Wafu Walio Hai

Wafu Walio Hai

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
360,354
Reaction score
829,542
Unaweza kudhani najichanganya sasa kwa post zangu mwenyewe! La hasha kuna kitu tofauti kabisa kwenye hii mada
Nazungumzia wale wapendwa wetu walitwaliwa kutoka maisha haya lakini unahisia za ukaribu kabisa kuwa hawako mbali nasi, na kuna wakati tukiwa pekeyetu tunahisi kabisa tuko nao pamoja, ni experience ya ajabu na ni tofauti kabisa na ndoto za usiku
Inawezekana kabisa ni hallucinations lakini kwanini itokee kwa hawa baadhi tu na si wengine wote? Je ni kweli wamekufa ama wapo hai kwa namna nyingine? Kwakuwa zile hisia za uwepo wao huwa halisi kupita kawaida
Mara nyingi huwa ni wazazi ndugu watoto jamaa marafiki na hata majirani, sometimes ni watu ambao wala hatukuwa na ukaribu nao lakini tulifahamiana... Kifo kina siri nyingi na hii ni mmojawapo.... Wafu walio hai
Usuwaze kuwa kafaje, usiwaze ushirikina wala misukule, wengine hufa vifo vya kawaida kabisa tena baada ya kuugua muda mrefu......
Maajabu ni mengi dhana ni nyingi kwenye hili lakini moja linaloweza kuwa na hakika zaidi ni mawasiliano ya kiroho yaliyopo kati ya Wafu na walio hai
Jihadhari usibebebwe na dhana potofu unapokumbana na hiyo hali kisha ukawasimulia walimwengu watakaokuja na dhana za misukule! Ama kurogwa! Jihadhari sana! Mawasiliano ya wafu na walio hai ni mengi na hutokea kwa namna tofauti tofauti.... Ni kila kitu ni uchawi ... Vingine ni asili ambavyo ufahamu wa kibinadamu haujavipatia majibu yote.... Wafu waishio ni mfano hai na halisi
525f20d9e80344aaa91d1f6deb561a30.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mshana jr" ni kwel wakati mwingine wafu huwakinga na majanga wapendwa wao walio hai?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nakumbuka kuna siku nilikua napita njiani peke angu nikakutana na mbwa. Huyo mbwa alikua ananiangalia kwa upole sana then akawa ananifuata aliniisindikiza mpk home ndo akarudi alikotoka. Siku ile niliwaza sanaa
 
Mimi naamini kuwa:

Mtu akishakuwa Mfu hana mawasiliano tena kwakuwa hawezi kuzungumza wala kufanya lolote. Labda kama Hakufa.

Hiyo ya kuwasiliana na walio hai ni imani potofu tu/uzushi. Au ni mbinu za kishetani katika kuwafanya watu waogope.

Mtu akifa...basi Amekufa na hakuna organ yake yoyoye ifanyayo kazi na organs ndizo zinawezesha mawasiliano.
 
Naamini sana ktk hilo ni kweli sio ushirikina nadhani ni nature. Kama kuna mpendwa wako alikufa basi atakuja kwa njia nyingi na huwa wanaatuombea na kutulinda sometymz.
 
Sisi wakatoliki tunaomba watakatifu marehemu watuombee
 
Naamini sana ktk hilo ni kweli sio ushirikina nadhani ni nature. Kama kuna mpendwa wako alikufa basi atakuja kwa njia nyingi na huwa wanaatuombea na kutulinda sometymz.
Wewe ulishajiwa na mpendwa wako yeyote aliyekwishakufa?
 
Nilifiwa na mtu wangu wa karibu miaka mingi tuu imepita msiba ule ulikaa wiki tukisubiri kuzika. Siku ya nne tangu msiba utokee usiku niliota amenijia nilipo lala na akaniambia kitu ambacho anakiona kwangu na sikuwa nimemwambia mtu yeyote kuhusu hicho kitu yaani hakuna aliyekuwa anajua. Na kabla hajafa hatukuwahi kuongea nae kuhusu hilo jambo wala linalofanania na hilo na wala yeye hakuwa anahusika au kuwa na ujuzi wa hayo mambo. Kulipo kucha niliogopa sana nikajiuliza inamaana marehemu ameniona yaani kwenye ulimwengu wa roho amejua kilichonikumba/kilichonisibu. Basi nikajua ni roho yake ndo iliongea na nafsi yangu kwenye ulimwengu wa roho.

Kingine kuna mtu wangu wa karibu nae amekufa siku nyingi pia alikuwa akiniasa na kunifundisha mambo mengi mno ya maisha. Huyu alikuwa kila akimaliza kuniasa au kunielekeza jambo humalizia na msemo...."mtanikumbuka kwenye maisha yenu hata nikifa mtanikumbuka haya niwaambiayo. ...." hadi niandikapo hapa sauti yake bado naisikia masikioni mwangu kana kwamba nimekaa nae hapa mezani tunazungumzia jambo.

Asante mshana jr kunifikirisha na kunikumbusha zamani.

Michyuuuu.
 
Mimi naamini kuwa:

Mtu akishakuwa Mfu hana mawasiliano tena kwakuwa hawezi kuzungumza wala kufanya lolote. Labda kama Hakufa.

Hiyo ya kuwasiliana na walio hai ni imani potofu tu/uzushi. Au ni mbinu za kishetani katika kuwafanya watu waogope.

Mtu akifa...basi Amekufa na hakuna organ yake yoyoye ifanyayo kazi na organs ndizo zinawezesha mawasiliano.
Wewe unaamini HIVYO ni sahihi kabisa kwa imani yako ambayo hata hivyo haitandoa ukweli na uhalisia wa kile kilichopo na nilichoandika

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom