Wafanyabiashara wenye maduka Kariakoo wagoma kufungua Maduka wakipinga mashine za TRA

bila shaka hata Ritz aliimba kauli mbiu hiyo....habari njema sana
 
Last edited by a moderator:
Buku 7 kwenye huu uzi wanaingia na kutoka haraka sana, hawana uzushi wa kuweka kwenye uzi huu.
 
Hapa naona kuna matatizo mawili yamsingi:-
La kwanza ni uelewa mdogo wa wananchi/wafanyabiashara juu ya maana na umuhimu wa kulipa kodi(ambapo EFDs zinarahisisha ukusanyaji wa mapato.)
Endapo wananchi watapata elimu juu ya faida/umaana wa wao kulipa kodi kwa serikali na umuhimu wa wafanyabiashara kutumia mashine za risiti sizani kama ghasia za namna hii zitajitokeza tena kwani naamini vurugu hizi zinatokana na wao kutokuelewa.

Tatizo la pili ni baadhi ya watu kuwa wabinafsi kwa kiwango kilichopitiliza hata wanathubutu kusabotage mipango mizuri ya serikali ili kujinufaisha.
Bado sijapata ushahidi wa kutosha juu ya uwepo wa mikono ya wanasiasa flan katika hili la kugomea EFDs lakini kitendo cha wafanyabiashara kukiimba chama flani wakati wa mgomo ni moja ya ushahidi.
NITOE RAI KWA SERIKALI KUFANYIA KAZI TATIZO HILI.
KWA KUWA WAFANYABIASHARA WENGI WANALALAMIKIA GHARAMA YA KUNUNULIA HIZO EFD BASI UANGALIWE UWEZEKANO WA KUWAPATIA KWA MAELEWANO YA KUZILIPIA KWA AWAMU NA PIA BEI ZISHUSHWE KWA KIWANGO CHA KUELEWEKA.
 
Kwa muda mrefu nimekua nikilisemea sana suala la watanzania wenzangu kuingiza SIASA kwenye kila kitu.
Wanasiasa walipanda vichwani mwetu mbegu hii na sisi tukaipalilia bila kufikiri kwa kina mpaka sasa matunda yake yanatutia upofu.
Tumekua wavivu wa kufikiri wenyewe badala yake tumeacha watu wachache(wanasiasa) watulishe mashudu kwa maslahi yao hivyo kujikuta tukifanya wapendavyo kama ng'ombe.
Nimeangalia habari ITV wafanyabiashara waliopata nafasi ya kuzungumza wamenisikitisha sana.
Wanadai hawazitaki EFDs sababu TRA wanaona kila wanachouza.
Wao ni mfano wa wenzao wengi wenye mawazo ya aina hiyo.
Kabla ya mh.Mkapa kufuta kodi ya maendeleo, watu walitambua wajibu wao wa kulipa kodi. Lakini sasa wafanyabiashara wanaambiwa walipe kadili ya wanavyoingiza wanagoma.
WATANZANIA TUAMKE NA KUANZA KUFIKILIA KWA MAPANA AMA TUTAJA JUTA SIKU ZA USONI.
"A mistake can be corrected at the threshold, carry it on with you and thou shalt suffer bitterly in its destruction"
-M.C
 
Serikali inapoteza mapato mengi kwa wafanyabishara wadogo na wakubwa kukwepa kodi. Mimi nadhani ni mwanzo mzuri, wafanyabiashara wanatakiwa wazoee. Kenya, hadi mtu mwenye kibanda cha CHIPS, ana EFD machine. Sina interest hapa ila naomba kusimamam upande wa TRA. Nimeona wafanyabishara wengine wanasema hawataki kulipa na 18% ni kubwa. Kama serikali itajadili kupunguza VAT sawa, lakini watu lazime walipe kodi. Serikali inapata kodi za wafanyakazi wake kwa kukata mishahara yao, sasa ni wakati wa wanyabiashara kupata elimu na kuanza kujua kwamba kodi ni wajibu na wakefeel pinch ya kodi, wataendelea kujifunza taratibu. Mabadiliko haya yana gharama ila lazima serikali iwe na msimamo, hii siyo division 5, inamezeka.

Mi nakuunga mkono wafanya biashara wengi wa Tanzania hawana elimu ya kulipa kodi,bidhaa nyingi tunazonunua kodi tunalipa sisi walaji nyie Wafanyabiashara ni kama mawakala wa kukusanya Kodi kwa niaba ya Serikali,sasa inapofika muda wa Serikali kupokea Kodi yake nyie wafanyabiashara munahisi kuwa fedha mlizokusanya kwa niaba ya Serikali nazo pia ni za kwenu acheni fikra zisizo sahihi! Tafakari
 
Kulipa kodi ni sawa. Lakini je, hao wengine wanaojitapa kwamba ndio wenye nchi wanalipa kodi? Taifa bila utawala wa sheria unaozingatia haki sawa kwa wote ni vurugu tu!!
 
