Wahaya sio masikini kama watu wanavyodhani

mambo_safi

Senior Member
Jul 22, 2019
147
392
Hicho kiwango kinachoingia TRA (serikalini) kinatoka moja kwa moja mikononi mwa wahaya! Hakitokani na makampuni au watu wachache kuhodhi uchumi na serikali kupata hela juu kwa juu ambazo hazihakisi hali halisi ya maisha ya wananchi husika! Hivi mlishawahi kutembelea mkoa wa kagera mkalinganisha na hali ya maisha ya baadhi ya mikoa? Nawapa mfano:

Waleta mada wengi hapa jukwaani hawajawahi kutembea! Ulishawahi kwenda na kuona maisha ya watu wa shinyanga ndani ndani au hata viunga vya mji wa shinyanga? Nenda utaniletea mrejesho! Makusanyo ya kodi (TRA) ya shinyanga yanatokana na wingi wa kodi ya migodi.

Hela ya migodi haiingii mikononi mwa wananchi inaenda mojakwamoja katika kapu la serikalini na inakwenda kujenga miundombinu katika mikoa yenye ushawishi wa utashi wa kisiasa na kuacha hali ya maisha ya watu wa shinyanga wakiwa fukara! Wakileta takwimu wanasema shinyanga hiko juu lakini angalia wananchi wake hoi taabani.

Mkoa wa kagera tangu henzi za mwalimu serikali haijawahi kuwekeza! Sasa itachuma mahali ambapo hawajawekeza? Wahaya walijitahidi na wanajitahidi kadri ya uwezo wao kutumia kidogo walichonacho kusapoti watu wao! Kwataarifa yako hicho kidogo kinachoonekana serikali inakipata kinatokana na shughuri za moja kwa moja za wanakagera sio makampuni au taasisi kubwa zinazohodhi uchumi na kuwaacha wananchi fukara!

Nikuulize tena swali hapa jukwaani! Kila mtu aangalie mtaani kwake ni wahaya wangapi masikini? Wahaya ni kabila lililo juu katika hali bora ya maisha na wanakimbizana na wachaga.
 
Wahaya sio masikini foolstop! And will never! Hustlers wanazopitia wangekuwa weak (dhaifu) wangekuwa wameisharun into extinction! Hawa jamaa wako vizuri upstairs! Serikali tangu mwalimu haijawahi kuwasapoti wanakagera hata serikali ikitaka viongozi wa kihaya lazima wachague wale ndumilakuwili wasio na uchungu na mkoa wao!
 
Simfahamu mhaya tajili, ila najua wengi ni wafanyakazi na wasomi, tuje kwenye ukweli kuna mahusiano ya usomi na utajili, kama upo basi wahaya tajili, ila ukweli wahaya wengi ni maskini.
 
Wahaya ni matajiri wa sifa na manebo na mbwembwe ila kiuhalisia ni nasikini sana,Bukoba mjini pa kawaida sana,vijijini mmejitahidi kujenga,ila hata ndege hujenga viota,mfukoni hamna kitu
 
Hicho kiwango kinachoingia TRA (serikalini) kinatoka moja kwa moja mikononi mwa wahaya! Hakitokani na makampuni au watu wachache kuhodhi uchumi na serikali kupata hela juu kwa juu ambazo hazihakisi hali halisi ya maisha ya wananchi husika! Hivi mlishawahi kutembelea mkoa wa kagera mkalinganisha na hali ya maisha ya baadhi ya mikoa? Nawapa mfano:

Waleta mada wengi hapa jukwaani hawajawahi kutembea! Ulishawahi kwenda na kuona maisha ya watu wa shinyanga ndani ndani au hata viunga vya mji wa shinyanga? Nenda utaniletea mrejesho! Makusanyo ya kodi (TRA) ya shinyanga yanatokana na wingi wa kodi ya migodi.

Hela ya migodi haiingii mikononi mwa wananchi inaenda mojakwamoja katika kapu la serikalini na inakwenda kujenga miundombinu katika mikoa yenye ushawishi wa utashi wa kisiasa na kuacha hali ya maisha ya watu wa shinyanga wakiwa fukara! Wakileta takwimu wanasema shinyanga hiko juu lakini angalia wananchi wake hoi taabani!

