Wahamiaji haramu 79 watiwa mbaroni

Wahamiaji haramu 79 watiwa mbaroni

Safiiii sasa hivi ndo tuna serikali kah lilikuwa dampo mtu anakuja anaanzisha makazi kaaa kwao kesho mnakutana njia anakusalimia kidhungu unamuona kaenda shule kumbe mkenya na wabongo wakisikia how ar u wanaona ohhhh huyu si mwenzetu kasoma huyu kumbe mkenya aiisee balaaaaaa
 
Ikumbukwe hawa watu hawafukuzwi ila wanatakiwa wafate sheria zetu, hata raia wetu akikamatwa anazubaa mjini atashikwa tu aulizwe anafanya nini huku mbona anazagaa tu, sasa wageni waje kihalali hakuna atakayewabughudhi. Nilishawahi kukataliwa kupewa huduma kwenye hospital ya serikali kwa sababu nilikuwa na tourist visa na waligoma wakadai labda niende private huko.
 
Mbona hatuwataji fulani na fulani wapo mahali fulani hamjawakamata. Kwa nini tunataka kuwa watu wakulia lia?
 
Wilaya ya Kaliua wapo kibao ila watu wa uhamiaji wamegeuza wakimbizi ATM. Wakiishiwa wanaenda wapiga biti wanapewa mpunga jamaa wanaendelea kupeta.
 
Uonevu tu. Na nchi nyingine wakisema wafukuze watanzania tutapona
Mkuu kwenye sheria hakuna Deko wala mahaba,wafate tu sheria waendelee "kutesa" bongo hayo ya nchi nyingine ni ya Ngoswe tumuachie mwenyewe Ngoswe.
 
pale chuo kikuu cha kimataifa kampala mbona wapo wengi sana ina maana hamjawaona
Hizi ni drama eti mhindinmmoja.. Ha ha haha hh uhamiaji nashauri ifumuliwe haluna kitu pale.. Haya maigizo mchana kweupeee
 
Hawa wapo kibao hapa huawei Tz HQ, wameshajipatia hadi uraia kwa njia ya magumashi na mbaya zaidi huyo anayehangaika kuwatafutia uraia ni mkenya na wanamlipa vizuri anaitwa bea
Nchi ishakuwa ya kisengerema tayari.
 
Hii kamata kamata feki hakuna Mkenya hata mmoja.
 
Uonevu tu. Na nchi nyingine wakisema wafukuze watanzania tutapona
Sio uonevu ndugu yangu kwani haukusikia watu wa south Africa walivyokuwa wanawafukuza wageni sababu wanafanya kazi ambazo wao wanaweza kufanya mfano petrol station so wawafukuze tu Kama wanapenda Tanzania wafate process Kama wengine
 
Hawa watanzania waliokamatwa kama makuwadi kuwapeleka mabint wetu arabuni ni pamoja na yule akiyekuwa mbunge wa tmk? Kama yule hawajamkamata basi hii ni batili.
 
Watu 79 wamekamatwa na Idara ya Uhamiaji nchini kwa kosa la kuishi nchini bila vibali na kufanya kazi wasizo na taaluma nazo. Akizungumza na gazeti hili jana, Naibu Kamishna wa Uhamiaji Dar es Salaam, John Msumule alisema watuhumiwa hao wanatoka katika nchi 15.

Nchi hizo na idadi ya wahamiaji haramu ni Nigeria (4), China (20), Ethiopia (23), Korea (9), Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo-DRC (6), Somalia (3),Uganda (2), Madagascar (5), Burundi (2), Ivory Coast (1), Lebanon (1), India (1), Zimbabwe (1) na Ghana (1).

Alisema katika ‘kamata kamata’ hiyo pia wamefanikiwa kukamata Watanzania watatu, ambao wamekuwa wakijishughulisha na kukusanya, kuwahifadhi na kuwasafirisha wasichana kuwapeleka nchi za mbali, kwa ajili ya kufanya kazi mbalimbali.

“Tumewakamata wasichana sita ambao walikuwa wamekusanywa na watanzania hao ili kusafirishwa na tutawachukulia hatua za kisheria ili kutoa fundisho kwa wengine wenye nia ya kufanya mtindo kama huu,” alisema Msumule.

Aliongeza kuwa idara hiyo imewarudisha nchini mwao wahamiaji 23 raia wa Ethiopia na watuhumiwa nane wa nchi mbalimbali,wamefikishwa mahakamani. Alisema shughuli ya kuwarejesha raia wengine katika nchi zao zinaendelea.

Msumule aliwataka wamiliki wa nyumba za kulala wageni na nyumba za kupanga, wahakikishe wanatambua wateja wao ni raia wa wapi na anafanya kazi gani, kabla ya kufanya naye mkataba wa aina yoyote.

Aliwataka pia watanzania wanaooa na kuolewa, wahakikishe wanafahamiana na mtu huyo na kumchunguza kujua anakotoka na yupo nchini kwa kazi gani, la sivyo mtu akibainika anaishi na mhamiaji, anaweza kujiingiza katika matatizo.

“Sisi hatutajali, tutamkamata kwa kosa la kumhifadhi kwa hiyo lazima wajenge dhana ya kuwachunguza watu hao, hata wasichana wa kazi za ndani, lazima umjue vizuri na sio unamchukua tu bila kujua historia yake ,” alisema.

Msumule aliwataka raia wengine ambao hawana vibali vya kuishi nchini, waondoke wenyewe na wasisubiri hadi sheria ichukue mkondo wake. “Wapo wengi, tunachoomba waondoke wenyewe bila kushurutishwa, wengine wanafanya kazi ambazo hata watanzania wanaweza kuzifanya, wakubali na waondoke,” aliagiza.
Vipi kinanaa hayupo kwenye huo mkumbo?
 
Unadhani Nchi nyingine unaweza ishi bila kibali?
Tembea uone, UK hata siku 2 haziishi ukarudishwa ulikotoka.
Vipi yule mzee wa binduki kiunoni wa tabora kapona kweli?
 
Kwenye makampuni ya simu wamejaa kibao, wamefrustrate Watanzania na kajaza wahindi kibao. Kipindi cha uongozi wa kaburu kazi zilifanywa na Watanzania kwa kiwango cha juu, akaja dalali anaitwa Nokia Siemens 'NOKIA' kufanya yake, control center Kahama Shia India Chenai, huku kakata ajira. Ni mengi, anafanya hadi udalali kwa Vodacom kula cha juu kwenye mishahara ya Watanzania kwa kupitia makampuni ya ndani.
 
Back
Top Bottom