kamili
JF-Expert Member
- Feb 10, 2011
- 1,219
- 855
Miaka michache iliyopita rais Museveni wa Uganda aliwahi kwenda china na kuwaomba wachina angalao wawe wanakunywa kikomba kimoja cha kahawa kila siku.
Museveni alisema kwa kufanya hivyo kahawa yote ya Uganda ingepata soko. (kwa kawaida wachina huwa wana chai yao wenyewe)
Kwa kipindi cha miaka miwili nimekuwa nikifika Kampala. Ni vigumu kupata chai au kahawa kwenye migahawa ya kawaida. Uchunguzi wangu unaonesha katika migahawa 10, saba siku zote watakuambia hawana chai.
Tena ukiagiza chai asubuhi mhudumu atakushangaa halafu atasema no tea, au , tena mara nyingi ataondoka na kukuacha. Migahawa miwili watasema not ready but we can prepare for you.
Halafu atachemsha mara nyingi ya kwako tu. Na hata ukirudi siku ya pili yake na kuendelea utapata majibu hayo hayo na watakuandalia, hakuna siku utakuta chai ipo.
Halafu mgahawa moja kati ya kumi ndio unaweza pata chai saa zote.
Vile vigenge vya kahawa na chai kwa mama ntilie ambavyo vimesambaa Tanzania nzima ukiwa Uganda sahau, unaweza pata chai au kahawa kwenye mahoteli makubwa saa zote lakini si katika mazingira ya kawaida.
Jumapili iliyopita saa tatu nilikuwa Makindye road na nikamwambia rafiki yangu Mganda nahitaji chai, haikuwa kazi rahisi tuliuliza kwenye migahawa mpaka akaanza kukasirika. Cha ajabu nimekuwa nikiwauliza Waganda kama wanakunywa chai asubuhi wote husema wanakunywa.
Kwa upande mwingine kama unapata kinywaji kidogo (alcohol), hapa utajirusha mpaka uone.
Ushauri wangu ni kuwa ipo haja ya kuwashauri Waganda wawe wanakunywa chai na kahawa ina manufaa ya kiuchumi, kuliko kuwashawishi wachina wakati wenyewe hawaitumii sana.