Wafuasi wa JPM kujiunga NCCR Mageuzi

Wafuasi wa JPM kujiunga NCCR Mageuzi

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
143,392
Reaction score
289,518
Hii ndio Taarifa iliyoripotiwa na Gazeti la Raia Mwema , Inadaiwa kwamba kitendo cha Ofisi ya Msajili kukalia Usajili wa Umoja Party , ambacho inasemekana kiliundwa na wafuasi wa JPM , Plan B ni wote kuhamia NCCR .

Ngoja tujionee hizi sarakasi mpya .

JPM.jpg
 
Mkuu ni kweli kwamba hawa mamluki wa Sukuma gang wanakuja kwenu ?
Sina hii taarifa nimeona kwenye magazeti nafikiri pia kwenye mamlaka za chama hakuna taarifa kama hizi. Nimesikia pia anayesemekana ni Mwenyekiti wa Umoja Party akikana taarifa hii kupitia ujumbe wa Sauti.

Zaidi ya hapo mamlaka za NCCR-Mageuzi zinazohusika kama vile Idara ya Uenezi na Mahusiano ya Umma inayoongozwa na Comrade Simbeye au Ofisi ya Katibu mkuu wa chama au Ofisi ya Mwenyekiti mpaka zitakapo kuwa na maelezo zaidi. Ila hata mimi nimeona na kusoma kupitia Magazeti.
 
Hii ndio Taarifa iliyoripotiwa na Gazeti la Raia Mwema , Inadaiwa kwamba kitendo cha Ofisi ya Msajili kukalia Usajili wa Umoja Party , ambacho inasemekana kiliundwa na wafuasi wa JPM , Plan B ni wote kuhamia NCCR .

Ngoja tujionee hizi sarakasi mpya .
Mkuu, 'Erythro.' watakwenda NCCR ipi/ya nani; si hata huko tayari CCM ya Samia na Kinana washawahi kupavuruga?

Wao wangekomaa tu na Umoja Party kwa kukabiliana na msajiri huko huko.
 
Sasa tunaanza kuelewa sarakasi inayoendelea NCCR, na kama kawaida Kama ilivyo kuwa kwa CUF msajili atachezesha mechi hii.
Na huku kwingine Samia akiwatia usingizi CHADEMA. Wakizinduka, wanajikuta 2025 Samia sha funga bao la mkono!

Mikakati inaanza kujionyesha inavyosukwa.
 
Hii ndio Taarifa iliyoripotiwa na Gazeti la Raia Mwema , Inadaiwa kwamba kitendo cha Ofisi ya Msajili kukalia Usajili wa Umoja Party , ambacho inasemekana kiliundwa na wafuasi wa JPM , Plan B ni wote kuhamia NCCR .

Ngoja tujionee hizi sarakasi mpya .
Hii nchi ngumu sana! Ila mbele ya kina kinana januar,nape na wengine hiyo itengano cup yao wataishia kuisoma kwa gazeti
 
Kundi la sukuma gang linahangaika bila mafanikio.

Sasa wameamua kutafuta chama nje ya CCM ili wamuangushe mama yetu kwenye uchaguzi ujao.

Niwaaambie tu kuwa kamwe hawataweza maana wana nguvu wakiwa ndani ya ccm tu.

Wakiwa nje ya ccm hakuna atakaye wasikiliza na wataishia hivyo hivyo kuwaya waya tu.


20220711_062432.jpg
 
Back
Top Bottom