Wahindi wawili wafia hotelini Dar | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wahindi wawili wafia hotelini Dar

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Makaayamawe, Jun 9, 2009.

 1. Makaayamawe

  Makaayamawe JF-Expert Member

  #1
  Jun 9, 2009
  Joined: Feb 21, 2009
  Messages: 341
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Wahindi wawili wafia hotelini Dar

  Na Mwanaidi Swedi
  8th June 2009

  Wahindi wawili ambao mmoja ni raia wa Canada na mwingine wa Afrika Kusini wamekutwa wamefariki dunia katika mazingira ya kutatanisha ndani ya vyumba vya hoteli ya Harbours View iliyopo kwenye jengo la JM Mall Jijini.
  Kamanda wa Polisi katika Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Seleiman Kova, ameiambia Alasiri leo asubuhi kuwa miili ya wahindi hao ilikutwa katika vyumba tofauti vya hoteli hiyo, majira ya saa 8:00.

  Akielezea zaidi, Kamanda Kova amesema kuwa Polisi walipata taarifa toka kwa Meneja Masoko wa hoteli hiyo aitwaye Bw. Laizer Manukwa, aliyeeleza kuwa usiku, kuna mteja wao aliyekuwa chumba namba 10-12, aliyefahamika kwa jina la Sulman Zuber, 41, Mhindi aliye raia wa Canada, alikutwa akiwa amekufa chumbani humo.

  Kamanda akasema kuwa katikaƄ tukio jingine lililojiri hotelini hapo, ilibainika kuwa katika chumba 12- 09, ghorofa ya pili, mtu aitwaye Nickel Kumar Taluar, 33, raia wa India, alieleza kuwa mpangaji mwenzie ambaye pia ni mhindi aitwaye Yusuf Seda, raia wa Afrika Kusini, alikutwa pia amefia chumbani kwake.

  Aidha, Kamanda Kova akasema kuwa vifo vya watu hao wanaodaiwa kuwepo hotelini tangu Mei 19 mwaka huu havionyeshi kuwepo na purukushani yoyote kabla ya kutokea kwake.

  Hata hivyo, akasema taarifa za awali toka kwa uongozi wa hoteli hiyo zinaonyesha kuwa watu hao walirejea jana alfajiri toka kwenye sehemu za starehe na kwamba kuna wakati, mwingine alionekana kwenye maeneo ya Casino ya hotelini hapo.

  Akasema inawezekana walikuwa wamezidisha vinywaji walipokuwa katika maeneo hayo.

  Akasema kutokana na tukio hilo, Polisi wameunda timu ya wataalam mbalimbali akiwemo Mkemia Mkuu na Daktari ili kuweza kubaini chanzo cha vifo vya watu hao.

  Akasema upelelezi unaendelea na hadi sasa hakuna aliyekamatwa kuhusiana na tukio hilo.
   
 2. Makaayamawe

  Makaayamawe JF-Expert Member

  #2
  Jun 9, 2009
  Joined: Feb 21, 2009
  Messages: 341
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Kuna nini wanachokikimbilia hawa wahindi na kukutania huko kwa Wadanganyika? Hivi huko serikalini/ usalama wa taifa hakuna hata anayekuna kichwa?
   
 3. R

  Rwabugiri JF-Expert Member

  #3
  Jun 9, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 2,777
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135


  Mhhh.. sasa huyu aliye andika hii habari naye tumuite mbaguzi? kwa vile kasema wahindi wawili.. pengine angesema watu wawili wenye asili ya Asia.. (sorry wakuu naona ndivyo wabongo tunavotakiwaga tuseme hasa tunapo zungumzia wageni nchini kwetu!)
   
 4. H

  Hauxtable JF-Expert Member

  #4
  Jun 9, 2009
  Joined: Nov 5, 2007
  Messages: 386
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  tusubiri taarifa za huo uchunguzi.....
   
 5. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #5
  Jun 9, 2009
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,159
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Yaani wote wawili wazidiwe na kilaji kiasi cha kupoteza maisha......!
   
 6. W

  WildCard JF-Expert Member

  #6
  Jun 9, 2009
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Sio tu ni mbaguzi bali pia mnyanyapaaji. lugha ya Kitanzania sio hiyo. Zeruzeru tunawaita walemavu wa ngozi; bubu walemavu wa ulimi; viziwi tunawaita wasiosikia; hani*** tunamwita sio rizki.....
   
 7. Makaayamawe

  Makaayamawe JF-Expert Member

  #7
  Jun 9, 2009
  Joined: Feb 21, 2009
  Messages: 341
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Rwabugiri,

  Lugha iliyotumiwa ni sahihi kabisa.

  Watu wawili wenye asili ya Asia sio sahihi na pia sio lazima wawe wahindi. Wanaweza kuwa yeyote tokea Palestine mpaka Japan.

  Lisilo la kawaida ni kwa Wahindi kufurika nchini na kufia huko kiajabu ajabu.
   
 8. H

  Hauxtable JF-Expert Member

  #8
  Jun 9, 2009
  Joined: Nov 5, 2007
  Messages: 386
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  ......sisi waenda kwa miguu/wapanda dalaX2 twawaita wenye mashangingi mafisadi,wafanya biashara wazalendo twawaita fisadi papa,wasio wazalendo twawaita fisadi nyangumi....
   
 9. Makaayamawe

  Makaayamawe JF-Expert Member

  #9
  Jun 9, 2009
  Joined: Feb 21, 2009
  Messages: 341
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Mhindi akiitwa Mhindi kuna ubaguzi gani? Kama ataitwa G.A.Bacholi labda hapo ndio mtu anaweza akalalamika kulingana na mazingira ya alivyoitwa hilo jina.

