Uchaguzi 2020 Wagombea Ubunge, Udiwani kuanza kuchukua fomu leo

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Wanachama wa vyama vya siasa nchini leo wanaanza kuchukua fomu za uteuzi kuomba kugombea ubunge na udiwani wakati wa Uchaguzi Mkuu Oktoba mwaka huu.

Hivi karibuni Tume ya Uchaguzi Tanzania (NEC) ilisema kuwa fomu za ubunge zitatolewa kwenye ofisi za wasimamizi wa uchaguzi kwenye makao makuu ya halmashauri na za udiwani kwenye kata husika. Fomu hizo zitatolewa kuanzia leo hadi Agosti 25 mwaka huu.

Kwa mujibu wa NEC kutakuwa na Majimbo ya Uchaguzi 264, yakiwemo 214 Tanzania Bara na Zanzibar kutakuwa na majimbo 50. Pia zipo Kata 3,956 kwa ajili ya uchaguzi wa madiwani.

Chama cha Wananchi (CUF) kimesema wagombea wake wa ubunge na udiwani leo wataanza kuchukua fomu za uteuzi kwenye majimbo na kata zao.

Agosti Mosi mwaka huu NEC ilikutana na vyama vya siasa jijini Dar es Salaam, ambapo pamoja na mambo mengine ilisema fomu za uteuzi za ubunge na udiwani zitatolewa kwenye halmashauri yalipo majimbo na kata.

Mkurugenzi wa Habari, Uenezi, Mahusiano na Umma wa CUF, Mohamed Ngulangwa alilieleza HabariLeo jana kuwa Baraza Kuu la CUF lilikutana Agosti 8 na 9 mwaka huu na moja ya ajenda ilikuwa kupitisha majina ya wagombea ubunge na uwakilishi katika majimbo.

Alisema baada ya kupitishwa kwa wagombea kazi ya chama kwa sasa ni kumtambulisha mgombea katika eneo lake la kugombea.

“Tunaizingatia ratiba ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuhusu uchukuaji wa fomu za uteuzi. Kumtambulisha mgombea haina maana kuwa ni mchakato tofauti na uchukuaji wa fomu bali mgombea anapoenda kuchukua fomu anatakiwa awe na barua ya utambulisho kutoka katika chama kinachomdhamini; kwa hiyo wagombea wetu wataanza kesho (leo) kuchukua fomu katika maeneo mbalimbali,”alisema Ngulangwa.

Aliwataka wagombea wote wa ubunge na udiwani, kuzingatia muda wa kuchukua na kurejesha fomu ambao ni kuanzia leo hadi Agosti 25.

Ngulangwa alisema kuwa CUF kimesimamisha wagombea ubunge katika majimbo yote 214 ya Tanzania Bara na wawakilishi katika majimbo yote 50 ya Zanzibar.

Kwa wagombea wa udiwani, alisema kuwa mpaka sasa chama hicho kimefanikiwa kwa asilimia 80 kusimamisha wagombea udiwani na lengo lao ni kufika asilimia 100 katika kata zote 3,956
 
Back
Top Bottom