Wagombea wa upinzani na utapeli wa kisiasa

Frey Cosseny

JF-Expert Member
Feb 4, 2015
1,984
1,405
UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA: WAPINZANI NA PROPAGANDA NYEUSI

Moja ya kitengo muhimu katika vyama vya siasa ni Kitengo cha Propaganda.

Vyama vingi vya kifidhihina (Conservatives) utumia propaganda nyeusi kufikisha ujumbe kwa wafuasi wao ili kuwarubuni wasing'amue ukweli ya mambo yaliyomo ndani ya vyama vyao.

Propaganda Nyeusi ni mchanganyiko wa ukweli 10% na uongo 90%, ngoja nitoe mfano kidogo.

Wakati wa mchakato wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ilipoanza wapinzani wanajidi kuwa watashinda uchaguzi huu kwasababu Chama cha Mapinduzi hakipendwi na Watanzania. Wakakusanya wapiga propaganda wao maarufu kwenye mitandao ya kijamaii na vyombo vya habari kuwadanganya wafuasi wao kuwa vyama vyao viko imara.

Lakini mchakato ulipoanza ndani ya Vyama vyao hakukua na utaratibu wowote wa kuandaa wagombea wao walichofanya walienda kuwapa fomu watu ambao kimsingi hawakuchaguliwa na wanachama wa vyama vyao kwa mujibu wa taratibu wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, maana yangu hakuna kikao halali kilichofanyika kufanya Uteuzi wa hao wagombea.

Ilipowadiwa zoezi ya kuchukua fomu wakaanzisha sarakasi kuwa wamenyimwa fomu za kugombea cha ajabu ni pale ilipofika zoezi ya kurudisha fomu wakatangazia umma kuwa wagombea wao wamenyimwa fursa ya kurejesha fomu sasa tukabaki tunajiuliza watu waliyonyimwa fomu na watendaji walipata wapi tena fomu za kurejesha?

Kwa kigezo kilekile cha Propaganda Nyeusi wakaaza kuzusha watendaji wa kata wamefunga ofisi na huku wakisambaza picha ya baadhi ya wagombea wa CCM wakisaidiwa kujaza fomu na watendaji kata haya yote walifanya kuonyesha kuwa wanaonewa wao na CCM wanapendelewa.

Zoezi la kuchukua na kurejesha fomu ikaisha ikaanza zoezi la uteuzi sasa ndiyo tena sarakasi nyingine imeanza wagombea wao wameenguliwa unakaa unajiuliza watu ambao hawakupewa fomu ya kugombea, watu ambao hawakupewa nafasi ya kurejesha fomu watendaji walifunga ofisi wasirejeshe fomu hao watu wanapata wapi wagombea wa kuteuliwa?

Vyama vya upinzani hasa ACT Wazalendo, CUF na CHADEMA lazima waelewe kuwa serikali ina wabeba wasijisahu kuwa serikali inawapendelea sana kuliko Chama cha Mapinduzi na mimi nadhani umefika muda sheria ya vyama vya siasa ifanye kazi sawasawa make hii kupendelewa na kuonewa huruma ndiyo inawafanya wajione wana haki.

Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa ifanye kazi zake ipasavyo kusimamia utaratibu ndani ya vyama haiwezekani chama chenye miaka 27 katika Usajili ushindwe kufanya uchaguzi ndani ya chama ndani yake kwa dharau tu.

Kama sheria zitafuatwa kwa uhakika hivi vyama kasuku vinavyofadhiliwa na nchi za Magharibi zitakufa.

ACT Wazalendo mpaka sasa huu ni mwaka wa tatu hawana mwenyekiti wala katibu mkuu, wote waliyopo wana kaimu. Inawezekanaje chama kinachoamini juu ya demokrasia kutokuwa na viongozi wa kitaifa kwa mujibu wa sheria ya vyama vya siasa?

ACT Wazalendo toka alipojiuzulu Komred Samson Mwigamba miaka mitatuiliyopita hawajawahi kumchagua katibu na kwa mujibu wa Katiba yao katibu mkuu ndiye mtendaji mkuu wa chama na anachaguliwa na Halmashauri Kuu ya Taifa ya chama hicho lakini kila Halmashauri Kuu ikikaa inamkaimisha tu.

Kama suala la uchaguzi ni demokrasia kwanini isianzie kwao?

Chama ambacho kinashindwa kuchagua Katibu Mkuu Taifa kinaweza kuwa na vikao vya tawi, kata au wilaya wa kuidhinisha wagombea?

Matokeo yake wameachiwa kazi vijana wanaojifanya wanachama wakitembea kugawa vyeo kwa watu ambao wanategemea kuwaunga mkono katika mchakato wa kugombea ubunge mwakani hatuwezi kuendesha siasa kitapelitapeli hivi.

