Wafanyabiashara wenye maduka Kariakoo wagoma kufungua Maduka wakipinga mashine za TRA

Ritz

JF-Expert Member
Jan 1, 2011
46,956
32,344
Wanaukumbi.

Wafanyabishara ambao wanamiliki maduka maeneo yote ya kariakoo leo asubuhi wameweka mgomo wa pamoja wakutofungua maduka yao wakipinga uamuzi wa TRA kutaka kila duka kuwa na mashine.

Mitaa yote ya Kariakoo, Msimbazi, Uhuru, Lumumba, Aggrey, Mchikichi, Narung'ombe, Tandamti, Congo, kote maduka yamefungwa baada ya kutangaziwa na umoja wa wafanyabiasha.

Wafanyabishara wanapinga bei kubwa ya mashine ambayo ni milioni moja mpaka lakini nane.

=======================
UPDATES...19.11.2013
=======================
Mgomo wa wafanyabiashara Kariakoo bado unaendelea maduka bado yamefungwa.

============================================================
UPDATE...9. Jan 2014
============================================================
==============================================
TRA%286%29%282%29.jpg

Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA)

Wadau wa biashara watakutana na wafanyabiashara nchini ili kutoa marejesho yaliyojadiliwa katika mikutano iliyowakutanisha Jumuiya ya Wafanyabiashara, Waziri wa Viwanda na Biashara, Waziri wa Fedha pamoja na Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA).

Mkutano huo unaotarajiwa kufanyika leo, utawakutanisha wadau hao ili kutatua changamoto za matumizi ya mashine za kielektroniki kutolea risiti (EFDs) na kuwasihi kuacha migomo. Mshauri na Msemaji wa wafanyabiashara wa Kariakoo, Johnson Minja, aliyasema hayo wakati akizungumza na NIPASHE jijini Dar es Salaam jana.

Alisema kuwa katika mkutano huo, ajenda zitakazojadiliwa ni tatu ikiwamo ya kutengeneza Jumuiya ya Wafanyabiashara ambao watawawakilisha wenzao.

“Tunataka kuchagua viongozi wapya watakaotutetea kwani waliopo wameshindwa kufanya hivyo,” alisema Minja.

SOURCE: NIPASHE

clip_image002%25255B4%25255D.jpg

2013-11-19+12.43.41.jpg

2013-11-19+12.45.46.jpg

Source: Ritz wa JF
 
daaah......naona kila sehemu hizo mashine zinagomewa....juzi zilileta kasheshe kubwa mji kasoro bahari
 
Wanaukumbi.

Wafanyabishara ambao wanamiliki maduka maeneo yote ya kariakoo leo asubuhi wameweka mgomo wa pamoja wakutofunga maduka yao wakipinga uamuzi wa TRA kutaka kila duka kuwa na mashine.

Wafanyabishara wanapinga bei kubwa ya mashine ambayo ni milioni moja mpaka lakini nane.

Source: Ritz wa JF

Tumeweka mgomo wa kutokufungua siyo kufunga. Nchi nyingine hizi machine hutolewa bure kwa wafanyabiashara hapa tunauziwa km mali zetu
 
Last edited by a moderator:
We riz kipindi mbeya wanagoma si ulisema nyie huko kariakoo mmeshaanza kutumia? Au sio wewe?
Ni kweli baadhi ya maduka walikuwa wanatumia na wengine walilipa pesa nusu, lakini leo wameungana wote kupinga hilo jambo.
 
Acha tu wagome, wakikaa wiki moja bila kuuza watafungua maduka wao wenyewe...

