Mtukudzi
Senior Member
- Nov 14, 2013
- 103
- 408
Inaweza kuonekana kama mzaha lakini amini nawaambieni mpaka leo tarehe 28 September 2020 watanzania wameishaamua ni nani awe Rais wao. Kwa hiyo mizengwe vitisho na maneno matamu ya wagombea wetu hayabadilishi maamuzi ya wapiga kura wa mwaka huu.
Taja makundi yote katika nchi hii, yote yaliamua nani wanaenda kumchagua siku ile NEC na ZEC walipotangaza wagombea wa vyama vyote. Kwa hiyo wanaolalamika kutopewa nafasi TBC na media wako sawa tu na wanaofurahi kupewa fursa kwenye vyombo hivyo.
Kwa chama tawala zile live coverage za mgombea wao wakati wote wa miaka 5 iliyopita inatosha kuwapa confidence na kuwaondolea unyonge wa nini kitatokea kwenye sanduku la kura. Kwa wapinzani watanzania wameishamchagua yule ambaye wanaona ni mpinzani halisi na hivyo wapo naye bila kujali itikadi zao ( tumeona Chadema ACT na baadhi ya makada wa CCM, NCCR na CUF).
Kampeni za mwaka huu zimeanza wakati watu wameishachagua upande. Kwa ajili hiyo wagombea Urais punguzeni presha zinazopelekea kuvunja sheria na maadili ya uchaguzi kwa sababu hamtabadilisha maamuzi ya wapiga kura wa safari hii. Kwa taarifa ni kuwa wapiga kura wanatamini iwe hata kesho wawafurahishe.