CHADEMA nacho pamoja na kuwepo kuanzia 1992 lakini wameshindwa kufanya uchaguzi wa kikatiba na kwa mujibu wa Sheria ya Vyama vya Siasa, muda wa uongozi wa CHADEMA kwa mujibu wa katiba yao iliisha toka tarehe 24/9/2019 lakini cha ajabu kwa makusudi kabisa chama icho mwaka huu haijafanya uchaguzi kuanzia ngazi ya chini sasa kama chama haijafanya Uchaguzi wa ngazi ya chini wagombea wao wanapitishwa na kikao gani cha uteuzi wa wagombea?

Chama hakina viongozi ngazi ya chini nani atawaelekeza wagombea wao kujaza fomu kwa usahihi?

Vyama hivi baada ya kugundua kuwa hawana mfumo au organization ya kuwawezesha kufanikisha kuchaguliwa walipanga njama ya kuharibu uchaguzi wakipanga baadhi ya wanachama wao kujifanya kugombea ili waonyeshe kuwa wanaonewa.

Ushauri wangu kwa Serikali Iache kuwabeba vyama vya upinzani, sheria na kanuni zifuatwe kama zilivyotungwa.

Vyama vya upinzani hapa nchini ajenda yao kuu ni kuvuruga amani ya nchi kwa maslahi ya wafadhili wao kutoka nchi za Magharibi.
 
Wanashinda Twitter kupiga majungu

Zitto siasa zake za ulaghai zimefika mwisho sasa
Abweke mwisho mwisho anapojiandaa kukabidhi jimbo
 
matatizo ya kuishi in a pithole country,why chama dola kama kweli wanawafanyia watanzania kile ambacho wengi wetu tunafurahishwa nacho mbona bado wanaweweseka?mbona hawajiamini?uandikishaji wa wapiga kura uliandamana na vitisho vingi mno hasa kwa watumishi wa serikali na mashirika yake maana nilikuwa nategemea kungekuwa na mafuriko ya watu kwenda kujiandikisha maana wananufaika na serikali iliyopo.kama haya ni uongo chama dola fanya yafuatayo just level playing field ya politics nchini,then matokeo yake yataonekana,kura zihesabiwe vituoni na matokeo yake yapelekwe moja kwa moja kwenye kituo kikuu cha ukusanyaji na kuonyeshwa live .siku ambayo middle class yetu itakapotambua yaliyopo na yanayotokea on the ground ndio siku hoja kama hizi hatutaziona.
 
Samahani mkuu ila naona ulicho andika ni Ujinga mtupu. Unasema vyama vya upinzani ni matapeli halafu Chama chako cha CCM kinawaogopa hao matapeli wa Upinzani mpaka wanafunga ofisi na kukimbilia kushinda maporini. Au ule Moshi wa kule Ruangwa umewadhuru wote.
 
Mtoa post nadhani hujafanya utafiti wowote kabla ya kuja na huu upuuzi,lkn nadhani utakua unaishi nje ya Tanzania kwa sababu kwa upande wako na kwa akili yako hujui chochote kinachoendelea hapa nchini kwetu hali iliyopelekea kuja na utumbo wa bata.

Acheni masiala watu wanaumia.Hii Amani ambayo mnaichezea gharama yake ni kubwa sana.Kwa hiyo Chadema ndio walifunga ofisi za watendaji,CHADEMA ndio wamejiengua kwe uchaguzi wa serikali za mitaa,Kweli haya ni madhara ya moshi.
 
UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA: WAPINZANI NA PROPAGANDA NYEUSI

Moja ya kitengo muhimu katika vyama vya siasa ni Kitengo cha Propaganda.

Vyama vingi vya kifidhihina (Conservatives) utumia propaganda nyeusi kufikisha ujumbe kwa wafuasi wao ili kuwarubuni wasing'amue ukweli ya mambo yaliyomo ndani ya vyama vyao.

Propaganda Nyeusi ni mchanganyiko wa ukweli 10% na uongo 90%, ngoja nitoe mfano kidogo.

Wakati wa mchakato wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ilipoanza wapinzani wanajidi kuwa watashinda uchaguzi huu kwasababu Chama cha Mapinduzi hakipendwi na Watanzania. Wakakusanya wapiga propaganda wao maarufu kwenye mitandao ya kijamaii na vyombo vya habari kuwadanganya wafuasi wao kuwa vyama vyao viko imara.

Lakini mchakato ulipoanza ndani ya Vyama vyao hakukua na utaratibu wowote wa kuandaa wagombea wao walichofanya walienda kuwapa fomu watu ambao kimsingi hawakuchaguliwa na wanachama wa vyama vyao kwa mujibu wa taratibu wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, maana yangu hakuna kikao halali kilichofanyika kufanya Uteuzi wa hao wagombea.

