Wafanyakazi wajipanga kumng'oa katibu Mkuu TUCTA

Watumishi wanatukanwa kama mbuzi hakuna hata mmoja wa kusimama na kulaani? waondoke kwanza hawana aibu hata kidogo, 2010 mtu anatamba mishahara ilikuwa 250,000 leo 300,000 ongezeko elfu 50,000 kwa miaka sita? jamaa hana soni hata kidogo
 
Laki 3 ni mshahara wa kibarua siyo wa mtu na familia yake, huku bado makato na mtu anatamba, je yeye analipwa shs ngapi na TUCTA? aibu yake huyu babu.
 
wamechelewa sana kumtoa kwani vitu vingi wanavyolaumiwa serikali kama kungekuwa na vyama imara vya wafanyakazi kusingekuwa na manyanyasho na pia pesa za wafanyakazi zilizoko kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii kutumika kwa miradi ya serikali
 
Mkutano Mkuu wa Wafanyakazi, TUCTA leo

Waziri Mkuu kahutubia

Mgaya kasoma risala ila kasahau ishue muhimu FAO la Kujitoa..

Anaongelea Mikataba, amesahau Ufisadi kwenye hii Mifuko

Huyu Jamaa amezeeka, hafai pale TUCTA
 
Back
Top Bottom