Wafungwa wagoma kula, mmoja afa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wafungwa wagoma kula, mmoja afa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Yetuwote, Jun 19, 2011.

 1. Y

  Yetuwote Senior Member

  #1
  Jun 19, 2011
  Joined: Jul 22, 2010
  Messages: 194
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Na Restuta James 19th June 2011 Wafungwa zaidi ya 20 walio katika gereza la Maweni, mkoani Tanga, ambao wamehukumiwa kunyongwa wamegoma kula na mmoja anadaiwa kufariki dunia. Taarifa zilizolifikia gazeti hili zinaeleza kwamba wafungwa hao wamegoma kwa siku ya tano sasa kwa madai ya kupewa chakula kibovu. Hata hivyo, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Shamsi Vuai Nahodha, amesema hana taarifa za wafungwa hao kugoma. “Ndio nasikia kwako mie silijui hilo,” alisema Nahodha. Hata hivyo, aliahidi kuzifuatilia. Wakati Nahodha akieleza hayo, Waziri Kivuli wa Wizara hiyo, Godbless Lema, alithibitisha kuwepo kwa mgomo huo akieleza kwamba hadi jana, ni siku ya tano tangu wafungwa hao wagome kula. Alisema baada ya kupata taarifa za kuwepo kwa mgomo huo, aliwasiliana na mkuu wa gereza hilo, ambaye naye alithibitisha wafungwa hao kugoma. “Lakini amekanusha kuhusu huyo aliyekufa, amesema hakuna mfungwa ambaye amekufa,” alisema Lema. Lema ambaye pia ni Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), alisema “Kambi yetu inafanya a very close follow-up (inafuatilia kwa karibu), suala hilo, lakini nasema haiwezekani wafungwa wakagoma tu kula lazima kuna tatizo lingine.” Aliongeza kuwa haiwezekani wafungwa hao wakagoma tu kula kwa kuwa wanakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo rufaa zao kuchelewa kusikilizwa. “Nimetembelea magareza Arusha nikaingia jela ya wanawake na wanaume, niliyoyaona huko ni hatari kubwa sana, wafungwa waliokata rufaa inachukua muda mrefu kusikilizwa na wakishinikiza sana wanahamishwa gereza…asilimia 50 ya mahabusu wanakaa hadi miaka minane kesi zao hazijasikilizwa kwa kisingizio cha upelelezi kutokamilika, kwa hiyo nina amini kwamba hata hao waliogoma wana madai zaidi ya chakula,” alisema. Lema alifafanua kuwa “Taarifa nilizonazo ni kwamba wafungwa sita wapo katika hali mbaya…nafuatilia suala hili na ikiwezekana nitaenda Tanga ili kupata ukweli wake kabla ya kulitolea taarifa rasmi,” alisema. Lema alisema wafungwa hao ni waliohamishwa kutoka gereza la Ukonga. CHANZO: NIPASHE JUMAPILI
   
 2. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #2
  Jun 19, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Kilichonichanganya eti Shamsi Vuai Nahodha hajui hili lakini Lema ana details za kutosha kuhusu mgomo na uthibitisho keshawasiliana na mkuu wa gereza Maweni kuthibitisha tukio hilo! Hii ni aibu kwa waziri vinginevyo labda kama alilenga kuficha ukweli kwa sababu anazozijua yeye.
  Hili lisipopatiwa tiba mapema litasambaa sasa hivi magereza mengine, ni bora viongozi wetu wakashughuliikia madai ya wafungwa hao kikamilifu kuliko kuendelea kutafuta mchawi wa matukio ambayo huenda sababu zake ziko wazi.
   
 3. Ziada Mwana

  Ziada Mwana JF-Expert Member

  #3
  Jun 19, 2011
  Joined: May 20, 2011
  Messages: 201
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kama kawa, endeleeni kufuatilia kila kitu kilichopo mbele yenu,mtapata tu umaarufu.
   
 4. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #4
  Jun 19, 2011
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,250
  Likes Received: 3,853
  Trophy Points: 280
  Waziri mkuu unajua kuwa kuna waziri anakaa hotelini pale New africa? "Sijui nitafuatili" Waziri Nahodha unajua kuwa kunawafungwa wamegoma kula na leo nisiku ya tano? "Sijui nitafuatilia"

  Nilishasema cdm ndiyo inayongoza nchi japo haina makazi magogoni!!!
  Rais anaendelea na biashara zake huko ughaibuni!!!
   
 5. MAYOO

  MAYOO JF-Expert Member

  #5
  Jun 19, 2011
  Joined: Feb 14, 2011
  Messages: 200
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Hivi huyu vuai anafanya kazi gani huku bara? Au ndo kaja kutalii ktk hotel za kifahari tu? Shame on you vuai, go back to your homeland, unatufilisi tu hata kazi hujui.
   
 6. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #6
  Jun 19, 2011
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,320
  Likes Received: 5,610
  Trophy Points: 280
  Sasa napata picha kuwa EL hakuwa size ya JK alishamfunika mbaya ....ndio maana akaamua kumtafuta mtu kilaza ili amfunike sasa ndio akapatikana mtoto wa mkulima ......na mawaziri kanma yeye...ambao wote waanafunikwa na kilaza mwenzao!!!!PM hajui...waziri hana taarifa Spika anawatetea!!!kuna watu hapo??
   
 7. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #7
  Jun 19, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,516
  Likes Received: 19,940
  Trophy Points: 280
  nani mwenye ile katuni waziri akiwa hotelini?
   
 8. Hassan J. Mosoka

  Hassan J. Mosoka JF-Expert Member

  #8
  Jun 19, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 647
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
   
 9. z

  zamlock JF-Expert Member

  #9
  Jun 19, 2011
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 3,849
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  yani jamanwafungwa wanashida sana huyu vuai sijui walimtoa wp kwanza anaishi hotel kwa kodi zetu na bado atekelezi yale ambayo ni muhimu kwetu kama wananchi
   
Loading...