Wagombea kitovu cha mtoto mchanga! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wagombea kitovu cha mtoto mchanga!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by ndyoko, Nov 28, 2011.

 1. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #1
  Nov 28, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 279
  Trophy Points: 180
  Dunia bado inakua, leo nimeamini!

  Nikiwa ktk matembezi yangu, wiki jana, maeneo ya chang'ombe hapa dodoma nikakuta mkusanyiko wa watu nje ya nyumba moja ya kupanga. Kama kawaida ya watu wenye tabia kama yangu ya nyatunyatu, nikasogea walau nipate cha kujifunza. Baada ya kuwauliza nilowakuta, kulikoni wanawake wanagombana, nkaambiwa huo ni ugomvi kati ya mke na mama mkwe wake. Kisa? Wanagombea kitovu cha mtoto kilichoanguka jioni ile. Mama mkwe anakitaka ili akakifanyie utaratibu kadiri ya mila zao, ili hali mama wa kachanga hako naye alikuwa anakitaka kitovu cha mwanawe iili akakitunze kadiri ya mila zao. Hapo ndo mgogoro ulipojikita. Ulikuwa ni mtiti wa kufa mtu kwani kwa yeyote alokuwa akipita karibu angeshawishika kutaka kujua kinachoendelea.

  Niwaulize wanajf, hivi kwa karne hii ya 21, issue ya kitovu inaweza ikawa na msaada gani ktk kujiletea maendeleo? Kuna ubaya gani mtu anaoweza kuupata kutokana na 'mismanagement' ya kitovu chake cha utotoni? Ktk maisha yetu haya ya 'kiswahili swahili' nmepatwa na mashaka na natamani hata kumuuliza mamsapu wangu vilipo vitovu vya wanangu, nshaingiwa na woga mie kutokana na hili tukio!

  Hebu walimwengu nijuzeni kuhusu umuhimu wa hivi vitovu vya watoto ktk makuzi yao na maisha yao ya baadae, nimeogopa kweli.

  Nisaidieni nijue ukweli na umuhimu wa kuwa na hivyo vitovu vya watoto vinavokatika/dondoka wiki chache baada ya kuzaliwa! Upssssssssssssssssss!
   
 2. Vin Diesel

  Vin Diesel JF Gold Member

  #2
  Nov 28, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 8,403
  Likes Received: 737
  Trophy Points: 280
  Ushirikina tu hapo...hakuna la maana.
   
 3. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #3
  Nov 28, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 279
  Trophy Points: 180
  Mkuu inatisha hii kitu!
   
 4. Billie

  Billie JF-Expert Member

  #4
  Nov 28, 2011
  Joined: Aug 13, 2011
  Messages: 5,335
  Likes Received: 2,341
  Trophy Points: 280
  Vuta picha huo ugomvi ungekuwa ni wa kumgombea mtoto ili wa msomeshe TZ na manchi mengne ya kiafrika tupo juu sana kushupalia mambo ya kijinga kuliko hata mazuri na ndo hapo WAZUNGU WANAPOTUPITIA.yaani hapo hakuna lolote zaidi ya kurithishana mizimu wee fikilia kitovu cha nini sasa ndo maana wabongo tupo kama tumerogwa all the time.BIBI HAPO APOTEE ZAKE MAANA HAWAKAWII KUMCHAGUA MTU WA KUMRITHISHA MIKOBA YAKE PINDI AFAPO.
   
 5. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #5
  Nov 28, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 279
  Trophy Points: 180
  Hahahaaa! Taratibu Billie, mbavu zangu zimeteguka plz!
   
 6. Vin Diesel

  Vin Diesel JF Gold Member

  #6
  Nov 28, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 8,403
  Likes Received: 737
  Trophy Points: 280
  shule na umaskini vyaleta yote haya....
   
 7. nyumba kubwa

  nyumba kubwa JF-Expert Member

  #7
  Nov 28, 2011
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 10,279
  Likes Received: 1,720
  Trophy Points: 280
  Ndyoko mila zipo na zinafuatwa. Hapo ndio ujue tatizo la kuoa mke wa kabila lingine na aliye mbishi; hao wame differ katika mila zao. Kitovu cha mtoto mama yangu alinambia kinapaswa kutunzwa (si kutambika) na kutupwa sehemu salama kwa sababu wachawi kwao ni dili ni kama wanavyonyofoa sehemu za siri za watu. Kwa hiyo nisingependa mtu achukue kitovu cha mwanagu akatumie kwa jinsi atakavyo yeye. Najua kuna watakao sema it doesn't matter, fikiria umzike nduguyo afu wachawi wamfukue wamle; utaendelea kusema it doesn't matter kwa kuwa kafa ni mzoga tu??? Well ili ni cost nothing kufuata ushauri wa mama yangu.
   
 8. nyumba kubwa

  nyumba kubwa JF-Expert Member

  #8
  Nov 28, 2011
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 10,279
  Likes Received: 1,720
  Trophy Points: 280
  Vitovu vina mambo. Nakumbuka mama mkwe wangu alinambia nihakikishe kitovu kikianguka akimwangukii mtoto kwenye mdudu wake; kwani kwao mwanza wanaamini kuwa kikigusa mdudu, mtoto akikua atakuwa functionless; Basi nilikuwa makini kweli; nani anataka kuwa na mtoto si riziki.
   
