Wafuatao, wanaweza kuvivaa viatu vya Magufuli na vikawaenea

Uraisi siyo sweet dreams,na kwa mfumo upi wa kuwachagua?
Ukiondoa Mwalimu Nyerere tumekuwa tunapata surprise ya viongozi wakuu,labda Kikwete alipousaka uraisi mara ya pili.
Kwa vyama vya upinzani navyo vinapitia changamoto ya uchanga,mtaji mdogo,na CCM kutokubali upinzani kushiriki siasa za nchi yetu kikamilifu.
Kwa leo hiyo list ulioiweka hapa yawezekana ikawa list tofauti 2025,kwani Mama yetu ndio leading candidate.
List ya 2030 ni mapema mno kubashiri maoni ya wananchi.
 
Hakuna hata mmoja hapo kwenye orodha yako
 
Tuna uchaguzi 2025.
 
Lissu yupo hapo kwenye list Kwa sifa tajwa hapo juu,

Nimekuuliza Lissu Hana UZALENDO?

Hana Uthubutu?

Hana Maono?

Hana misimamo isoyumba?

Yote hujajibu.
Weka vigezo unavyotaka kisha mpime Lissu kivyake. Wenye akili tutachambua hivyo vigezo na tutamchambua Lissu kiuwiano.

Lakini kama kigezo ni Magufuli sahau habari ya Lissu. Ongeza hao niliokutajia - ambao, btw, wana hizo sifa zote ulizotaja na Magufuli alikuwa ndio kila kitu kwao.
 
Sijaona wa kumzia Mama
Uchumi
Elimu
Afya

She is OK and she is doing fine.
1. Uchumi zero
2. Elimu ya ovyo na wanafunzi elimu ya juu wananyimwa mikopo kisa 'o level' walisoma shule binafsi wakati kuna watoto wa viongozi waliosoma shule binafsi lakini wamepata mikopo mpaka asilimia 100!!!!
3. Mpango mbovu na usiofanya kazi kuhusu afya za wananchi wa kada za chini kimapato
4. Hakuna barabara hata moja aliyofaulu kuijenga na yenye ubora zaidi ya kuziba mashimo kila baada ya miezi miwili na kuipendelea Dar Es Salaam
5. Ajira ya upendeleo
6. Kunyanyasa wananchi watoa taarifa kuhusu maovu yanayofanywa na watendaji
7. Kusifia vitu visivyokuwepo
8. Kutochukua hatua dhidi ya watendaji wanaotajwa kwenye ripoti ya CAG tangu mwenye mamlaka kuchukua kiti hivyo ubadhirifu kutamalaki isivyo kawaida maana wafujaji hawana hofu yoyote kwa kuwa wanakingwa na 4Rs (mchukua maamuzi anaona aibu kuwashughulikia)
 
Kwa Tundu Lissu hapo umegusa mlemle mkuu. Tawareeee!
 
Kwa Tundu Lissu hapo umegusa mlemle mkuu. Tawareeee!
Atavuka kihunzi Cha CDM?

Maana tangu kuanzishwa CDM, hawajawahi rudia mgombea Urais!!🤔

Anyway, vyama vipo vingi,

Tusubiri!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…