Bei ya mashine ni ghiliba tu, hawa wamezoea MFUMO CCM unaowafanya wasilipe kodi, sasa mashine za TRA zitawafanya walipe kodi. Haiwezekani serikali iendelee kukamua wafanyakazi kulipa kodi huku wafanyabiashara hawalipi kodi. TRA hakuna kulegeza uzi, hawa jamaa wa kariakoo wanaolipa chumba milioni mbili kwa mwezi hawashindwi kulipia mashine kwa laki nane, waache usanii walipe kodi. Nyambaaaaf
 
Wadau kuna mgoma unaendelea kariakoo asubuhui hii maduka yote yamefungwa, kisa kupinga mashine za efd za risiti, wafanya biashara wengi wanadhani mradi ni wa fisadi mwingine ambao una lengo la kumnyonya mtanzania wa hali ya chini.. Hakuna elimu iliyotolewa na kwa nini uuzwe kwa bei wanayotaka wao wakat wafanya biashara wengine wangeweza kuleta kwa bei ya chini.
 
Wanaukumbi.

Wafanyabishara ambao wanamiliki maduka maeneo yote ya kariakoo leo asubuhi wameweka mgomo wa pamoja wakutofunga maduka yao wakipinga uamuzi wa TRA kutaka kila duka kuwa na mashine.

Wafanyabishara wanapinga bei kubwa ya mashine ambayo ni milioni moja mpaka lakini nane.

Source: Ritz wa JF

Bravooooooo! Kiukweli huu ni wizi! unaweza kupata home theater au flat screen tv ya maana kwa laki 6 tu! sasa hiki kimashine hiki laki 9?

Kariakoo ndio Tanzania sasa tuone jeuri ya TRA!!!
 
daaah......naona kila sehemu hizo mashine zinagomewa....juzi zilileta kasheshe kubwa mji kasoro bahari

Kuna Afisa wa TRA kwenye Kipima Joto ITV majuma mawili yaliyopita alisema wafanyabiashara watarejeshewa fedha zao wanazonunulia mashine baada ya hesabu ya mwaka mmoja, MAJI SHINGONI
 
ni vizuri ukawa mgomo wa nchi nzima kabisa. mambo mengine ni ya kipumbavu kabisa. Kwa njia hii TRA wanaiongezea maadui serikali yetu sikivu.
 
Wanaukumbi.

Wafanyabishara ambao wanamiliki maduka maeneo yote ya kariakoo leo asubuhi wameweka mgomo wa pamoja wakutofunga maduka yao wakipinga uamuzi wa TRA kutaka kila duka kuwa na mashine.

Wafanyabishara wanapinga bei kubwa ya mashine ambayo ni milioni moja mpaka lakini nane.

Source: Ritz wa JF

Mkuu hapo kwenye RED unamaanisha "hawapo tayari kufunga maduka yao?"
Ila miccm kama kina Ritz na mingine sijawai kuona ikipost Mambo yenye maana humu.
 
Ritz Kumbe kuna wakati unakuwa na busara eee, hizi ndizo thread za kutuleta humu - hebu lamba Thanks yangu kwa mara ya kwanza, Jitambue ubadilike!!
 
Kuna mtu mmoja hapa msimbazi amejaribu kufungua kapigwa vibao duu! Ni mtu mzima amefunga mwenyewe bila kupenda.

Usiwaseme wenzio wakati ni miongoni mwao na kiduka chako uzushi ili usionekane fisadi, na pia kivuli cha kuficha biashara yako ulokamatwa nayo China. Lakini usijali kwani meno ya tembo bado unasafirisha.
 
Kuna Afisa wa TRA kwenye Kipima Joto ITV majuma mawili yaliyopita alisema wafanyabiashara watarejeshewa fedha zao wanazonunulia mashine baada ya hesabu ya mwaka mmoja, MAJI SHINGONI

Wanadanganya, alafu wasitufanye mazuzu wao TRA wanaposema watarudisha gharama zetu kwani wanatumia pesa zao za mfukoni? Hizo pesa si kodi zetu? Yaani miradi yao tugharamie kwa kodi zetu?

Hicho kimachine uchwara hakina hadhi ya kuuzwa laki 9! Waache uhuni! Hata dekoda za HD ambazo zinaunganishwa na mitandao yao kama Startimes ,Azam n.k haziuzwi zaidi ya laki?

Hizo machine wauze elfu 80 tu full stop hawataki tupa kule!!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom