Wagombea kudai kura kuhesabiwa upya, ni kukiuka utaratibu uliotangazwa awali wa ulinzi wa kura

WATANABE

JF-Expert Member
Apr 13, 2011
1,092
466
Wakati wa hoja ya wapiga kura kukaa mita 200 kulinda kura, wananchi tuliambiwa na Tume kuwa sheria za uchaguzi zinawatambua mawakala walioteuliwa na vyama/wagombea ndio walinzi wa kura kwa niaba ya vyama. Hivyo sio ruksa kwa mtu mwingine yeyote kuchukua jukumu la mawakala wa vyama/wagombea kulinda kura.

Sasa iweje baada ya kura kupigwa na kuhesabiwa na mawakala kuweka sahihi katika nyaraka za matokeo baadhi ya wagombea wanaoshindwa wadai kuwa kura zihesabiwe upya kwa maana ya kutowaamini mawakala wa vyama/wagombe (walinzi wa kura) kiasi cha kuiweka amani ya nchi katika hatari. Ni dhahiri kuwa walinzi wa kura (Mawakala) baada ya kura kuhesabiwa na nyaraka za matokeo kuwekwa sahihi na mawakala wote kwa kukubalina na matokeo na kubandikwa vituoni kwa ajili ya wananchi kujua matokeo. Mawakala husika waliondoka vituoni na kuacha masanduku pasipo ulinzi wowote toka vyama. Hivyo sio haki kwa masanduku ambayo hayakuwa chini ya walinzi wa kura wa vyama kuhesabiwa upya.

Laiti kama wagombea na mawakala wangebaini matatizo yeyote katika zoezi la kuhesabu kura wasingekubaliana na zoezi hilo na nyaraka za matokeo zisingewekwa kuwekwa sahihi na mawakala wote kuashiria kukubalina na matokeo husika, hivyo masnduku ya kura ya ngeendelea kuwa chini ya walinzi wa kura wa vyama wanaotambuliwa na Tume hadi muafaka kupatikana.

Ushauri wangu kama mamilioni ya watanzania waliweza kukubali kuwa mawakala ndio walinzi wa kura kwa niaba ya vyama na kusitisha zoezi la kukaa mita 200 toka vituo vya kupiga kura. Naiomba Tume ya Taifa ya Uchaguzi baada ya kura kupigwa, kuhesabiwa na nyaraka za matokeo kuwekwa sahihi na mawakala wote kukubalina na matokeo isijichanganye na kukubali kuwa mawakala sio walinzi wa kura wa vyama kwa sababu hili linaweza kusababisha uvurugaji wa uchaguzi mkuu ujao kwa kuwa wananchi watajenga imani kuwa mawakala sio walinzi wa kutra kwa niba ya vyama. .

Yeyote mwenye ushahidi kuwa kura hazikuhesabiwa kama ilivyotakiwa anatakiwa kuwasilisha malalamiko yake mahakamani badala ya kuhatarisha amani ya nchi.
 
Back
Top Bottom