Wahamiaji haramu wamiminika Rukwa

Wahamiaji haramu wamiminika Rukwa

BabuK

JF-Expert Member
Joined
Jul 30, 2008
Posts
1,845
Reaction score
330
MKOA wa Rukwa bado unaendelea kusumbuliwa na wimbi la wahamiaji haramu kutoka nchi jirani za Congo DRC, Burundi, Zambia, Uganda na Rwanda imeelezwa.

Kamanda wa Uhamiaji Mkoa wa Rukwa, Wilson Bambanganya alisema kutokana na wimbi hilo, wahamiaji haramu 391 walikamatwa kati ya mwaka jana na mwaka huu.

Aidha alisema wahamiaji haramu 172 walirejeshwa makwao.

Alisema kuwa changamoto wanazokabiliana nazo ni pamoja na vituo vya uhamiaji kuwa katika hali mbaya na chakavu sana. Aidha, alisema kuna tatizo la usafiri hasa vya mwambao wa Ziwa Tanganyika ni kubwa.

Wakati wa ziara ya Makamu wa Rais, Dk Mohamed Gharib Bilal akipewa taarifa ya mkoa, Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya alimfahamisha kuwa kunakisiwa kuwapo kwa wahamiaji haramu 20,000 mkoani humo.

Chanzo- HabariLeo
 
Back
Top Bottom