  Lakini hapa cha kudadisi ni kwa hao Wahindi kukutania kwenye hoteli moja huko TZ waliyokaa kwa muda mrefu na kufia hapo?

  Je kuna nini walichokifuata hao Wahindi na kujikusanya mahali pamoja licha ya wao kutokea nchi tofauti? Hili linahitaji uchunguzi.
   
 10. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #10
  Jun 9, 2009
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,322
  Likes Received: 1,788
  Trophy Points: 280
  I like the way you have written your comments.imenichekesha sana. Inawezekana tuna kawaida ya kutumia njia ndefu kwenye safari ambayo inawekekana kwa njia fupi. Maana nimefikiria kuwa, hata mtu akiiba, tena akiwa kigogo, ukimwita mwizi unaweza ukaambiwa umekosa heshima mana wezi wako uswazi tu.Wao hawaibi...wanafanyaje sijui??!!
   
 11. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #11
  Jun 9, 2009
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,322
  Likes Received: 1,788
  Trophy Points: 280
  Hii ndo nchi pekee unakuja maskini halafu unaiba big time na kuwa milionea kama umesimama. Siwachukii hawa jamaa ila imefika sehemu tuanze kuwa makini na wanayoyafanya.Wanaiharibu TZ na siku ya kugundua hilo hatutakuwa na wakulia nao maana watakuwa wameenda Canada na UK.Wengi hawana nia nzuri na TZ. period!
   
 12. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #12
  Jun 9, 2009
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Ndiyo hapo mkuu wangu NL. Haiwezekani kuwa wote walikunywa kiasi sawa cha pombe na kuwa stamina ya miili yao ni sawa, na ndipo wakafa. Ukiniambia walikula sumu ya aina moja, nitakubali!!!!!!!! Je ni deal gani lilikuwa hapa, imagine Canada and South Africa!!!! Na wenyeji wao ni akina nani?? Tangu May ni lazima walikuwa na wenyeji wao hapa Tz!!!!!Walikuja kwa kazi au biashara gani??? Kama ni biashara formal ni ofisi gani walikuwa wana-deal nao?? Ni nani close employee wao wa hapo hotelini??? Nyendo zao zilikuwaje i.e in and out hotelini???!!! Walikuwa wanatembelewa na akina nani??? !!!Mbona ni rahisi kupata uchunguzi wake??? Wanipe mimi hiyo kazi???
   
 13. T

  Tujisenti JF-Expert Member

  #13
  Jun 9, 2009
  Joined: May 21, 2008
  Messages: 330
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kusema wahindi wawili na watu wawili wenye asilia ya Asia whats the difference?
   
 14. W

  WildCard JF-Expert Member

  #14
  Jun 9, 2009
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Mbona sioni R.I.P. Wahindi?
   
 15. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #15
  Jun 9, 2009
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Mkuu Wildcard, kuliko niseme R.I.P kwa mhindi afadhali virus wakiweza watafune hii keyboard nishindwe kubonyeza hizi three alphabets!!!! Swine fever ingekuwa selective ningeiomba ije iwatafune wenye sijui uhindi au asili ya kiasia wote!!!! Yaani mnaenda kuharibu mali za mh. Kimaro kwa kutumwa na haohao wenye hizo ngozi kwa kuwa wao ndiyo mafia wa ufisadi halafu eti mnaacha biashara na maduka yao yanapeta huku matusi na unyanyasaji wa vibarua weusi wa tz vinaendelea??? Hapa ndipo, Watz tunaonekana bonge la......malizia.
   
 16. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #16
  Jun 9, 2009
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Nchi hii ni kama SHAMBA LA BIBI! Mtu anaingia anavyotaka na kuchukua anachotaka na kutokomea kusikojulikana. Hakuna wa kumwuliza. Tusubiri tuone ukweli uko wapi juu ya hawa wahindi. Lazima kuna jambo zito!
   
 17. W

  WildCard JF-Expert Member

  #17
  Jun 9, 2009
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Hawa Wahindi hatujaambiwa walikuja kutuibia, wamefikia kwenye hoteli tulizojenga na kuna ajira za watu wetu humo, mmoja niliona amegongwa mhuri wa "Club Bilicanas" kwenye kiganja cha mkono wake. Huko nako walikwenda kutuchangia. Mbona tunakuwa hivi? Au mahubiri ya Mzee wetu Mengi yameanza kutuingia? Xenophobia? chauvinism or racism? Acheni hizo!
   
 18. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #18
  Jun 9, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  kwikwikwikwikwikwi watz wanafiki......
   
 19. R

  Rwabugiri JF-Expert Member

  #19
  Jun 9, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 2,777
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Mkuu wangu tofauti ni kubwa, kwa maana hata wakiwa mafisadi hutakiwi kuwasema kwani kwa kufanya hivo utakuwa unawabagua!

  Hata hivo kwa vile walio kufa ni wageni, na wamefia hotelini hatupaswi kuwachunguza kwasababu tukiwachunguza tutaonekana ni wabaguzi na tutawatisha wageni wengine wasije kulala hotelini nchini kwetu na hivyo tutapoteza mapato kwa nchi! lol!
   
 20. Kilbark

  Kilbark JF-Expert Member

  #20
  Jun 9, 2009
  Joined: Feb 25, 2008
  Messages: 558
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Wao mbona hawataki tuwaoe watoto wao. Wanatuita sisi ma GOLO unajua maana ya GOLO?
   
Loading...