Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 18,305
- 33,924
Kwa taarifa za uhakika nilizonazo ni kwamba Wagombea wawili wa udiwani kupitia CHADEMA Bw. Andwear Palaiga wa Kata ya Gangilonga na Bw. Godfrey Lufyagila wa Kata ya Kwakilosa wameporwa fomu zao kwa nyakati tofauti na toka maeneo tofauti na watu wasiojulikana.
Inadaiwa kwamba wa kwanza kuporwa fomu hizo ni Godfrey Lufyagile wa Kata ya Kwakilosa ambaye aliingiliwa nyumbani kwake na mtu aliyefunika uso wake jana saa tatu usiku na kumtaka atoe fomu yake ya ugombea kwa usalama wa maisha yake.
Mtu huyo alivyochukua hiyo fomu aliondoka kwa Pikipiki aliyokuja nayo na mtu mwingine.Baada ya tukio hilo Mwenyekiti wa mtaa aliitwa na kupewa taarifa na Lufyagile tayari keshatoa taarifa kituo Kikuu cha Polisi mjini Iringa.
Tukio la pili limetokea leo Asubuhi wakati Mgombea wa Kata ya Gangilonga Bw. Palaiga alipokuwa anatafuta wadhamini kwenye mitaa ya Kata hiyo alipokutana na mtu aliyemnyang'anya begi lililokuwa na fomu hizo za ugombea. Inadaiwa unyang'anyi huo ulitumia silaha aina ya Bastola. Palaiga naye keshatoa ripoti kwenye kituo Kikuu cha Polisi mjini Iringa kwa msaada zaidi.
Uchaguzi kwenye Kata tano zilizo kwenye Manispaa ya Iringa Jimbo la Iringa Mjini unarudiwa baada ya Madiwani waliokuwepo hapo awalil kujiuzulu na kujiunga na CCM.