JAMHURI
JF-Expert Member
- Dec 15, 2010
- 449
- 60
Wahamiaji haramu wawili wafungwa jela
Na, MOHAMED HAMAD-KITETO.
Mahakama ya hakimu Mkazi Wilayani Kiteto Mkoani Manyara imewatia hatiani Wahamiaji Haramu wawili raia wa Ethiopia kutumikia kifungo cha miezi nane jela kila mmoja kwa kosa la kuingia nchini kinyume cha sheria.
Mwendesha mashitaka wa jeshi la Uhamiaji, mkaguzi msaidizi wa uhamiaji Kiteto, Mmasa Samweli Omari, aliwataja kuwa ni Bw. Barakat Gatebo Anose na Mokone Gabure Dakebu, wote raia wa Ethiopia.
Mbele ya hakimu mkazi wa Mhakama hiyo Mmasi alieleza mahakamani hapo kuwa watuhumiwa hao walikamatwa kutokana na ushirikiano mzuri uliopo baina ya kampuni za mabasi ya abiria na vyombo vya ulinzi na usalama wilayani Kiteto.
Raia hao wa kigeni walikuwa wanasafirishwa kwa basi la kampuni ya Struggle linalofanya safari za Arusha-Kiteto na walifikishwa kituo cha Polisi Kiteto baada ya kutiliwa mashaka.
Katika hatua hiyo raia wa Tanzania Bw. Abdul Ramadhani Gilo mkaazi wa Wilaya ya
Kondoa mkoa wa Dodoma, amefunguliwa mashtaka ya tuhuma kujihusisha na biashara ya kusafirisha Wahamiaji Haramu kinyume na Kifungu cha 46 (1) (c) na (g) cha sheria ya Uhamiaji Sura ya 54, rejeo la mwaka 2018.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Uhamiaji Kiteto, Ikomba Mathew nje ya mahakama alitaja mafanikio ya kukamatwa watu hao kuwa ni matokeo ya mpango endelevu wa elimu kwa umma kuhusu madhara ya wahamiaji haramu katika usalama na maendeleo ya nchi pamoja na ushirikiano mzuri wa utendaji baina ya vyombo vya ulinzi na usalama.
Alitoa wito kwa wananchi Wilayani Kiteto kuwa wazalendo na wenye mapenzi mema na nchi yao, kuepuka kujihusisha na biashara hiyo haramu ambayo madhaya yake ni makubwa kwa mtu mara inapothibitika kufanya kazi hiyo.
Mwisho.