Nimesikitika kuona bungeni mbunge wa mbeya mjini Ng Mbilinyi alikuwa akisema kuwa miongongoni mwa matatizo ya afya ni pamoja na ukosefu wa vifaa tiba mahospitalini akatoa mfano wa mitungi ya gesi kuwa haikidhi mahitaji ya wagonjwa,
Chakushangaza kuna wabunge wakawa wanampinga na kuomba kutoa taarifa kila mara ilimradi kama vile kufanya hoja yake isieleweke!
Sijui kwanini wale wabunge wamefanya vile [emoji87][emoji87]
Taarifa mbali mbali za kitafiti na ni wazi kuwa TZ kuna tatizo la uhaba wa vifaa tiba lakini wao wakawa wanaonesha kupingana na hilo!
Sasa najiuliza kweli kutoka mioyoni mwao wameamua kufanya hivyo?!
Wameenda hospitali za serikali mbali mbali wakaona hali ilivyo?
Je wameenda hospitali za mikoa, wilaya, vituo vya afya, zahanati n.k na kuona hali ilivyo?
Yani sijaelewa hata sasa ule ni ushabiki au ?
Yatupasa kujitafakali na kumuogopa sana Mungu!
Uadilifu ni pamoja na kusimamia ukweli siku zote!
Sent using
Jamii Forums mobile app