Wafanyakazi zaidi ya 700 wagoma mgodi wa Bulyanhulu

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,820
287,886
Posted Date::10/25/2007
Wafanyakazi zaidi ya 700 wagoma mgodi wa Bulyanhulu
Na Andrew Msechu
Mwananchi

WAFANYAKAZI zaidi ya 700 wa mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu Wilayani Kahama wamegoma kuanzia jana.

Taarifa zilizopatikana jijini Dar es Salaam jana zilielezea kuwa mgomo huo ulioanza asubuhi ni kwa ajili ya kuushinikiza uongozi wa mgodi huo kutekeleza makubaliano baina ya uongozi na Chama cha wafanyakazi Madini na ujenzi (Tamico) tawi la Bulyanhulu Oktoba 17.

Malalamiko hayo ni pamoja na utekelezwaji wa makubaliano ya kuondoa askari wa Kikosi cha Kuzuia Fujo (FFU) ndani ya eneo la mgodi huo, kwa kuwa kwa kuwepo kwa kikosi hicho katika eneo hilo kunawafanya wafanyakazi na familia zao kuishi kwa hofu.

Kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa na uongozi wa Barick, mgomo huo ulianza baada ya Tamico kuueleza uongozi wa mgodi huo juu ya adhma ya kuanza rasmi kwa mgomo huo jana, baada ya kutoona utekelezaji wa makubaliano waliyofikia.

Taarifa hiyo ilieleza kuwa uongozi ulilazimika kujibu barua hiyo na kuwashauri wafanyakazi hao kutogoma, kwa kuwa kwa kufanya hivyo ni kwenda kinyume na sheria na utaratibu na kwa kufanya hivyo uongozi huo utalazimka kuchukua hatua kali kwa maslahi ya kampuni ya Barick.

Hata hivyo taarifa hiyo ilieleza kuwa uongozi wa Barrick upo tayari kuendelea kutafuta ufumbuzi wa matatizo hayo kwa njia ya mazungumzo hadi kuhakikisha kuwa yanamalaizika.

Lakini hili haliwezi kufanyika iwapo wafanyakazi wanaendelea na mgomo, makubaliano yetu yalikuwa wazi kuwa tutaendelea kufanya mazungumzo hatua kwa hatua hadi tutakapoyapatia ufumbuzi kwa pande zote,? ilisema sehemu ya taarifa hiyo.

Hata taarifa hiyo ya Barick ilieleza kuwa uongozi umekuwa ukiendelea kuwaomba wafanyakazi wote kuendelea na kazi kwa mujibu wa utaratibu wao na kuahidi kuendelea kujali mikataba baina yake na wafanyakazi wote waliogoma.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom