Wagombea wa udiwani - kanda ya kaskazini hawa hapa

Wagombea wa udiwani - kanda ya kaskazini hawa hapa

Crashwise

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2007
Posts
22,227
Reaction score
8,760
CHMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO – CHADEMA KANDA YA KASKAZINI
(Tanga, Kilimanjaro, Arusha & Manyara)
​

TAARIFA KWA UMMA
WAGOMBEA WA UDIWANI - KANDA YA KASKAZINI
Tarehe 15 Januari 2014, wagombea wafuatao wa CHADEMA walipitishwa na TUME YA UCHAGUZI kuwania nafasi za uwakilishi (UDIWANI) katika maeneo ya kata mbalimbali za kanda ya Kaskazini.

Wagombea hawa walipita katika mchujo wa uteuzi wa chama. Chama kina matarajio makubwa sana kuwa wananchi wa maeneo haya ya kata hizi watapata fursa nzuri ya kuwachagua wagombea wa CHADEMA ambao wana dhamira njema sana na ya kweli katika kuwatumikia.
Wagombea waliopitishwa pamoja na mikoa yao ni:
[TABLE="width: 699"]
[TR]
[TD]JINA LA MGOMBEA[/TD]
[TD]KATA[/TD]
[TD]JIMBO[/TD]
[TD]MKOA[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]BI. MWANAISHA MOHAMED OMARI[/TD]
[TD]KIOMONI[/TD]
[TD]TANGA DC[/TD]
[TD]TANGA[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]BW. KAGOMA FRANK HENRY[/TD]
[TD]KIBORLONI[/TD]
[TD]MOSHI MJINI[/TD]
[TD]KILIMANJARO[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]BW. ALLY BANANGA[/TD]
[TD]SOMBETINI[/TD]
[TD]ARUSHA MJINI[/TD]
[TD]ARUSHA[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]BW. CHARLES SAMWEL MGATA[/TD]
[TD]PARTIMBO[/TD]
[TD]KITETO[/TD]
[TD]MANYARA[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]BW. SANING'O KONE[/TD]
[TD]LOLERA[/TD]
[TD]KITETO[/TD]
[TD]MANYARA[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

Katika uchaguzi huu CHADEMA imejipanga kushiriki kikamilifu sana tukiwa na uhakika kuwa chama kimewapa wananchi wapiga kura chaguo lao kwa kuzingatia uwezo wa wagombea, utayari wa wagombea wetu kushirikiana na kuwatumikia wananchi na dhamira njema ya kutatua matatizo na kero za wananchi zilizoletwa na CCM kwa kushindwa kutimiza wajibu wao.

Aidha chama kimesikitishwa sana na uhuni na ushenzi uliofanywa wa kumteka mgombea wa CHADEMA ndg. ALLY SAIDI JAHA saa nane mchana siku ya tarehe 15.01.2014 muda mfupi kabla ya muda kurudisha fomu kufungwa. Tukio hili limetokea huku tukiwa na taarifa zilizopatikana baadae kuwa mida ya saa nne asubuhi mgombea wetu alifuatwa na kiongozi mmoja wa CCM wa wilaya. Uongozi wa kanda tumesharipoti tukio hili polisi na kupewa RB namba LUS/RB/75/2014 TAARIFA.16.01.2014 ya kutekwa/kupotea kwa ndg ALLY SAIDI JAHA. Hali kadhalika uongozi chama wa Jimbo la Mlalo umeshwandikia barua msimamizi wa uchaguzi kuhusu tukio hili la kutekwa nyara na kupotea kwa mgombea wetu na kuwa baada ya kupata taarifa ya tukio hili kwa kina chake, chama kitakuwa na mahali pa kuanzia.

Hivi sasa tumetuma timu ya intellijensia ya chama kuchunguza kwa kushirikiana na Red Brigade ya wilaya ili kupata undani wa tukio hili ambalo limetufedhehesha sana na ambalo litakuwa limewanyima demokrasia ya kuchagua kwa watu wa Mtae ya kiongozi na chama wanachokitaka.

Niwahakikishie wakazi wa Mtae na Watanzania wote wapenda mabadiliko ambao jambo hili limetukera wote kuwa ndg Ally Saidi Jaha atatafutwa mpaka apatikane akiwa mzima au vinginevyo ili ifahamike nini kimemtokea na pia awaeleze watu wa Mtae na Watanzania wote hili jambo kuna nini nyuma yake. Hapa kuna mtu au watu watawajibika kwa gharama yoyote, hili jambo halitaisha kirahisi hivi hivi.

Niwaombe wakazi wa Kanda ya Kaskazini, kwenye uchaguzi huu tuunganishe nguvu zetu kwa sisi wenyewe kujitolea na muda wetu na rasilimali zetu, ili tuwashughulikie CCM ambao wamekuwa wakiendelea kuwatesa Watanzania kwa sera zao mbovu na uongozi wa kihuni ambao haujali kabisa maisha ya Watanzania.

Imetolewa leo tarehe 16 Januari 2014.
Amani Golugwa
Katibu wa Kanda ya Kaskazini
+255 754 912 914 au 0784 343 275
golugwa@gmail.com
 
Naoma MACHADEMA mmeangalia nyumbani kwenu tu
 
Hili nalo kuwa na mgombea anayetekeka ni tatizo la kukosa umakini. Tutalia sana CCM CCM, lakini kukosekana umakini-Tunapiga sana makelele lakini umakini zero.
 
unawashwa na chuchu, nitafute nitakukuna vizuri, hujickii vizuri bila kuitaja cdm,
Kwa vile mwenyekiti wenu ji mzinifu, kila mwanachama na mfuasi wa chadema anawaza uzinifu tu. pole sana
 
Ukiona kauli kama hizi jua kuna mtu atauwawa kwenye hili sakata.

Wewe kuwajibika kwa gharama yoyote unakokujua ni kuuwawa tu?

Ndio Maana Nchi haiendelei kutokana na Ma-CCM kuogopa kumwajibisha mkosaji KWA GHARAMA YOYOTE. Watu wanaiba then wanaishia kuhamishwa vitengo tu.
 
Siasa za Tz zinaharibiwa na tamaa ya madaraka na kujikomba kwa viongozi wa ccm wilayani, kwa nini wasiache siasa ipite kwenye barabara yake sahihi? Ndiyo maana mkifa watu wanafurahia badala ya kuhudhunika, roho mbaya haijengi acheni kuteka vipenzi vya wapiga kura
 
Naoma MACHADEMA mmeangalia nyumbani kwenu tu

Labda nisaidie kuelewa; CDM ilianzishwa Kaskazini? Makao yake Makuu yapo Kaskazini? Wajumbe wa Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ni kutoka Kaskazini? Hebu nijuze ili nione kama nikuunge mkono kwa hili la ukaskazini wa cdm!
 
Back
Top Bottom