Wafanyakazi NSSF tumejiroga wenyewe

Wafanyakazi NSSF tumejiroga wenyewe

Mzalendo Kibwaya

New Member
Joined
Jan 8, 2020
Posts
1
Reaction score
2
Wakati mwingine upuuzi unapozidi mtu anaweza kufanya jambo bila kufikiria madhara yake hata kwake mwenyewe. Ni kama ile wapemba wanayoiita hasira za Mkizi ambazo humfanya aingie kwenye mtumbwi wa wavuvi yeye mwenyewe.

Nmekumbuka Hekaya za Abunuwasi jinsi alivyokuwa akikata tawi huku akiwa amelikalia. Ndivyo alivyofanya huyu bwana.

Siku mbili zilizopita, mfanyakazi mwenzetu aliandika jambo kuhusu uongozi wa NSSF bila kutushirikisha sisi wengine, pengine ana sababu zake za msingi, lakini kiukweli ametuumiza sana watwana sisi.

Amesababisha tupoteze matarajio yetu ya miaka mingi kuhusu maslahi, na sijui atatulipaje. Natamani hata kumsomea dua Shetani huyo ili apotee kabisa maana ameua nafsi zetu kimaslahi.

Katika yote aliyoyaandika lililonikera ni lile suala la NSSF Hiari. Hebu fikirieni wafanyakazi wenzangu, NSSF Hiari iliwekwa kwenye ripoti ya CAG na ikafikishwa hadi kwenye Kamati ya Bunge ya Fedha za Serikali, na ikaonekana mwajiri hakutakiwa kutoa asilimia 10 kuwachangia wafanyakazi kwenye NSSF Hiari, kwa sababu sheria inamtaka mwajiri amchangie mfanyakazi kwenye Mfuko mmoja tu wa lazima, na si wa hiari. Na kuchangia sehemu mbili mwajiri alikuwa anakiuka sheria kwa kuchangia zaidi ya asilimia anayotakiwa kuchangia.

Ina maana huyu jamaa hajui kuwa tunachangiwa PSSSF asilimia 15 na sisi tunakatwa asilimia 5 (HAJUI HILO ?). Majinun huyu bila kutuuliza sisi wengine akaenda kuibua mtandaoni kuwa kile tulichokuwa tunachangiwa kwenye NSSF Hiari ni halali yetu, wakati tayari ilikuwa ni oditi kwere. Sisi wenye ufaham tulijaribu kupenya kwenye uongozi, ili itafutwe namna ya kunusuru schem yetu na tayari wawakilishi wetu walishaifanya kazi hiyo ili schem yetu iendelee. Ilikuwa imebaki wiki mbili tu matunda ya kuinusuru schem yetu yangeonekana. Sasa huyu mwanaizaya akatibua nyongo.

Ina maana alikuwa hajui kuwa sheria inataka tuchangiwe kwenye PSSSF asilimia 15 tu ? Sasa kwa kuchanganya asilimia 10 tulizokuwa tukichangiwa PSSSF na asilimia 10 za huku NSSF Hiari tayari imeshakiuka sheria, je, ni mwajiri gani makini angeendelea kuchangia wakati anajua kuwa ni kinyume cha sheria, na Kamati ya Bunge na hata CAG mwenyewe alikuwa akisubiri majibu kwa nini tunchangiwa mara mbili ?

NAANDIKA NIKIWA NA UCHUNGU MKUBWA SANA NA TENDO ALILOFANYA ZIRAILI HUYU.

Naweza kutabiri kuwa maamuzi yatakayofuata itakuwa ni kurudishiwa michango yetu tu kama schem itafungwa kwa kuwa hatuna uhalali wa kudai ile asilimia 10 aliyochangia mwajiri. Kama tungevuta subira, shcem ikaendelea tungeokoa zote bila kuondolewa zile za mwajiri.

Sasa wafanyakazi wenzangu tunaopenda mitandao tusaidiane jinsi ya kunusuru hili, tukapige magoti kwa DG au Mwenyekiti wa Bodi kama watoto wakosefu tusipoteze kwa ujinga wetu kile tulichochangia kukipanda.

