Wafanyakazi wa mochwari ya Mwananyamala wapasua maiti kuuza madawa ya kulevya waliyoyakuta

Nucky Thompson

JF-Expert Member
Sep 20, 2016
1,817
4,059
Kamishna wa polisi Dar Simon Sirro amesema wamekamata watu 4 ambao ni wafanyakazi wa mochwari ya Hospitali ya Mwananyamala kwa kupasua maiti ya raia wa Ghana aliyekutwa amefariki tarehe 14/3/17 Red Carpet Guest House Sinza

Wafanyakazi wa mochwari hiyo walipata taarifa mwili huo una madawa ya kulevya na kuupasua na kuyatoa na kuyauza, wamekiri kufanya hivyo na kutoa kete 32 na polisi walifanya uchunguzi na kumkamta huyo aliyeuziwa na hayo madawa, walimhoji pia na kumkamata aliyemuuzia ambaye anaitwa Ali Nyundo amabaye alitajwa na Makonda kwenye list yake na alipimwa akaonekana ni mtumiaji

Kweli elimu hata kama haina faida bado ina umuhimu.
Badala ya kumpasua huyo maiti, si wangeingiza tu mkono kwenye tigo na kuyafikia hayo madawa bila kumpasua? Ona sasa wamejitia hatiani. Kuingiza mkono kupitia tigo kusingekuwa na ushahidi wa kuwatia hatiani kwa kuwa kusingekuwa na mshono wowote.
 
"Mapato yameshuka" teh teh teh PRA(Police Revenue Authority) Bwana!

BTW hivi hayo madawa yakikamatwa wanayapeleka wapi?
 
Polisi wa Usalama Barabarani sasa hivi wanashindana na mashirika kama TANAPA na TRA kwa kukusanya maduhuli. Makosa ambayo mtu anapaswa kuonywa wanalikuza hadi wachukue elfu 30. Mabosi wao wawape vitabu vya risiti halali ili watoe wanapochukua faini siyo kuwaambia watu wakachukue risiti ofisini. Mtu unakamatiwa Segera hupewi risiti unaambiwa kachukue Korogwe wakati wewe unatokea Tanga ni upumbavu usiokubalika.
 
Ila mleta uzi alikusudia kuongelea hao watumishi wa umma waliofanya uhalifu wa kumsachi marehemu na kuchukua hayo madawa haramu
 
Kweli elimu hata kama haina faida bado ina umuhimu.
Badala ya kumpasua huyo maiti, si wangeingiza tu mkono kwenye tigo na kuyafikia hayo madawa bila kumpasua? Ona sasa wamejitia hatiani. Kuingiza mkono kupitia tigo kusingekuwa na ushahidi wa kuwatia hatiani kwa kuwa kusingekuwa na mshono wowote.
mmmmh kwenye tigo?? Watu mna ujanja
 
Ndi mchezo wao hata mimi kuna siku nilivyoenda kuchukua maiti na wenzangu kuna mchezo kama huo tuliuona sema walipotezea kiutu uzima sana na sisi tukaupotezea
 
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro amefunguka kuwa wahudumu wa mochwari ya Mwananyamala wameiba jumla ya kete 32 za dawa za kulevya zilizokuwa kwenye mwili wa Raia wa Ghana aliyefariki dunia akiwa katika nyumba ya wageni 14/ 03/ 2017 kwenye nyumba ya wageni ya 'Red Carpet' na alichukuliwa na kupelekwa mochwari Mwananyamala lakini inaonekana wale wahudumu walipata taarifa kuwa ule mwili una dawa za kulevya.

"Kimsingi walikula njama wakampasua na kutoa kete 32 za madawa ya kulevya na baada ya kuyapata waliyauza hayo madawa"alisema Sirro

Kamanda Sirro aliendelea kusema kuwa mpaka sasa wanawashikilia watu wanne ambayo wamehusika katika jambo hilo.

"Mpaka sasa tunawashikilia watu wanne ambao wanakiri kupasua mwili huo ambao ni wahusika wakuu na ni wahudumu wa mochwari ya Mwananyamala lakini tumekwenda mbali zaidi baada ya kufanya upasuaji wamemuuzia nani naye amekatwa pia na anaeleza kuwa alinunua hayo madawa, lakini pia naye alichukua na kumuuzia mtu mwingine anayefahamika kwa jina la Ally Nyundo, huyu Nyundo tulishamkataga na kumpeleka kwa Mkemia Mkuu yeye alionekana ni mtumiaji, kimsingi tuna hao watuhumiwa wanne na huyo wa tano aliyekamatwa sasa tunaandaa jalada" alisisitiza Sirro
 
Back
Top Bottom