Wafungwa wataja vigogo dawa za kulevya

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,000
9,862
WAFUNGWA 130 katika Magereza ya Hong Kong nchini China, wametaja majina ya watu maarufu wakubwa, wanaojihusisha na biashara ya dawa za kulevya nchini.

Majina hayo ya wafanyabiashara wakubwa, baadhi yao wanamiliki maduka makubwa yakiwemo ya vifaa vya ujenzi, ‘supermarket’, maduka ya nguo na maeneo ya kuuza magari maarufu yadi.

Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kudhibiti Dawa za Kulevya, James Kaji amesema katika majina waliyopokea, wengi wao ni wafanyabiashara wakubwa na kwamba wameanza kuyafanyia kazi.

Mwishoni mwa wiki iliyopita, Kamishna huyo alikutana na Padri raia wa Marekani, Fr John Wotherspoon maarufu ‘Father John’ ambaye alimkabidhi orodha ya wafungwa wa Tanzania wanaotumikia kifungo Hong Kong, baada ya kukamatwa na dawa za kulevya walizoingiza huko.

Katika orodha hiyo, Kamishna Kaji alisema “tumepokea na taratibu za kiuchunguzi zinaendelea, njia wanazotumia kuwatumia hao watu, lengo letu ni kung’oa mizizi ya tatizo.

“Kuna majina nikikuonyesha hutaamini, ni ‘mabig fish’, wapo mstari wa mbele kulipa kodi na kusaidia jamii, lakini nyuma ya pazia wanaendesha biashara haramu kwa kuwatumia watu.”

Alisema baadhi ya raia kutoka nje wanaokuja nchini, hawaji kwa nia njema, kwani wmekuwa wakitoa mafunzo na kuwaandaa vijana wadogo, kujiingiza katika mtandao huo wa dawa za kulevya, ikiwemo biashara ya madangulo kwa wasichana.

Alisema kitengo chake kipo mstari wa mbele katika mapambano dhidi ya dawa za kulevya kama vile kokeini, heroin na aina nyingine ya dawa za kulevya. Alieleza kuwa hiyo ni vita ngumu, hatari na inahitaji kubadili mbinu kila wakati.

“Wauzaji, wabebaji Tanzania na kwingineko duniani, wamekuwa wepesi katika kubadili mbinu ili kukwepa jicho na mkono wa dola, ni wajanja sana sana na mbaya zaidi ni watu wenye mikono mirefu,” alisema.

Hata hivyo, Kaji alisema baada ya kudhibiti uchochoro wa kiwanja cha ndege, wamebaini kuwa njia ya bandari imekuwa uchochoro kwa dawa hizo kupitia kwenye magurudumu na milango ya gari, kuwekwa kwenye saruji nyeupe na pipi.

Alisema kwa nchini wamedhibiti utumiaji na uingizaji wa dawa hizo kwa asilimia 98. Kwamba kwa sasa wauzaji hao wa dawa za kulevya, wanatumia nchi za Afrika Kusini na Msumbiji, kama uchochoro wa kupitishia dawa hizo.

“Kuna Watanzania watatu ambao wamekamatwa mwezi huu wa Januari huko Hong Kong. Watanzania hao walitokea Ethiopia, hawakupita kwenye ‘airport’ zetu,” alisema.

Kauli ya Kaji imekuja kufuatia mwishoni mwa wiki, ‘Father John’ ambaye anahudumu kwenye magereza, alikutana na familia za wafungwa wa dawa za kulevya waliopo Hong Kong na China.

Alisema zaidi ya Watanzania 1,000 wapo kwenye magereza mbali mbali duniani huku 68 wakisubiri kunyongwa.

Kwa mujibu wa Kaji, Gereza la Hong Kong peke yake lina wafungwa 130 na wengi wao ni vijana wadogo, waliotumika kubeba dawa hizo.
Magereza mengine yenye idadi kubwa ya Watanzania ni ya India na Afrika Kusini.

Chanzo: Habari Leo
 
Na serikali ijitafakari huenda mifumo si rafiki ya vijana kujipatia kipato halali ndio maana tunajazana magerezani!
Elimu inayopika taifa iangaliwe vizuri binafsi naona kuna watu hakunaga hata haja ya kuwasomesha vitu vingi bora iangaliwe fani anayoiweza ajitose huko!!
Mazingira ktk nchi yetu yanatakiwa yawe rafiki lkn pia na bongo zetu zinatakiwa kuwa safi alasivyo tutatumika sana,sifa mbaya Sana kwa nchi.
 
Vyombo vyetu vya habari navyo vijikite ktk kuibua mambo kama haya sio kila siku udaku wa kina Amber nani mara diva! Mnatuaibisha hii ni fedheha kwa nchi.. toeni taarifa za hivi ili vijana pia tujue ilete uoga ama tujue uhuni huu unaweza gharimu maisha na kifungo..
 
Hii taarifa sijajua kamishna kama anakusudia kuwatisha wahusika au ndo yuko serious na majina anayo kwa ajili ya uchunguzi....!

