Wahariri wamemtendea haki Lema,wapinzani na watanzania kwa ujumla

Salary Slip

Platinum Member
Apr 3, 2012
49,068
151,315
Magazeti karibu yote ya leo yametawaliwa na hotuba ya Lema na wahariri wamejaribu kuueleza umma sababu hasa za hotuba ya Lema kuzuiwa kusomwa Bungeni.Habari za serikali Bungeni magazeti mengi ya leo yamezipa kisogo katika kurasa za mbele.

Magazeti yaliyotawaliwa na habari za hotuba ya upinzani katika kurasa zake za mbele ni The Citizen, Majira, Mtanzania, Mwananchi, Raia Tanzania,Tanzania Daima, Nipashe,The Guardian na Jambo leo.

Serikali kama mnadhani kuzuia shughuli za Bunge kurushwa live mnakomoa wapinzani,basi mjue mnajidanganya na uamuzi wenu huu naweza nikasema umeanza kuwa "counterproductive kwenu".
 
Siku hizi hawana zile za kununua magazeti yoote kabla hayajatoka au kwenda hack production ya gazeti lisitoke?? Hizo alikuwa anafanya sana RA! Naona umafia ule wa pesa na nguvu za dola naona umepungua sana! Walikuwa wanamtumia sana Kova kwa madude kama hayo!
 
Ilibidi iwe hivyo maana hakuna namna, hili bunge lijitazame upya maana huu mwendo ni kama viongozi wake wamewekwa pale ili kulipa fadhilia za nafasi walizokalia.
 
Magazeti karibu yote ya leo yametawaliwa na hotuba ya Lema na wahariri wamejaribu kuueleza umma sababu hasa za hotuba ya Lema kuzuiwa kusomwa Bungeni.Habari za serikali Bungeni magazeti mengi ya leo yamezipa kisogo katika kurasa za mbele.

Serikali kama mnadhani kuzuia shughuli za Bunge kurushwa live mnakomoa wapinzani,basi mjue mnajidanganya na uamuzi wenu huu naweza nikasema umeanza kuwa "counterproductive kwenu".
Ni vigumu kuwafanya watz wote ni wajinga. Huyu Lugumi atashusha sana heshima ya serikali hii!
 
Walivyo mabwege hawatashindwa kuzuia magazeti yasisomwe kwenye TV na radio, maana wanajitahidi sana kuturudisha enzi ya ujima, na mbaya zaidi kuficha ufisadi wa viongozi wanaojipambanua wanatumbua majipu, kumbe wanatumbua vipele.
wanahangaika tu, ukweli utabaki kuwa ukweli tu...
 
9d325bbf5044be8f1df12ce4dd0e8296.jpg
 
Magazeti karibu yote ya leo yametawaliwa na hotuba ya Lema na wahariri wamejaribu kuueleza umma sababu hasa za hotuba ya Lema kuzuiwa kusomwa Bungeni.Habari za serikali Bungeni magazeti mengi ya leo yamezipa kisogo katika kurasa za mbele.

Hao wahariri wote ukiwadaka na kuwaburuza mahakamani hachomoki hata mmoja.Hotuba ya Lema haikusomwa ina maana kisheria haipo!! Sababu Hotuba iliyopo bunge ndio lenye wajibu kisheria wa kuitoa na kuiweka kwenye Hansard!!

Hiyo waliyoweka magazetini si hotuba ya Lema ni hadithi za kutunga walizotunga wahariri.Mtu yeyote aliyeumizwa na habari zilizoandikwa aweza kuwaburuza mahakamani na akawashinda hao wahariri na wakamlipa mabilioni ya bure.
 
Back
Top Bottom