Yale mengine aliyoyaandika hayanisumbui akili akili kwa kuwa nafahamu undani wake. Mimi huwa napenda haki, kwa hiyo nilifustilia kuona yale mengine yamekaaje. Ngoja nishee na ninyi kidogo, mkitaka na nyie mtafuatilia kwa wakati wenu.
  1. Ubaguzi wa wafanyakazi
    Wafanyakazi waliohamishiwa kwetu kutokea PSSSF waliletwa kujaza mapengo yaliyoachwa wazi kwa sababu mbalimbali. Kwa mfano ule wizi uliotokea hapa makao, ambapo wajamaa walikwepua bilioni 2 na laki moja ulisababisha mapengo kwenye uhasibu. Sasa tulitaka wahasibu walioletwa waende mikoa ipi kulikoibiwa hizo fehda wakati gepu liko Dar. Sasa hizi hawa wageni wana uwezo wa kudhibiti wizi hata kutokea makao makuu. Sasa wenzetu wameona mwanya wa kuiba umezibwa wanatushawishi tuwachukie watumishi wa umma kama sisi waliohamishiwa kwetu. Halafu jamani hawa wageni hawakutokea PPF, wametokea PSSSF tusije tukaona wajinga kwenye kuandika kwetu.
    Pia mikoani kwetu nimeona kuna wa kutoka PSSSF mfano Meneja wa Arusha, Songwe, Morogoro, na Dodoma.
  2. Ubaguzi kwenye mishahara
    Kuna Mhasibu amenipa data kuwa mishahara wanayoipata hawa waliotokea PSSSF wamekuja nayo wala hawajaongezewa hapa. Kila mtu aliyehamishwa amelekuja na kitu kinaitwa service particulars ambazo zimetaja kabisa mshahara wake. Mbele ya erio hakuna anayeweza kuthubutu kuongeza mshahara mwenyewe.
  3. Udanganyifu katika utendaji wa Shirika
    Kama tunakumbuka sote, kuna kikao alikiitisha Mheshimiwa Raisi Magufuli, cha wadau wa mambo ya Hifadhi ya jamii. Hadi tarehe 28 Disemba 2018 NSSF ilikuwa na wanachama 448,000 tofauti na taarifa zilizokuwa zikitolewa na uongozi uliopita kuwa kuliuwa na wachana milioni 1,000,000.
    Kwa kuzingatia taarifa hizi NSSF ilipanga kufikia wanachama 1,582,247 ifikapo Juni 2019. Sasa lengo hilo lisingewezekana kwa sababu hata msingi wake ulikuwa takwimu za uongo. Kwenye review ya nusu mwaka ilikuwa lazima kurekebisha kuwa wanachama walikuwa laki nne sio milioni moja ili lengo liwe la kweli.
    Kwa asiye na akili au kwa mwenye nia ya kutuvuruga ndio anasema malengo yameshushwa. Mtu unaweza kujikuta unatukana bure.
  4. Michango kutoka PSSSF
    Katika utaratibu wa kuhamishiana wanachama baina ya Mifuko ya NSSF na PSSSF, michango ya wanachama haikuhamishwa bali ni wanachama pekee ambao wamehamishwa. Baadhi ya waajiri waliendelea kuwasilisha michango katika mfuko wa awali hasa waajiri wa sekta binafsi waliokuwa wakichangia PSSSF. Zaidi ya bilioni 38 zimepelekwa PSSSF badala ya kuletwa kwenye mfuko wetu. Taratibu za kurudishiana zinaendela baina ya mifuko, kwa hiyo hata hilo ongezeko la makusanyo kwa mwaka 2018/19halikutokakana na fedha kutoka PSSSF bali lilitokana na mikakati mbalimbali iliyokwa na Menejimenti na Bodi ya Wadhamini katika kuongeza mapato ya Shirika.
    Mikakati mbalimbali niliyofanikiwa kuiona ni;-
  • Michango kukusanywa kupitia GePG
  • Kufanya ukaguzi wa mara kwa mara kwa kutumia wafanyakazi wengine wa ndani tofauti na wale waliokuwa wakifanya kazi hizo siku zote
  • Kuwaondoa wafanyakazi wasio waaminifu
  • Ushirika na TRA kuwatambua waajiri wasiochangia NSSF
  • Kuanzisha billing system kuanzia mwezi wa 4 2019
  • Kuchukua hatua stahiki kwa waajiri wasiotimiza wajibu wao.
  1. Mikopo ya mabenki
    Jamani kwenye Uislamu tunafundishwa kutosema uongo. Sisi wenyewe, kwenye Mkutano wetu na DG pale kwenye ukumbi wa Mwalimu Nyerere tulimwomba DG turuhusiwe tuanza kukopa kwenye mabenki kwa sababu menejimenti iliyopita wazuia utaratibu huo. Leo hii sisi wenyewe tunautuhumu uongozi kwa hilo. Astaghafirulah. Ee mola tuepushe na moto wa jahanam. Mnataka Menejimenti ituzuie kukopa ? Kama wewe hutaki usituharibie hapa.
    Pamoja na yote, Mheshimiwa DG naomba utusaidie kwa sababu huyu mtu na wenzake wachahe wanataka menejimenti imeamini kuwa tumemtuma. Sisi wafanyakazi wengine waminifu tuko pamoja na menejimenti katika kuhakikisha ustawi wa Shirika letu. Tutakuwa tunakuletea majina ya baadhi ya waharibifu hawa wanotaka menejimenti ionekane haifai. Tunawajua mheshimiwa, na wengine wako karibu na wewe. Hawa wa ndani wanashirikiana na wachache waliohamishwa kutoka NSSF, akina Kirondera na genge lake. Wanapinga juhudi zako na juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais wetu mpendwa Mheshimiwa Dr. Johs Pombe Joseph Magufuli.
    Hawa wenzetu wanajaribu kuharibu kwenye maeneo mengi na tunayafahamu na jinsi wanavyofanya. Tutakupa taarifa tu Mkuu lakini Mungu atakulinda na utayashinda mabaya yote yanayopangwa. Inshallah.
    Ushauri wa bure kwa wana NSSF wakongwe na hata wale wapya kuwa tutumie njia zetu za ndani kutatua matatizo yetu ya ndani, kwa sababu hata kile unachoona ni kidogo kimaslahi huku, kuna mtu huko nje hakipati. Tukiendelea kutembea hadharani bila nguo kwa kufichua usiri wetu kuna siku tutapoteza hata kile tulichonacho. HAPO TUTAMLILIA NANI ?
    Halafu ni bora hata kuandika ukweli uongo ni mwiko kwetu waislamu. Nimelazimika kunukuu baadhi ya makatazo kwa faida yetu kutoka kwenye Qur’an Tukufu
380. Allah swt anatuambia katika Qur’an Tukufu, Surah An-Nahl 16, Ayah ya 105,