Lakini je, angeendelea na uchunguzi bila kukutana na vyombo vya habari angepungukiwa nini..? Kwa sababu ni anawa alert wahusika ili wakae mbali na aina yoyote ya ushahidi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hata ulaya na marekani na Asia mamilioni hawana kazi ila wao wamechagua kuza na kusambaza madawa kama kazi

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
WAFUNGWA 130 katika Magereza ya Hong Kong nchini China, wametaja majina ya watu maarufu wakubwa, wanaojihusisha na biashara ya dawa za kulevya nchini.

Majina hayo ya wafanyabiashara wakubwa, baadhi yao wanamiliki maduka makubwa yakiwemo ya vifaa vya ujenzi, ‘supermarket’, maduka ya nguo na maeneo ya kuuza magari maarufu yadi.

Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kudhibiti Dawa za Kulevya, James Kaji amesema katika majina waliyopokea, wengi wao ni wafanyabiashara wakubwa na kwamba wameanza kuyafanyia kazi.

Mwishoni mwa wiki iliyopita, Kamishna huyo alikutana na Padri raia wa Marekani, John Wotherspoon maarufu ‘Father John’ ambaye alimkabidhi orodha ya wafungwa wa Tanzania wanaotumikia kifungo Hong Kong, baada ya kukamatwa na dawa za kulevya walizoingiza huko.
Katika orodha hiyo, Kamishna Kaji alisema “tumepokea na taratibu za kiuchunguzi zinaendelea, njia wanazotumia kuwatumia hao watu, lengo letu ni kung’oa mizizi ya tatizo.

“Kuna majina nikikuonyesha hutaamini, ni ‘mabig fish’, wapo mstari wa mbele kulipa kodi na kusaidia jamii, lakini nyuma ya pazia wanaendesha biashara haramu kwa kuwatumia watu.”

Alisema baadhi ya raia kutoka nje wanaokuja nchini, hawaji kwa nia njema, kwani wmekuwa wakitoa mafunzo na kuwaandaa vijana wadogo, kujiingiza katika mtandao huo wa dawa za kulevya, ikiwemo biashara ya madangulo kwa wasichana.

Alisema kitengo chake kipo mstari wa mbele katika mapambano dhidi ya dawa za kulevya kama vile kokeini, heroin na aina nyingine ya dawa za kulevya. Alieleza kuwa hiyo ni vita ngumu, hatari na inahitaji kubadili mbinu kila wakati.

“Wauzaji, wabebaji Tanzania na kwingineko duniani, wamekuwa wepesi katika kubadili mbinu ili kukwepa jicho na mkono wa dola, ni wajanja sana sana na mbaya zaidi ni watu wenye mikono mirefu,” alisema.

Hata hivyo, Kaji alisema baada ya kudhibiti uchochoro wa kiwanja cha ndege, wamebaini kuwa njia ya bandari imekuwa uchochoro kwa dawa hizo kupitia kwenye magurudumu na milango ya gari, kuwekwa kwenye saruji nyeupe na pipi.

Alisema kwa nchini wamedhibiti utumiaji na uingizaji wa dawa hizo kwa asilimia 98. Kwamba kwa sasa wauzaji hao wa dawa za kulevya, wanatumia nchi za Afrika Kusini na Msumbiji, kama uchochoro wa kupitishia dawa hizo.

“Kuna Watanzania watatu ambao wamekamatwa mwezi huu wa Januari Hong Kong. Watanzania hao walitokea Ethiopia, hawakupita kwenye ‘airport’ zetu,” alisema.

Kauli ya Kaji imekuja kufuatia mwishoni mwa wiki, ‘Father John’ ambaye anahudumu kwenye magereza, alikutana na familia za wafungwa wa dawa za kulevya waliopo Hong Kong na China.

Alisema zaidi ya Watanzania 1,000 wapo kwenye magereza mbali mbali duniani huku 68 wakisubiri kunyongwa.
Kwa mujibu wa Kaji, Gereza la Hong Kong peke yake lina wafungwa 130 na wengi wao ni vijana wadogo, waliotumika kubeba dawa hizo.
Magereza mengine yenye idadi kubwa ya Watanzania ni ya India na Afrika Kusini.

Chanzo: Habari Leo

Mimi nasubiri tu hayo majina, maana umekuwa kama wimbo kwa viongozi mbalimbali wa serikali kudai kuwa wanamajina ya wahalifu/watu wanaotuhumiwa kwa makosa mbalimbali, lakini hata siku moja sijasikia wakiwataja hadharani.
 
Hii taarifa sijajua kamishna kama anakusudia kuwatisha wahusika au ndo yuko serious na majina anayo kwa ajili ya uchunguzi....!

Lakini je, angeendelea na uchunguzi bila kukutana na vyombo vya habari angepungukiwa nini..? Kwa sababu ni anawa alert wahusika ili wakae mbali na aina yoyote ya ushahidi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Nakumbuka msanii fulani miaka kadhaa iliyopita nae alidai kuwa na majina! masikini ikagharimu maisha yake. Sasa hapa tena eti majina yapo na yale ya yule kaka wa dar yamefikia wapi?? usanii katika ubora wake
 
Supplier mkubwa hkko China alikuwa kiboko
Na kiboko yuko jela huku bongo
Hiyo list ingepatikana ingekuwa vizuri
Any way naona mzee John kajilipua kupambana na wauzaji....

Ova

Sent using Jamii Forums mobile app
 
baba K alijinasibu kuwa na The list ila najua ni mpenda misifa sio mbaya mkizuia kuingizwa nchini ila mjue vijana sasa hivi ni Do or Die when they try to be rich. Ajira ni changamoto Graduate ni wengi Ajira chache. vipi unataka kusema wajiajiri ? wapiii hiyo sio rahisi kujiajiri wakati hana dhamana zaidi ya vyeti vyake .
Vijana wa Tz nawakubali sana mjilipue kadri inavyowezekana majuu mbona wanaigeria na waghana wameenda mbali kila nchi huikosi race yao.
rahisisheni mambo ya passport vijana waendelee kujilipua
 
WAFUNGWA 130 katika Magereza ya Hong Kong nchini China, wametaja majina ya watu maarufu wakubwa, wanaojihusisha na biashara ya dawa za kulevya nchini.

Majina hayo ya wafanyabiashara wakubwa, baadhi yao wanamiliki maduka makubwa yakiwemo ya vifaa vya ujenzi, ‘supermarket’, maduka ya nguo na maeneo ya kuuza magari maarufu yadi.

Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kudhibiti Dawa za Kulevya, James Kaji amesema katika majina waliyopokea, wengi wao ni wafanyabiashara wakubwa na kwamba wameanza kuyafanyia kazi.

Mwishoni mwa wiki iliyopita, Kamishna huyo alikutana na Padri raia wa Marekani, John Wotherspoon maarufu ‘Father John’ ambaye alimkabidhi orodha ya wafungwa wa Tanzania wanaotumikia kifungo Hong Kong, baada ya kukamatwa na dawa za kulevya walizoingiza huko.
Katika orodha hiyo, Kamishna Kaji alisema “tumepokea na taratibu za kiuchunguzi zinaendelea, njia wanazotumia kuwatumia hao watu, lengo letu ni kung’oa mizizi ya tatizo.

“Kuna majina nikikuonyesha hutaamini, ni ‘mabig fish’, wapo mstari wa mbele kulipa kodi na kusaidia jamii, lakini nyuma ya pazia wanaendesha biashara haramu kwa kuwatumia watu.”

Alisema baadhi ya raia kutoka nje wanaokuja nchini, hawaji kwa nia njema, kwani wmekuwa wakitoa mafunzo na kuwaandaa vijana wadogo, kujiingiza katika mtandao huo wa dawa za kulevya, ikiwemo biashara ya madangulo kwa wasichana.

Alisema kitengo chake kipo mstari wa mbele katika mapambano dhidi ya dawa za kulevya kama vile kokeini, heroin na aina nyingine ya dawa za kulevya. Alieleza kuwa hiyo ni vita ngumu, hatari na inahitaji kubadili mbinu kila wakati.

“Wauzaji, wabebaji Tanzania na kwingineko duniani, wamekuwa wepesi katika kubadili mbinu ili kukwepa jicho na mkono wa dola, ni wajanja sana sana na mbaya zaidi ni watu wenye mikono mirefu,” alisema.

Hata hivyo, Kaji alisema baada ya kudhibiti uchochoro wa kiwanja cha ndege, wamebaini kuwa njia ya bandari imekuwa uchochoro kwa dawa hizo kupitia kwenye magurudumu na milango ya gari, kuwekwa kwenye saruji nyeupe na pipi.

Alisema kwa nchini wamedhibiti utumiaji na uingizaji wa dawa hizo kwa asilimia 98. Kwamba kwa sasa wauzaji hao wa dawa za kulevya, wanatumia nchi za Afrika Kusini na Msumbiji, kama uchochoro wa kupitishia dawa hizo.

“Kuna Watanzania watatu ambao wamekamatwa mwezi huu wa Januari Hong Kong. Watanzania hao walitokea Ethiopia, hawakupita kwenye ‘airport’ zetu,” alisema.

Kauli ya Kaji imekuja kufuatia mwishoni mwa wiki, ‘Father John’ ambaye anahudumu kwenye magereza, alikutana na familia za wafungwa wa dawa za kulevya waliopo Hong Kong na China.

Alisema zaidi ya Watanzania 1,000 wapo kwenye magereza mbali mbali duniani huku 68 wakisubiri kunyongwa.
Kwa mujibu wa Kaji, Gereza la Hong Kong peke yake lina wafungwa 130 na wengi wao ni vijana wadogo, waliotumika kubeba dawa hizo.
Magereza mengine yenye idadi kubwa ya Watanzania ni ya India na Afrika Kusini.

Chanzo: Habari Leo
Hata wakita haitasadia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Issue za madawa ya kulevya unaweza ukakuta huyo anaye wataja wenzake naye yupo kwenye list.
 
Back
Top Bottom