Wafanyabiashara wengi ni wabinafsi

OMOYOGWANE

JF-Expert Member
Dec 30, 2016
3,626
9,173
Hellow wakuu,

Kutokana na ugumu wa ajira vijana wengi waliohitimu vyuo wamekuwa wakitaka kujiajiri.

Mfano mtu anataka kufanya biashara ya bucha, anamfuata mwenye bucha kiroho safi kutaka kupata taarifa sahihi ili na yeye akafungue bucha mkoa mwingine au wilaya nyingine, akaanza kwa kuulizia mtaji wa kuanzia ni kiasi gani?

Taratibu mbalimbali za upatikanaji wa leseni ya biashara n.k, Kijana atajibiwa short short tu au kupewa taarifa nusu makusudi, lakini akija kuanza utekelezaji anagundua kuna mambo mengi alifichwa.

Hata hapa jukwaani wapo watu wengi tu tena wasomi waliojiajiri lakini ukitaka akufunulie kuhusu undani wa biashara anayoofanya ili na wewe ukafungue eneo la mbali(wilaya nyingine) hautapata taarifa yeyote.

NB: Mimi ni shuhuda

Swali: Je, umewahi kukumbana na hali kama hii? Je kwanini wafanyabiashara ni wabinafsi?
 
Hata mimi wakati naanza biashara yangu ya aiskirimu, juice na umama n`tilie kuna vitu vingi nilifichwa lakini kwa sababu nilikuwa nafanya kitu ambacho nakipenda yaani kupikapika sikufa moyo nilianza mzima mzima kwa kile kidogo nilichokuwa nacho.

Nadhani wengi hawasemi ukweli kwa sababu zao binafsi tu au pengine ni uchoyo wa maarifa.
 
Hata mimi wakati naanza biashara yangu ya aiskirimu,juice na umama n`tilie kuna vitu vingi nilifichwa,lakini kwa sababu nilikuwa nafanya kitu ambacho nakipenda yaani kupikapika sikufa moyo nilianza mzima mzima kwa kile kidogo nilichokuwa nacho,.nadhani wengi hawasemi ukweli kwa sababu zao binafsi tuu au pengine ni uchoyo wa maarifa.
Lunch leo inanihusu kwako wapi tuje
 
Mkuu.....

Biashara ni kitu kingine na ubinafsi ni jambo lingine.

Selfishness ni tabia ya mtu, haina uhusiano kabisa na biashara.

Mfano mzuri tu, hapa ndani naona jinsi vijana ambavyo hampeani taarifa sahihi kuhusu ajira, ndoa nakadhalika.

Lakini pia, kama kweli unahitaji kufanya jambi flani, yes yawezekana usipate taarifa sahihi kama utakavyo hitaji lakini kama kweli unayo nia na umedhamiria basi lazima utatoboa.
 
Haya mambo yapo kila sehemu, kumbuka hakuna mtu anaetaka ufanikiwe hapa duniani japo wachache wana mioyo mizuri tu kwani hii ni tabia ya mtu tu.

Cha muhimu usikate tamaa unapoamua kufanya jambo lako.
 
Back
Top Bottom