jmushi1
Platinum Member
- Nov 2, 2007
- 26,329
- 25,257
JK akwepa kitanzi cha wahisani
na Prisca Nsemwa
UMOJA wa Nchi za Ulaya (EU), umetangaza rasmi kuendelea kuichangia bajeti ijayo ya serikali, ikiwa ni siku chache tu baada ya kuwapo kwa taarifa za kusita kufanya hivyo kutokana na kukithiri kwa tuhuma za ufisadi miongoni mwa viongozi wa dola.
Tamko hilo ambalo kwa kiwango kikubwa limeinusuru Tanzania inayotegemea misaada ya wafadhili kuendeshea bajeti yake kwa kiwango cha zaidi ya asilimia 40, lilitangazwa jana mbele ya waaandishi wa habari na Balozi Kiongozi wa EU, Tim Clarke.
Clarke katika tamko lake hilo alisema uamuzi huo wa wahisani umechangiwa kwa kiwango kikubwa na kuridhishwa kwao na juhudi zinazofanywa na Rais Jakaya Kikwete katika kukabiliana na vitendo vya ufisadi ndani ya serikali yake.
Umoja huo ambao ni wachangiaji wakuu katika bajeti ya serikali, walifikia hatua ya kutaka kusitisha misaada yao kutokana na kukithiri kwa tuhuma za ufisadi zinazowahusisha viongozi wakubwa serikalini.
Ni kweli tulianza kupoteza imani kwa Serikali ya Tanzania baada ya kuibuka vitendo vya ubadhirifu, lakini kwa vile juhudi za rais katika kupambana na vitendo hivyo tunaziona, tumeamua kuendelea kushirikiana na Tanzania kuchangia bajeti ya serikali, alisema Clarke.
Akizungumza na waandishi wa habari katika makao makuu ya umoja huo jijini Dar es Salaam, alisema kuwa umoja huo umeisaidia Tanzania katika sekta ya elimu, kilimo, utamaduni na kuchangia bajeti kila mwaka.
Ingawa hakutoa mifano halisi ya kuridhishwa kwao na hatua zilizochukuliwa na serikali, ni wazi kwamba, wahisani hao wameridhishwa na namna Rais Kikwete alivyoshughulikia kashfa za EPA, Richmond na ile ya Andrew Chenge.
Taarifa za wahisani kupoteza imani kwa serikali kwa mara ya kwanza zilitolewa na Balozi wa Uingereza hapa nchini mwaka jana, Philip Parham, wakati aliposema bayana kwamba, imani waliyokuwa nayo kwa Serikali ya Rais Kikwete ilikuwa imepungua kuliko ilivyokuwa katika kipindi cha mwaka uliopita wa fedha.
Kutokana na hali hiyo basi, Parham alisema wahisani wanaotokana na kundi la nchi 14 zinazotoa misaada katika bajeti walikuwa wameitaka serikali kuchukua hatua za haraka kurejesha imani hiyo ambayo kuporomoka kwake kulichangiwa pia wasiwasi walionao katika matumizi ya fedha za misaada na mikopo wanazotoa kwa Tanzania.
Parham alitoa tamko hilo wakati akitoa taarifa ya wafadhili walipokuwa wakijadili utekelezaji wa bajeti ya serikali ya mwaka 2006/07, katika mkutano ulioshirikisha wadau mbalimbali wa maendeleo.
Kwa kuonyesha uzito wa kauli hiyo nzito, balozi Parham kabla ya kusema maneno hayo alianza kwanza kumwomba radhi aliyekuwa Waziri wa Fedha wakati huo, Zakia Meghji, kwa atakayoyasema, akisema ameamua kuwa muwazi kwa kueleza kile wafadhili wanachokiona.
Mafanikio bado yapo mbali. Ninaamini Mheshimiwa Waziri (Meghji) atanisamehe iwapo ninataka kuwa mkweli kuhusu mtazamo wa wahisani Mazingira ya leo yanatoa changamoto zaidi kuliko ilivyokuwa mwaka uliopita. Leo imani waliyokuwa nayo wahisani wa maendeleo imepungua kuliko ilivyokuwa mwaka 2006, alisema balozi huyo.
Kutokana na hali hiyo, Balozi Parham akionekana kuwasemea wahisani wenzake wengine ambao katika bajeti inayoisha Juni mwaka huu walichangia kiasi cha dola za Marekani milioni 673, sawa na asilimia 15 ya bajeti nzima, aliitaka serikali kuimarisha uwajibikaji kwa wadau wake, kikubwa akikitaja kuwa ni kukabiliana na usifadi.
Alisema washirika wa maendeleo wanataka kuongeza misaada kwa Tanzania hasa katika kipindi hiki kigumu ambacho misaada zaidi inahitajika.
Hata hivyo, alibainisha kuwa viwango vya juu vya ufadhili kwa upande mmoja, kwa upande mwingine vinahitaji utendaji makini kutoka serikalini, jambo ambalo Serikali ya Awamu ya Nne imelitekeleza.
Kuhusu washirika wa maendeleo, balozi huyo alibainisha kuwa yanapokea mwangwi wa hali halisi ya Tanzania kutoka kwa maofisa wa serikali, asasi za kiraia, wasomi na wananchi kwa ujumla katika mambo mawili makubwa.