إِنَّمَا يَفْتَرِي الْكَذِبَ الَّذِينَ لَا يُؤْمِنُونَ بِآيَاتِ اللَّهِ ۖ وَأُولَٰئِكَ هُمُ الْكَاذِبُونَ

Wanaozua uwongo hawana imani

381. Vile vile Mtume Muhammad s.a.w.w. amesema:

Mtu mwovu kabisa ni yule ambaye ni msema uwongo.”

382. Mtume Muhammad s.a.w.w. amesema:

“Allah swt humlaani mwongo hata kama atasema ukweli”

383. Mtume Muhammad s.a.w.w. amesema:

“Jitahadharisheni, Mimi ninawaambieni dhambi Kuu kabisa katika Madhambi Makuu:

Kumshirikisha Allah pamoja na mtu mwingine

Wazazi kukufanya Aaq

Na kusema uwongo

384. Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s. amesema:

“Ugonjwa wa kusema uwongo ndio ugonjwa mbaya kabisa.”

385. Vile vile Imam Hasan al-‘Askari amesema katika Mustadrad al-Wasa'il, Kitabu Hajj, mlango wa 12:

“Maovu yote yamefungwa katika chumba kimoja kwa kufuli, na uwongo ndio ufunguo wake.”

386. Amesema al-Imam Musa ibn Ja’far a.s:

“Mtu mwenye busara kamwe hawezi kusema uwongo hata kwa matamanio yake mwenyewe.”

Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s. amesema:

“Itakuwa vyema kwa Waislamu iwapo hawatafanya urafiki na udugu pamoja na Mwongo.”

Amesema al-Imam Muhammad al-Baqir a.s. katika Al-Kafi, j.2:

“Uwongo unateketeza misingi ya Imani.”


