Wafugaji wamwagiwa mabilioni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wafugaji wamwagiwa mabilioni

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Feb 20, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Feb 20, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,607
  Likes Received: 4,600
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Rais Jakaya Kikwete akimkabidhi Mkazi wa Wilaya ya Longido ng'ombe watano na mbuzi ambaye ni miongoni mwa kaya 6,128 za wilaya hiyo, Monduli na Ngorongoro mkoani Arusha ambazo mifugo yao yote ilikufa kwa kukosa maji na malisho kutokana na ukame.(PICHA:IKULU)


  Serikali imetenga Sh. bilioni 11.2 kwa ajili ya mradi wa uwezeshaji wafugaji waliopoteza mifugo yao kutokana na ukame katika kaya 6,128 za wilaya za Longido, Monduli na Ngorongoro mkoani Arusha.
  Mradi huyo ulizinduliwa jana na Rais Jakaya Kikwete wilayani hapa kuzipa kata hizo mitamba minne na mbuzi mmoja.
  Kikwete alikabidhi mitamba, madume na mbuzi kwa kaya 16 zilizopokea kwa niaba ya kaya hizo 6,128 ambazo mifugo yao ilikufa kutokana na ukame huo kuanzia mwaka 2008/09 hadi 2009/2010.
  Akizungumza katika uzinduzi huo, Kikwete aliwataka madiwani katika halmashauri husika kuwa wakali dhidi ya watumishi wasio waaminifu watakaotaka kujinufaisha kupitia zabuni zitakazotolewa kwa ajili ya kununua mifugo hiyo.
  “Halmashauri za wilaya zishirikiane wapi kwa kupata mifugo ya kununua na itoe haraka taarifa serikalini ili fedha zitolewe mapema…halmashauri zisimamie zabuni na kuhakikisha kwamba wanalete ng’ombe wazuri (mitamba) na sio wale ambao wameacha kuzaa," alisema na kuongeza kuwa
  “Kamilisheni zabuni za kuwapata ng’ombe, halmashauri itakayokamilisha mapema ndiyo itakayopata fedha mapema za kununulia mifugo.”
  Rais Kikwete aliwataka madiwani kuwa wakali na kuhakikisha kwamba zabuni zinafanyika kwa haraka na kwa kufuata taratibu za kisheria.
  Kuhusu uboreshaji wa mifugo, alisema serikali yake itashirikiana na wafugaji kuhakikisha inapata malisho na maji ya kutosha.
  “Kufuga bila malisho ya uhakika hakuleti tija…inatakiwa kila mmoja apate malisho na maji pale pale alipo, hali ambayo itasaidia kuboresha mifugo yetu,” alisema na kusisitiza kuwa: “kama Botswana wameweza na sisi tunaweza.”
  Aliagiza kufanyika kwa utaratibu wa baadhi ya wafugaji kwenda kujifunza ufugaji wa ng’ombe nchini humo kwa gharama za serikali.
  “Nataka Wizara ya Mifugo na Uvuvi, iwainue wafugaji kutoka hali duni na kufikia ufugaji kama wa Botswana,” alisema.
  Vilevile aliwataka kutunza mazingira kwa kupanda nyasi kwa ajili ya malisho kwa kila mfugaji na serikali itahakikisha jambo hilo linatekelezwa.
  Kuhusu tatizo sugu la upatikanaji wa maji, Rais Kikwete, alisema litatatuliwa kwa wilayani hiyo na za Karatu na Monduli.
  Alisema awali kulikuwa na mapendekezo ya kupata maji kutoka chanzo cha Mlima Meru, ingawa baadaye utafiti ulifanywa kwa kushirikiana na Benki ya Dunia (WB) uliowezesha kubaini maeneo 12 yenye vyanzo vya maji wilayani humo.
  Hata hivyo, alisema katika maeneo hayo kulichimbwa visima virefu vitano tu ndivyo vyenye kutoa maji.
  “Nataka tatizo la maji limalizike suala hilo nitaondoka nalo, sio hapa tu bali hata wilaya za Karatu na baadhi ya maeneo wilayani Monduli,” alisema.  CHANZO: NIPASHE
   
Loading...