points: 280
  Hiki ni chombo kama World Bank, kuna nchi wanachama wa Africa ila hata wale wa nje kama USA, UK ni wanachama na wana haki ya kupiga kura. Kuna 'madirisha' mawili ya misaada kwa nchi masikini na tajiri za Afrika. Maelezo zaidi inabidi uende kwenye tovuti yao.
   
 16. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #16
  May 13, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,944
  Likes Received: 2,091
  Trophy Points: 280
  Jambo la kupunguza misaada itatusaidia sana kwani kwa upande wa pili litatusaidia kufikiri na kufanya kazi kwa biddi ilimradi hatujiibii pesa zetu kwani JK alimwambia Bush kuwa hatuibi za waisani maana yake wanaiba za wanachi!
   
 17. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #17
  May 13, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Ndugu yangu,

  Kwa uzoefu uliopo na hali ya sasa, ni kwamba hakuna mipango ya kujitegemea kwa maana ya kuisimamia mipango tangia ngazi ya fikra mpaka utekelezaji. Trust me kutokana na hali hiyo taathira ni shurti iwepo na kusema ukweli hali itakuwa mbaya zaidi. Ukiwa tegemezi wewe ni wa kuburuzwa tu left and right, hakuna raha ya maisha kabisa wala matumaini.
   
 18. MchunguZI

  MchunguZI JF-Expert Member

  #18
  May 13, 2010
  Joined: Jun 14, 2008
  Messages: 3,623
  Likes Received: 590
  Trophy Points: 280
  Safri za mkuu wa nchi nje ya nchi zimezaa matunda gani? Wamegundua nini juu yake mpaka kufikia hatua hii?

  Kwangu mimi, mtu wa kawaida hiyo ni habari njema. Serikakli zetu hizi hazistahili misaada kabisa. Nadhani wahisani wanastahili kufanya 'resource assessment' ya nchi yetu na baadaye tuambiwe ni kiasi gani tunakiacha kwa uzembe. Msaada utokane na ziada tusiyoiweza.

  Enzi za kudai misaada kwa kisingizio cha kutawaliwa zimekwisha. Ndo maana tunahitaji watu makini ktk madaraka, waunde serikali ya watu makini na siyo uswahiba.
   
 19. G

  Godwine JF-Expert Member

  #19
  May 13, 2010
  Joined: Jan 15, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  wahisani si watu wa kutegemea tunatakiwa kuanza kujitegemea kuanzia sasa ni haibu taifa lenye rasilimali kama
  tanzania kuwa tegemezi
   
 20. Z

  Zungu Pule JF-Expert Member

  #20
  May 14, 2010
  Joined: Mar 7, 2008
  Messages: 2,139
  Likes Received: 682
  Trophy Points: 280
  Mkopo si msaada. Nchi nyingi tu, hata zile zinazojitegemea huwa, zinakopa.
   
Loading...