380. Mtume Muhammad s.a.w.w. amesema katika Al-Mustadrak al-Wasail:

“Mumin anaposema uwongo bila ya shida yoyote, basi Malaika elfu sabini humlaani!”

“Na hutoka harufu mbaya kabisa kutokea moyoni mwake, harufu hiyo hufika hadi ‘arsh.”

“Na Allah swt humwandikia kwa dhambi hilo moja, madhambi sabini ya zinaa na zinaa zenyewe si zinaa za kawaida bali zinaa pamoja na mama yake.”


Asalam Aleikhum

Nakutakieni jioni njema yenye barak za Mola wetu

Kibwaya
 
This is so real and Trueeeeee, Wachache wapenda kunufaika wamebanwa kufabya ubadhilifu wanakimbilia JF kutupa maneno ya uongo
 
Mmemtaja Brother K. Yule anaitwa Kabuyenze Kirondera. Huyu jamaa alihamishiwa huku RITA akitokea NSSF. Huyu jamaa amekuja kuripoti akiwa amebeba kiti chake ambacho kinafanana na viti vya wafalme wa kale.

Kuna ktu kanitonya kuwa huwa amekuwa na tabia ya kuhama na hicho kiti kila anakokwenda. Hicho kiti kina siri gani? Tena wengine wanasema ni mtu kama si wa Burundi ni wa Rwanda.

Hivi mtumishi wa umma anaruhusiwa kuja na kiti chake kwenye ofisi za umma. Tujuzeni mnaoyajua mambo hayo?
 
Ukweli tumechoshwa na watu wanaotuvuruga NSSF. Mheshimiwa DG tafadhali washughulikie wote wenye nia ovu ya kuupaka matope mfuko wetu.

Kwenye shirika hili kuna makundi kadhaa ya watu ambao wapo kwa ajili ya kuvuruga kama njia ya kutete makundi ya tawala zilizopita.

Wafanyakazi wengi wa NSSF ni ndugu wa wale wanaopambana na Menejimenti, kila linalofanywa katika shirika wao wanakwenda kujadili huko majumbani mwao. Nia yao kubwa ni kuuonyesha Umma na Serikali kuwa utawala wa Mkurugenzi Mkuu Fulani ambaye alikuwa ndugu yao ndio unaofaa.

Mr. Erio wewe ni mteule wa Raisi ni bora umshirikishe Raisi kuhusu hayo makundi na viongozi wao walioko ndani na nje.
Ukiwauliza wafanyakazi wakongwe watakutajia mpaka majina ya vikundi na wahusika. ni makundi hatari sana hayo believe me. Unahitaji msaa da wa Dola kuyaweka sawa
 
Noma kwa kweli, watu wanabeza maendeleo
Ukweli tumechoshwa na watu wanaotuvuruga NSSF. Mheshimiwa DG tafadhali washughulikie wote wenye nia ovu ya kuupaka matope mfuko wetu.
Kwenye shirika hili kuna makundi kadhaa ya watu ambao wapo kwa ajili ya kuvuruga kama njia ya kutete makundi ya tawala zilizopita.
Wafanyakazi wengi wa NSSF ni ndugu wa wale wanaopambana na Menejimenti, kila linalofanywa katika shirika wao wanakwenda kujadili huko majumbani mwao. Nia yao kubwa ni kuuonyesha Umma na Serikali kuwa utawala wa Mkurugenzi Mkuu Fulani ambaye alikuwa ndugu yao ndio unaofaa.
Mr. Erio wewe ni mteule wa Raisi ni bora umshirikishe Raisi kuhusu hayo makundi na viongozi wao walioko ndani na nje.
Ukiwauliza wafanyakazi wakongwe watakutajia mpaka majina ya vikundi na wahusika. ni makundi hatari sana hayo believe me. Unahitaji msaa da wa Dola kuyaweka sawa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi nyie watumishi si mnatakiwa kuweka vitu mnavovijua mkiwa kwny ajira zenu viwe 'confidential'...
Ni nini hii hadi kutaja majina ya watu?..
 
Lakini hii nssf makini ya urio,mbona hatuoni lolote linaloendelea?.
Hakunaga kiwanda,hakunaga hata ujenzi wa choo,,tabu gani?
 
Back
Top Bottom