Wageni Ka Babu Loliondo Bei Juu.

Barubaru

JF-Expert Member
Apr 6, 2009
7,161
2,323
Hakika nimesoma katika magazeti ya huko Tanzania yanabainisha kuwa BEI ya Kikombe cha Babu (Mchungaji Mwasapila) wa huko Samunge Loliondo kimepandishwa bei kwa wageni lakini wazawa bai ile ile TSh 500.

Kuanzia sasa Kila Mgeni ambaye sio raia wa Tanzania inampasa kulipa shilingi TSh 1500 au (Dola za Amerika moja).

Sasa suala langu hapa. Tunajuwa fika kuwa mchungaji huyu alishukiwa na maono ya kuonyeshwa dawa na kuamrishwa na aliyemuotesha atoze kwa kila mgonjwa TSh 500 bila kujali rangi, kabila au utaifa wake.

Sasa huku kuwatoza wageni zaidi ameoteshwa pia?
 
Hakika intatanisha!
 
wageni wamekulalamikia? Kama wanaona dola moja ni shida si wana uchaguzi wa kutokuja? Watu wengine bwana.....naona babu anawanyima usingizi, basi tumieni huo muda kufanya utafiti wa kisayansi kugundua alternative and scientific med to treat ailments babu treats
 
Mtoa hoja, nakuliza, Je shilingi mia tano ni dola ngapi? Kama mtu hana tsh cash ndio maana babu akasema iwe 1 dola, wapo wakenya wanatoa mia tano kwani huweza kuzibadili mpakani.Nafikiri hii ni kurahisisha ulipaji wa huduma sio ubaguzi.
 
Dr Barubaru,

Mcheza kwao, hutuzwa. Acheni na sisi tufaidi tukiwa kwetu na wageni nao wasote kidogo.

Ukiwa nchi za watu hadi unajuta kuwa Mtanzania. Kama hilo linauma basi kama wao wanavyosema tukiwa kwao.... "DON'T COME."
 
Back
Top Bottom