Wanyama Nyumbu nao wanatambua wakati.
Wanatambua majira ya kuishi mbugani Serengeti na mbugani Masai Mara.
Muda wa kutoka mbuga moja Hadi nyingine unakuwa mgumu Sana lakini hukabiliana nao.
Wengine hufa njiani kwa kulia na Mamba wanapovuka Mito, wengine hufa kwa uchovu wa safari, wengine huliwa na wanyama walanyama.
Ni safari ngumu lakini kwakuwa wanatambua wakati hulazimika kuitana kujikusanya na kuikabiri safari.
Wanyama wakufugwa nao huwa wanawatambua wanao wafuga.
Mbwa humtambua mfugaji wake, anayempa chakula.
Kama anavyotambua myama Paka, au Ng'ombe au Mbuzi au Punda.
Tunashindwaje sisi, sisi tuliojaaliwa busara na hekima...!
Sisi wenye wingi wa Maarifa, wingi wa Busara, wingi wa Akili, wingi wa Hekima.
Sisi tunashindwaje kuvumilia safari kama Nyumbu.
Au kumtambua Bwana anayetupa mahitaji kama Punda anavyomtambua anayemfuga...!
Kwanini sio sisi na kwanini ni sisi...!
Sisi binadamu