Chuma hunoa chuma

Chuma hunoa chuma

Vita dhidiyaujinga

JF-Expert Member
Joined
May 15, 2026
Posts
325
Reaction score
436
CHUMA HUNOA CHUMA

1.Je, ulishawahi kijiuliza ni kwanini MP4 file haisomi kwenye MP3 device na inaonekana kama kirusi?

2.Je, unajua kuwa MP4 device huwa inajitahidi kusoma formats zote kwa kutumia program tofauti na namuna tofauti?

3.Je, unafikiri kwanini kifaa chenye uwezo mdogo (mfano simu ndogo ya tekno) kinaonyesha faili kubwa kuwa kama kirusi au haiwezi kufunguliwa lakini kifaa chenye uwezo mkubwa (mfano simu janja ya Tecno) kinahakikisha faili husika linasomeka kulingana na aina yake na siyo kuliita kirusi?

Huenda maswali hayo ni magumu na ninafikiri kutokana na majibu juu ya maswali ya apo kabla utagundua ni kwanini kuna sehemu ulikataliwa au unakataliwa na kuonekana mjuaji, mtu unayejifanya mkamilifu, mtu unayejifanya umeokoka kuliko wote, mtu ambaye kauli zako zina utata, mtu ambaye unajiinua nk

Kwa yote naomba ujue kuwa siyo kosa lako lakini pia huenda ni kosa lako

-Matukio yamefungwa kwenye nyakati/majira pamoja na uendano (parity) pengine siyo wakati sahihi wewe kukubalika na hapo siyo mahala sahihi wewe kuwa

Tupite hapa kwa rejea zaidi kwanza
Biblia Mithali 27:17
Chuma hunoa chuma; Ndivyo mtu aunoavyo uso wa rafiki yake.

Biblia Mhubiri 3:1
Kwa kila jambo kuna majira yake, Na wakati kwa kila kusudi chini ya mbingu.

Ninachoandika hiki kinaweza kukusaidia unayemuamini Mungu katika KRISTO YESU na wewe usiyemwamini Mungu katika KRISTO YESU lakini itakuwa ngumu sana kwa usiyemwamini Mungu katika KRISTO YESU kuyahifadhi (to maintain/to contain them) maana unahitajika msaada wa ziada unaopita akili zote

Ina,...sikiliza...Mwamini YESU KRISTO BWANA Leo upate ondoleo la dhambi na kuweza kuzikabiri shida na raha kwa umakini mkubwa
 
Back
Top Bottom