Herbalist Dr MziziMkavu
Platinum Member
- Feb 3, 2009
- 43,101
- 34,919
Wafungwa hao wakipelekwa hospitalini
Waziri wa ulinzi wa Uruguay amesema wafungwa sita kutoka gereza la Guantanamo wameachiliwa huru na kupewa hadhi ya utaifa ya kuishi Amerika- Kusini.
Waziri Eleuterio Huidobro, aliliambia shirika la Reuters kwamba Uruguay haijapokea katazo ama kupokea vipingamizi vyovyote kutoka Marekani ilipokubali kuwapokea wafungwa hao wa zamani.
Wanaume hao sita walio huru hivi sasa wanne kati yao ni raia wa Syria,mmoja kutoka Palestina na mwingine ni kutoka nchini Tunisia waliwasili mjini Montevideo mwishoni mwa wiki iliyopita majira ya asubuhi na kupelekwa katika hosipitali ya kijeshi kwa uchunguzi wa kiafya.
Uhuru wao unakuja baada ya kutumikia kifungo cha miaka kumi na miwili gerezani wakituhumiwa kwa kujihusisha na kikundi cha Al-Qaeda na hawakuwahi kuhukumiwa katika kipindi chote walichokuwamo gerezani.
Chanzo:BBC