Balozi Parham aliyataja mambo hayo kuwa ni uhitaji wa serikali kutafsiri bajeti na kuifanya ionyeshe maendeleo halisi na kuinua hali ya wananchi maskini.
Lakini ni jambo la wazi kwamba kisiasa, viwango vya juu vya ufadhili kutoka washirika wa maendeleo vinahitaji viwango vya juu vya uwajibikaji serikalini.
Hofu kubwa ya washirika wa maendeleo, kama ambavyo inaonyeshwa pia na maofisa wa serikali, vikundi vya kijamii, wasomi na wananchi kwa ujumla, inahusu masuala hayo mawili, alisema.
Alisema hali inajionyesha kuwa ili kushinda vita dhidi ya rushwa, serikali ya Rais Kikwete imelifanya hilo kuwa kipaumbele, jambo lililogeuka kuwa mjadala wa kitaifa ambao waathirika wakuu ni wananchi maskini.
Miezi kadhaa baadaye Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (CHADEMA) wakati akichangia kwenye kikao cha mwongozo wa kutayarisha mpango na bajeti ya serikali kwa kipindi cha mwaka 2008/2009 kwenye Ukumbi wa DICC, Dar es Salaam alisema, nchi wahisani zilikuwa zimetishia kutochangia bajeti ya nchi ya mwaka 2008/2009 kama serikali haitachukua hatua kali dhidi ya watu wanaodaiwa kuchota mamilioni ya fedha katika Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA) na Kampuni ya kuzalisha umeme wa dharura ya Richmond.
Zitto, mwanasiasa aliyeibua hoja kuhusu utata uliozunguka kusainiwa kwa mkataba wa mgodi wa madini wa Buzwagi katikati ya mwaka jana na kuibua mtafaruku mkubwa nchini, alisema wahisani wameonyesha nia ya kutochangia kiasi cha fedha kama serikali haitachukua hatua kali dhidi ya mafisadi.
Mheshimiwa Mwenyekiti ningependa kupata maelezo kwa kuwa, kuna habari kwamba mwaka huu wahisani wameonyesha nia ya kutochangia kiasi chochote cha fedha kwa ajili ya bajeti yetu, je, tatizo nini? alisema Zitto ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA.
Alisema serikali iliomba kiasi cha sh bilioni 970 kwa ajili ya kuchangia bajeti ijayo, lakini wamegoma baada ya kutoa masharti kwa serikali na kwamba yasipotekelezwa kuna uwezekano mdogo wa kuchangiwa.
Mbunge huyo alisema, moja ya sharti lililotolewa ni kwamba serikali inatakiwa kuhakikisha inawakamata wahusika walioiba fedha kwenye Akaunti ya EPA na kuwataja majina, kisha kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria.
Alisema sharti la pili lililotolewa na wahisani hao ni kwamba, wameitaka serikali kuhakikisha inamaliza suala la mpasuko wa kisiasa kati ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha Wananchi (CUF).
Wahisani wameonekana kutaka suala la mazungumzo kati ya CCM na CUF limalizike haraka, kwa vile limeonekana kuwa tatizo kwa muda sasa, alisema Zitto.
Akijibu hoja hizo za Zitto, Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo, alisema ni kweli wahisani walishtushwa na hali ya mambo ilivyokuwa nchini na kuonyesha nia ya kutochangia bajeti kutokana na ufisadi katika EPA na Richmond.
Alisema si wahisani peke yake walioshtushwa na hali hiyo, bali hata serikali nayo ilipata mshtuko huo, lakini ilijipanga vilivyo na kuwawajibisha watendaji wote waliohusika na kashfa hizo ambazo zimelitia taifa aibu na kukwamisha maendeleo.
Mkulo alisema wahisani walitaka kuona hatua zitakazochukuliwa na serikali dhidi ya watu waliohusika na ufisadi huo ili waendelee kutoa misaada ya maendeleo nchini pamoja na kuchangia bajeti ya taifa ambayo asilimia 40 inategemea fedha kutoka kwao.
Kwa kusema kweli wahisani walisita kutoa misaada yao au kuahidi watatuchangia nini katika bajeti yetu, lakini mambo hivi sasa yanakwenda vizuri, alisema Mkulo.
Alisema uwazi wa serikali katika kuwashughulikia watu waliohusika na kashfa za Richmond na EPA, ikiwa ni pamoja na uamuzi wa kujiuzulu kwa aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa, kwa kiasi kikubwa umechangia kurudisha imani kwa wafadhili hao. Alisema mazungumzo kati ya serikali na wahisani hivi sasa ni mazuri na mwezi ujao wanatarajia kutangaza ahadi za wahisani ambao wanatarajia kuchangia bajeti ya Tanzania inayotegemewa kuwasilishwa bungeni mwezi wa Juni. Ili kuuthibitishia umma juu ya uhusiano mzuri unaoendelea baina yetu, mwezi ujao nitatangaza ahadi za nchi 16 ambazo ni wahisani wetu wanaotusaidia katika bajeti yetu, alisema Mkulo.