Wahalifu 20 wavamia Makao Makuu ya Tume ya Haki za Binadamu nchini Kenya

Wahalifu 20 wavamia Makao Makuu ya Tume ya Haki za Binadamu nchini Kenya

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
2,439
Reaction score
6,692
Wanaume takriban 20 wenye silaha walivamia makao makuu ya Tume ya Haki za Binadamu nchini Kenya siku ya Jumapili wakati taasisi hiyo ikiwa inajiandaa kufanya mkutano na waandishi wa habari uliolenga kuitaka Serikali ya Kenya kusitisha ukatili dhidi ya raia wake

Kupitia video ya CCTV, wanaume hao walionekana wakiingia kwa nguvu katika kituo hicho, baadhi yao wakiwa wameficha nyuso kwa kuvaa barakoa. Mashuhuda walisema wahalifu hao, kando na kufanya vurugu, pia walipora mali mbalimbali zikiwemo kamera za waandishi wa habari waliokuwa wanajiandaa kuripoti mkutano huo.

Baada ya tukio hilo, Tume ya Haki za Binadamu Kenya ilitoa tamko ikiituhumu Serikali ya Rais William Ruto kuhusika na shambulio hilo na kusisitiza kuwa hawatatishwa wala kunyamazishwa. Na kwamba maandamano yaliyopangwa kufanyika leo yataendelea kama ilivyopangwa.

========================

Full CCTV footage of the moment masked goons stormed the Kenya Human Rights Commission (KHRC) offices in Lavington, vandalized property, and ransacked the facility before disrupting a media briefing that was being held by KHRC reps and activists.

The goons also stole personal items of those they found inside the offices, including media equipment belonging to journalists who were covering the press conference, which was to highlight tomorrow's planned Saba Saba protests.


Source: Buzzroom Kenya
 
Back
Top Bottom