Mkoa wa kagera tangu henzi za mwalimu serikali haijawahi kuwekeza! Sasa itachuma mahali ambapo hawajawekeza? Wahaya walijitahidi na wanajitahidi kadri ya uwezo wao kutumia kidogo walichonacho kusapoti watu wao! Kwataarifa yako hicho kidogo kinachoonekana serikali inakipata kinatokana na shughuri za moja kwa moja za wanakagera sio makampuni au taasisi kubwa zinazohodhi uchumi na kuwaacha wananchi fukara!

Nikuulize tena swali hapa jukwaani! Kila mtu aangalie mtaani kwake ni wahaya wangapi masikini? Wahaya ni kabila lililojuu katika hali bora ya maisha na wanakimbizana na wachaga!
Utajiri unapimwa pia katika uzalishaji. Je, mkoa wa Kagera mnazalisha kahawa na ndizi kiasi gani? Ng'ombe kiasi gani? Mahindi je?
 
bahati mbaya usomi huwa hauendani na utajiri. wasomi wengi ni maskini na wakijitahidi sana huwa middle class. ila sio matajiri.
Hii ni Tanzania tu kwa mfumo wetu ulivyo...ila uko ulimwenguni wasomi wemgi ni matajiri

Na hii ndo maana Tanzania bado ni third world kwa sababu hailei wasomi matajii
 
Utajiri unapimwa pia katika uzalishaji. Je, mkoa wa Kagera mnazalisha kahawa na ndizi kiasi gani? Ng'ombe kiasi gani? Mahindi je?
Kagera inazalisha
70% ya kahawa yote
80% ya ndizi zote
25% ya maharage
80% ya vanilla..

Ukitaka takwimu nitakupa
 
Simfahamu mhaya tajili, ila najua wengi ni wafanyakazi na wasomi, tuje kwenye ukweli kuna mahusiano ya usomi na utajili, kama upo basi wahaya tajili, ila ukweli wahaya wengi ni maskini.
Hiv ukiachana na mfuruki ( mhaya) na mengi kuna mweusi gani alishawahi ingia hata top ten ya matajiri nchi kadri ya forbes?
 
Hii ni Tanzania tu kwa mfumo wetu ulivyo...ila uko ulimwenguni wasomi wemgi ni matajiri

Na hii ndo maana Tanzania bado ni third world kwa sababu hailei wasomi matajii
maprofesa na PHD holders dunia nzima sio matajiri, ni middle class. na hii inatokana na uelewa mwingi unaowafanay wawe concious kwenye kutake risks. hawajilipui, wanaforesee hasara na kupiga mahesabu hata kabla mradi haujaanza. ila wale wanaoenda kama kichwa hakiko vizuri wanajilipua tu, huwa wanapata hasara hawakati tamaa wanarudia tena mwisho wanadondokea kuwa matajiri wakubwa sana. then wanageuka kuwaajiri hao akili kubwa waendeshe makampuni yao.
 
Kagera inazalisha
70% ya kahawa yote
80% ya ndizi zote
25% ya maharage
80% ya vanilla..

Ukitaka takwimu nitakupa
ndizi hazitoki kagera tu, kilimanjaro kuna ndizi sana, mbeya pia kuna ndizi kulisha nyanda za juu kusini yote. ndizi za karega zinaishia mikoa ya kati, haziendi mikoa ya arusha na kilimanjaro wala Tanga. pia, maharagwe, mikoa ya kusini kama mbeya, iringa, songea wanalima sana kuliko bukoba. vanila nakubaliana na wewe. kahawa, umesahau mkoa wa kilimanjaro wanalima kahawa kuliko bukoba. nilishawahi kufanya kazi world vision miaka ile ya ukimwi mwingi bukoba, naijua sana, wanahitaji msaada mkubwa sana, ni masikini sana.
 
Ngoja nilete takwimu sasa...

Tuanza na kahawa...hii ilikuwa 2020 60% ya kahawa yote ni kagera

Acha ubishi...
Takwimu nyingine naleta
JamiiForums1758935727.jpg
 
Back
Top Bottom