 9. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #9
  Nov 28, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Imani za kishirikina tu. . .
  Hicho kitovu kina uhai? Wawe wanahifadhi mpaka kucha na nywele wakinyoa basi.
   
 10. M

  Muinjilisti Senior Member

  #10
  Nov 28, 2011
  Joined: Dec 20, 2010
  Messages: 105
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nielewavyo mimi kama mtu mbaya au mshirikina/mchawi atakipata kitovu chako anakuwa na access na wewe. Ni rahisi kwa mwenye kitovu chako kukupata katika anga za kichawi, na kukutumia apendavyo pamoja na kumilikishwa mikoba. Kama hana kitovu itakuwa kazi kwake kukupata kichawi hata kama atakupata. Ndiyo maana katika familia nyingine wakina mama wanaweza kugundua watoto wao ni wachawi wakati hao watoto wameshabobea. Mpaka ugundue kwanza ni kazi. Mimi yalishawahi kunikuta hayo ya kukataa kutoa kitovu cha mwanangu hadi mama Mkwe akamind kama siyo kukusirika. Nimeolewa na mchaga wakati mimi si mchaga, kumbe ukishajifungua tu, mama mkwe (sina uhakika kama ni wachaga wote wanafanya haya) lazima aje kuchukua kitovu, eti wanaenda kuvizika hiko migombani ambako vitovu vyote vya ukoo vinazikwa huko. Cha mtoto wa kwanza nilimpa, na mtoto ikawa bahati mbaya (lakini simaanishi ni kwa sababu ya hiko kitovu nilichompa). Katika kujifunza mambo ya watoto nikajua kuwa kitovu ni kitu sensitive, inabidi nikidestroy mwenyewe kwa kukichoma nk. Nikaamua nikizaa mtoto mwingine wala simpi mtu kitovu bila kujali mila za baba yake. Kilipokatika nikamwambia mume wangu na kumwambia nitakichoma mwenyewe safari hii sitampa mama na sababu nikampa. Mama Mkwe aliposikia hayo alikasirika akaona shughuli yote ya kuja kumuona mwali na mwanaye imekuwa nuksi
   
 11. nyumba kubwa

  nyumba kubwa JF-Expert Member

  #11
  Nov 28, 2011
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 10,279
  Likes Received: 1,720
  Trophy Points: 280
  Umeona eeh. Hawa wanaongea tu; wewe uambiwe mtu anaweza mchezea mwanao through kitovu kama mzazi kweli unaweza ku-ignore. mwanawane kitovu ni kitu sensitive; hata kama tunadharau mila sababu ya westernization kwangu ni big NO when it comes to my kids.

   
 12. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #12
  Nov 28, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Kwani watu wanasema ukiweke pambo sebleni?Siukitupe mwenyewe hata chooni bila sijui kwenda kuzika na kutambikia?
   
 13. nyumba kubwa

  nyumba kubwa JF-Expert Member

  #13
  Nov 28, 2011
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 10,279
  Likes Received: 1,720
  Trophy Points: 280
  Lizy kutambiaka hata mimi sikubali, kwani kunapingana na imani za dini. Ila nachosisitiza ni kuki destroy mwenyewe ili watu wabaya wasikitumie watakavyo. Kwa hiyo huyo mke aliyekataa kumpa mama mkwe wake naona amefanya sawa tu; kwani hajui huyo mama anakitaka cha NINI?

   
 14. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #14
  Nov 28, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Hapo tuko pamoja NK. . .

  Heehehe ukute anataka kumuandaa mtoto kurithi matunguli (kwa wale wanaomini).
   
 15. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #15
  Nov 28, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,323
  Likes Received: 22,157
  Trophy Points: 280
  Ndoa nyingine ngumu sana, mtu na mama mkwe wake wanaishi kama wake wenza.
   
 16. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #16
  Nov 28, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,323
  Likes Received: 22,157
  Trophy Points: 280
  Du..... Mambo ya vitovu kumbe big issue? Ngoja na mimi nianze kutafutwa kitovu changu kilipo, maana naona kuna mtu humu JF anatembelea nyota yangu
   
 17. Foundation

  Foundation JF-Expert Member

  #17
  Nov 28, 2011
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 1,458
  Likes Received: 256
  Trophy Points: 180
  Huyo mama mkwe atakuwa ana matatizo sio bure, yeye kitovu anakitaka cha nini. Nimekumbuka tukio moja lilishawahi kutokea miaka ya nyuma, mama wa mwanamke amesafiri kutoka kwao kuja kumuuguza mwanae, baada ya kumuuguza kwa muda fulani wakati anaondoka akataka kuondoka na kitovu kwa kulazimisha. Baba wa mtoto akakataa, mama mkwe wake analazimisha.Mama mtu alienda kuporwa kitovu na baba wa mtoto kituo cha basi.

  Kitovu kina uhusiano na mambo ya ushirikina.
   
 18. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #18
  Nov 28, 2011
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,873
  Likes Received: 6,226
  Trophy Points: 280
  washirikina tu hao
   
 19. Billie

  Billie JF-Expert Member

  #19
  Nov 28, 2011
  Joined: Aug 13, 2011
  Messages: 5,335
  Likes Received: 2,341
  Trophy Points: 280
  Hii ndo Tanzania..
   
 20. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #20
  Nov 28, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Ndiyo maana tuko kwenye hali tuliyonayo.
   
Loading...