Wahindi wawili wafia hotelini Dar

Wahindi wawili wafia hotelini Dar

Wao mbona hawataki tuwaoe watoto wao. Wanatuita sisi ma GOLO unajua maana ya GOLO?
Niko hapa ofisini tuko na dada mmoja mama yake ni Mhaya baba ni Mhindi. Unamfahamu ShyRose Bhanji? Naye ni combination ya Mhindi na Mswahili. Haujataka tu kumwoa Mhindi.
 
Pombe inauwa "double" kwa mpigo, real surprise. Tusubiri uchunguzi kwa kweli......
 
mwandishi kajuaje kaa wahindi wakati passport zao zinaonyesha canada na south africa? .....
kwa sura tu anaweza kuwa ana asili ya Pakistani even ...........kwa nini afutuke moja kwa moja na kusema wahindi wakati hana shahidi ( au anao sina mie?)
 
Watu wa UWT itabidi pia wachunguze, inawezekana hawa jamaa wameuawa 'kijasusi' katika shughuli za kijasusi, polisi peke yao inaweza kuwasumbua sana kama ni hivyo! Lakini baadae tuambiwe nini hasa kilitokea?
 
Sio tu ni mbaguzi bali pia mnyanyapaaji. lugha ya Kitanzania sio hiyo. Zeruzeru tunawaita walemavu wa ngozi; bubu walemavu wa ulimi; viziwi tunawaita wasiosikia; hani*** tunamwita sio rizki.....

Alivyo andika ni sahihi akimaanish raia wa India kama raia wa tanzania anavyoitwa Mtanzania.
 
mimi nashangaa sana watanzania na ujinga wetu wa kujifanya tunajali haki za binadamu za kutobaguana,
hao jamaa ni wahindi full stop, ukisema watu wenye asili ya asia hakuna mtu atakejua aidha ni mchina au mphilipino,
dunia nzima unapokwenda citizens first, na uwezi ukasema citizens first bila kupractize ubaguzi, fika kenya, rwanda, SA, hata US kwenyewe ni ubaguzi ambao wao wanaita ni uzalendo lakini hapa ukiongelea wahindi mafisadi unaambiwa ni ubaguzi wa rangi, nadhani muda umeshafika wa kurudia ule uzalendo wetu
we ulishaona wahindi wangapi wanajeshi au polisi hapa tanzania, kwa idadi yao hapa tanzania labda ni asilimia 0.0001,

kwa kifupi hao jamaa walikuja kazini na kuna uwezekano mkubwa ni mauaji ya kuzurumiana au ni kazi ya usalama wa taifa baada ya kujua nyendo zao
 
Kusema wahindi wawili na watu wawili wenye asilia ya Asia whats the difference?
Tofauti ipo kubwa tu Mkuu. Tofauti yake ni kwamba, Mhindi anaweza kuwa ni raia wa nchi yeyote nyingine isiyokuwa India na pia anaweza kuwa ni raia wa India. Anaweza kuwa na asili ya India na vile vile asiwe na asili ya India lakini akawa na uraia wa India.

Kwa upande mwingine, watu wenye asili ya Asia sio wote ni watokao India (sio wote ni wahindi). Kuna wachina, wapakistan, wahindi na kadhalika.


Nadhani maneno mazuri yanayotosha kuwaelezea wahusika katika janga hili ni Watu wenye uraia wa ......... na wenye asili ya India. Nadhani hiyo ingeweza kuwa sahihi zaidi.
 
Rwabugiri,

Lugha iliyotumiwa ni sahihi kabisa.

Watu wawili wenye asili ya Asia sio sahihi na pia sio lazima wawe wahindi. Wanaweza kuwa yeyote tokea Palestine mpaka Japan.

Lisilo la kawaida ni kwa Wahindi kufurika nchini na kufia huko kiajabu ajabu.

Kwanini asingesema Mkanada na Msauzi? "Uhindi" wao has what to do with anything? Wabongo tuko casual kinoma kwenye ubaguzi wetu.

Hii itakuwa poisoning, watu wawili wazidishe pombe at the same time? Tena wamerudi chumbani kwa nguvu zao wenyewe? Polisi wetu ndo hivo lakini hakuna CSI wanatafuta majibu rahisi kesi imeisha.
R.I.P
 
Wao mbona hawataki tuwaoe watoto wao. Wanatuita sisi ma GOLO unajua maana ya GOLO?

Huo ndo ubaguzi wenyewe mzee! WAO ndo akina nani? Kama kuna mtu kakutendea vibaya basi umchukie huyo mtu sio uchukie kila mtu mwenye ngozi sawa!
 
Nilikuwa pale JM leo. Kuna mtu wa pale kaniambia wale wahindi walikuwa watu wa kinywaji na unga kwa sana. Pia wacheza kamari Le Grande, ipo pale pale JM Mall. Mnajua mema na mabaya ya kamari. Labda walishinda pesa nyingi, au walimdhulumu mtu. Who knows?
 
Hivi nchi yetu huu mtindo wa kuunda timu utaisha lini?. Yaani hakuna timu maalum ya kushughulikia masuala kama haya mpaka litokee tatizo?. Yaani wanakuwa too reactive badala ya kuwa active, hii inachosha kabisa. Na haya mambo ya timu ni siasa tupu hakuna la maana. Ni mpaka pale tutakapopata vyombo vya usalama vyenye kufanya kazi kitaalam zaidi ya kuwa wanasiasa.
 
Back
Top Bottom