Kwa muda mrefu nimekua nikilisemea sana suala la watanzania wenzangu kuingiza SIASA kwenye kila kitu.
Wanasiasa walipanda vichwani mwetu mbegu hii na sisi tukaipalilia bila kufikiri kwa kina mpaka sasa matunda yake yanatutia upofu.
Tumekua wavivu wa kufikiri wenyewe badala yake tumeacha watu wachache(wanasiasa) watulishe mashudu kwa maslahi yao hivyo kujikuta tukifanya wapendavyo kama ng'ombe.
Nimeangalia habari ITV wafanyabiashara waliopata nafasi ya kuzungumza wamenisikitisha sana.
Wanadai hawazitaki EFDs sababu TRA wanaona kila wanachouza.
Wao ni mfano wa wenzao wengi wenye mawazo ya aina hiyo.
Kabla ya mh.Mkapa kufuta kodi ya maendeleo, watu walitambua wajibu wao wa kulipa kodi. Lakini sasa wafanyabiashara wanaambiwa walipe kadili ya wanavyoingiza wanagoma.
WATANZANIA TUAMKE NA KUANZA KUFIKILIA KWA MAPANA AMA TUTAJA JUTA SIKU ZA USONI.
"A mistake can be corrected at the threshold, carry it on with you and thou shalt suffer bitterly in its destruction"
-M.C

bado upo gizani hujaelewa wanagomea wao ni bei ya machine. 1,000,000/- ni hela nyingi sana kumbuka hiyo machine itawasaidia TRA kukusanya noti nyingi, ni kitendea kazi chao

Kwa nini wasiwe kama TANESCO wanaogawa mita ? Bora ya TANESCO wanakupa umeme TRA waleta nini kwa gharama ya 1M?
 
  • Thanks
Reactions: Ame

Isije kuwa ni mradi wa wakubwa
 
Ccm wanaiba kwa wino wa kupigia kura toka china,ndiyo maana serikali haiwakemei wachina hapa tanzania kwa ujangili wa wanyama,madini,misitu wanaofanya
 
Kariakoo waliofunga maduka ni wale wakwepa kodi;
na hasa wale ambao hawajafunga mashine za tra.

Mashine ni laki nane, na mnaingia mkataba hela yako
inakuwa inarudishwa kidogo kidogo kutokana na makusanyo
hadi urejeshewe laki nane yako na mashine inaendelea kuwa ya tra. Ritz najua una biashara zako mitaa hiyo je hapa niko sawa?

Je mfanyabiashara asiyetaka kulipa kodi avumiliwe ili aiimbie ccm mapambio?

Na wale wachumia matumbo wa tra ndio wanahimiza wafanyabiashara wagome
kufunga hizo mashine ili wawe wanawapitia madukani kwao na kukusanya hela
ya kutia kwenye matumbo yao yasiyojaa; na serikali ikose mapato.

Tanzania itajengwa na wenye moyo, @chama cha mapinduzi kitaendelea
kuwepo hata bila mapambio na nyimbo za wakwepa kodi
.
 
Serikali haijali cha mchina wa mswahili vunja sheria uone moto wake,
Jana nilikuwa hapo polisi msimbazi centre, nimekuta wachina wamelundikwa
sero; wenzao wanahaha kuwawekea zamana.

Ccm wanaiba kwa wino wa kupigia kura toka china,ndiyo maana serikali haiwakemei wachina hapa tanzania kwa ujangili wa wanyama,madini,misitu wanaofanya
 
Kwa vyovyote vile tutashinda uchaguzi wa 2015, hata kama utakuwa ushindi mwembamba. Na hawa wafanyabiashara wasiponunua hizi machine tutaanza kuwatoza kodi halali. Si hawalipi kodi halali? Kodi ya 10,000,000/= kwa mwaka huwa wanalipa kati ya 1,000,000/= na 2,000,000/= kwa mwaka. Wanaona noma gani kutuunga mkono katika hili? Wawaulize wale warabu wawili wa Morogoro mmoja anaitwa Balaboooo na mwingine ni yule aliyewahi kuwa mbunge moroboro vijijini kupitia chama tawala.
 
bado upo gizani hujaelewa wanagomea wao ni bei ya machine. 1,000,000/- ni hela nyingi sana kumbuka hiyo machine itawasaidia TRA kukusanya noti nyingi, ni kitendea kazi chao

Kwa nini wasiwe kama TANESCO wanaogawa mita ? Bora ya TANESCO wanakupa umeme TRA waleta nini kwa gharama ya 1M?

kifaa hicha thamani yake halisi ni sh elf 50, ila wenyewe wanauza 1mil. Pia wanagomea kutozwa asilimia 18 ya mapato, na hawataki tra wajue ni vitu gan wameuza ili waendelee kuiibia serikali
 
Isije kuwa ni mradi wa wakubwa

Tunajiandaa na uchaguzi, tulitaka kusitisha fao la kujitoa mkapiga kelele, tumebuni hii nayo mnaandamana, pembe zetu za ndovu zinakamatwa, biashara yetu ya unga imetibuka... nachanganyikiwa hadi nahisi sukari na presha vinapanda kwa mpigo..
 
Dah ni ishu ya kufikiri...... Mfano TRA wakiwapa bure ni rahisi kuiharibu na kusema imeharibika!!! So LABDA aim yao ni kuwabana.....

Establish and sustain...period!!!!!!!!!

Ni authority hii unajua kwa nini mkurugenzi anateuliwa na Rais???!!!
Halafu ashindwe hili???!!!
Kwa fikira hizi umasikini hautaisha???!!

Wewe binafsi umeshachezea mita ngapi za luku na za maji??!!!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom