Waheshimiwa wabunge tusaidieni walimu

Waheshimiwa wabunge tusaidieni walimu

JEMEDARI .H.

JF-Expert Member
Joined
Oct 29, 2012
Posts
341
Reaction score
63
Naomba nichukue fursa hii niwaombe wabunge watusaidie walimu kwani inauma sana hatusikilizwi kwani tunachohitaji ni nyongeza ya mishahara tu.Acheni unafiki wa kuongelea yasiyo na msingi(ukaguzi,mitaala) TUNATAKA MISHAHARA IPANDE la sivyo zuia bajeti
 
Haina haja ya ulalamika, kama wamepata suluhisho la matokeo mabaya kisiasa siasa, basi jibu litaonekana mwakani. tulia
 
Me naumia pale ninapoona sababu ya wanafunzi kufeli hawasemi walimu wamekosa morali,sasa nakerwa sana maana hata pinda alisema "hicho wanachokiita mshahara".
 
Ah..hawakusikii bhana temananao watakaokusikia labda ni CDM na unaelewa wapo wachache bungeni na walimu wamekataa kupigia kura CCM ing'olewe madarakani maana yameshiba sana.
 
Kiukweli inaumiza sn...walimu kwenye nchi hii tumefanywa matambala ya deki, "yaani tambala linasafisha nyumba hadi inang'aa there after linafichwa mbali kbs na halitakiwi kuonekana kbs" walimu wa nchi hii hawathaminiwi,wanapuuzwa,wanadharauliwa,wanakejeliwa na kunyanyaswa wazi wazi....CCM na serikali yenu tambueni sisi ndo tunazalisha wataalamu wote na hata raia wa kawaida sisi ndo tumewalea na kuwapa maarifa na uelewa hata wa kujua umuhimu wa kulipa kodi,kupiga kodi na elimu y kawaida ya kiraia. CCM ACHENI UNAFIKI,HIVI NI KWELI HAMJUI KUWA WALIMU TUNAMAISHA DUNI?? SERIKALI HIVI HAMJUI KUWA WALIMU HATUNA MAKAZI?? NYIE CCM NA SERIKALI YENU HIVI NI NANI ASIYEJUA KUWA WALIMU HATUNA ARI YA KUFANYA KAZI KUTOKANA NA UDUNI WA MAISHA?? Hakika CCM eleweni kuwa MUNGU atawalaani kwa DHULUMA na UDHALILISHAJI munaotufanyia walimu...TUMEWALALAMIKIA SN,TUMEWAOMBENI SN, TUMEWABEMBELEZENI SN ILA HAMTAKI KUSIKIA KILIO CHETU ....Sasa tunasema cha kufanya tunajua, TUNAMWAGA MBOGA SASA!!
 
Ulishaambiwa na hawa ndugu zako kuwa kama unauona ualimu haukufai we jiondokee, na pia ulishaambiwa na mzee mkubwa kuwa hata usipompa kura yako hakuongezei mshahara ng'oo! Walimu wameshindwa kujua jinsi ya kudai haki yao. Watakapojua namna ya kudai wataongezewa. Acheni lawama,unganeni kuidai haki yenu.
 
Ulishaambiwa na hawa ndugu zako kuwa kama unauona ualimu haukufai we jiondokee, na pia ulishaambiwa na mzee mkubwa kuwa hata usipompa kura yako hakuongezei mshahara ng'oo! Walimu wameshindwa kujua jinsi ya kudai haki yao. Watakapojua namna ya kudai wataongezewa. Acheni lawama,unganeni kuidai haki yenu.

Sasa hivi Walimu wameacha kazi kama walivyo ambiwa na mukulu na hivyo kubakia na Ajira tu.Ndio maana matokeo wanafinyanga kila kukicha
 
Wanao umia ni watoto wa walipa kodi wao watoto wao wanasoma kama sio shule za nje basi ni shule za st. Francis ninaombea sana laana hii iwakute hawa mafisadi 2015 walimu tuungane hakuna dawa waondoke 2015 pengine tutapata nafuu
 
Bado sio suluhisho. Taifa halijali kufeli kwa wanafunz wake, itawapeleka advance hata wenye zero na kamshahara ka walimu katabaki palepale. Hivo kuacha kufundisha haitoshi, unganeni, pazeni sauti zenu ili ijulikane kuwa ikifika tarehe 5 mnakuwa mshamaliza tuhela mnavyopata.
 
Back
Top Bottom