Ilipowadiwa zoezi ya kuchukua fomu wakaanzisha sarakasi kuwa wamenyimwa fomu za kugombea cha ajabu ni pale ilipofika zoezi ya kurudisha fomu wakatangazia umma kuwa wagombea wao wamenyimwa fursa ya kurejesha fomu sasa tukabaki tunajiuliza watu waliyonyimwa fomu na watendaji walipata wapi tena fomu za kurejesha?

Kwa kigezo kilekile cha Propaganda Nyeusi wakaaza kuzusha watendaji wa kata wamefunga ofisi na huku wakisambaza picha ya baadhi ya wagombea wa CCM wakisaidiwa kujaza fomu na watendaji kata haya yote walifanya kuonyesha kuwa wanaonewa wao na CCM wanapendelewa.

Zoezi la kuchukua na kurejesha fomu ikaisha ikaanza zoezi la uteuzi sasa ndiyo tena sarakasi nyingine imeanza wagombea wao wameenguliwa unakaa unajiuliza watu ambao hawakupewa fomu ya kugombea, watu ambao hawakupewa nafasi ya kurejesha fomu watendaji walifunga ofisi wasirejeshe fomu hao watu wanapata wapi wagombea wa kuteuliwa?

Vyama vya upinzani hasa ACT Wazalendo, CUF na CHADEMA lazima waelewe kuwa serikali ina wabeba wasijisahu kuwa serikali inawapendelea sana kuliko Chama cha Mapinduzi na mimi nadhani umefika muda sheria ya vyama vya siasa ifanye kazi sawasawa make hii kupendelewa na kuonewa huruma ndiyo inawafanya wajione wana haki.

Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa ifanye kazi zake ipasavyo kusimamia utaratibu ndani ya vyama haiwezekani chama chenye miaka 27 katika Usajili ushindwe kufanya uchaguzi ndani ya chama ndani yake kwa dharau tu.

Kama sheria zitafuatwa kwa uhakika hivi vyama kasuku vinavyofadhiliwa na nchi za Magharibi zitakufa.

ACT Wazalendo mpaka sasa huu ni mwaka wa tatu hawana mwenyekiti wala katibu mkuu, wote waliyopo wana kaimu. Inawezekanaje chama kinachoamini juu ya demokrasia kutokuwa na viongozi wa kitaifa kwa mujibu wa sheria ya vyama vya siasa?

ACT Wazalendo toka alipojiuzulu Komred Samson Mwigamba miaka mitatuiliyopita hawajawahi kumchagua katibu na kwa mujibu wa Katiba yao katibu mkuu ndiye mtendaji mkuu wa chama na anachaguliwa na Halmashauri Kuu ya Taifa ya chama hicho lakini kila Halmashauri Kuu ikikaa inamkaimisha tu.

Kama suala la uchaguzi ni demokrasia kwanini isianzie kwao?

Chama ambacho kinashindwa kuchagua Katibu Mkuu Taifa kinaweza kuwa na vikao vya tawi, kata au wilaya wa kuidhinisha wagombea?

Matokeo yake wameachiwa kazi vijana wanaojifanya wanachama wakitembea kugawa vyeo kwa watu ambao wanategemea kuwaunga mkono katika mchakato wa kugombea ubunge mwakani hatuwezi kuendesha siasa kitapelitapeli hivi.

CHADEMA nacho pamoja na kuwepo kuanzia 1992 lakini wameshindwa kufanya uchaguzi wa kikatiba na kwa mujibu wa Sheria ya Vyama vya Siasa, muda wa uongozi wa CHADEMA kwa mujibu wa katiba yao iliisha toka tarehe 24/9/2019 lakini cha ajabu kwa makusudi kabisa chama icho mwaka huu haijafanya uchaguzi kuanzia ngazi ya chini sasa kama chama haijafanya Uchaguzi wa ngazi ya chini wagombea wao wanapitishwa na kikao gani cha uteuzi wa wagombea?

Chama hakina viongozi ngazi ya chini nani atawaelekeza wagombea wao kujaza fomu kwa usahihi?

Vyama hivi baada ya kugundua kuwa hawana mfumo au organization ya kuwawezesha kufanikisha kuchaguliwa walipanga njama ya kuharibu uchaguzi wakipanga baadhi ya wanachama wao kujifanya kugombea ili waonyeshe kuwa wanaonewa.

Ushauri wangu kwa Serikali Iache kuwabeba vyama vya upinzani, sheria na kanuni zifuatwe kama zilivyotungwa.

Vyama vya upinzani hapa nchini ajenda yao kuu ni kuvuruga amani ya nchi kwa maslahi ya wafadhili wao kutoka nchi za Magharibi.
Kweli akili ni nywele,na kweli wanapendelewa kufunguliwa kesi ,kukamatwa n.k
 
Toa ushahidi wa "amani" kuvurugwa na upinzani.
 
Back
Top Bottom