nngu007
JF-Expert Member
- Aug 2, 2010
- 15,862
- 5,797
[h=2][/h]JUMAMOSI, SEPTEMBA 01, 2012 06:25 NA OSCAR ASSENGA, KOROGWE
WAFANYABIASHARA wa Soko la Manundu lililopo wilayani Korogwe, wameiomba Serikali kumuwekea ulinzi wa kutosha Mkuu wa Wilaya hiyo, Mrisho Gambo, kutokana na uchapakazi wake unaotaka kukwamishwa na baadhi ya watendaji katika Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe.
Kauli hiyo ilitolewa na wafanyabiashara wa soko hilo kwa nyakati tofauti, baada ya kuona taarifa zikieleza kuwa Mwanasheria wa Halmashauri ya Wilaya hiyo, Nujum Tekka, anakusudia kumburuza mahakamani baada ya kuwatetea wafanyabiashara hao na kumaliza mgogoro uliokuwapo kwa kipindi cha muda mrefu.
Mwenyekiti wa soko hilo, Mussa Hussein, alilieleza MTANZANIA kuwa maneno ya mwanasheria huyo aliyoyatoa hivi karibuni kuwa kadhalilishwa si kweli, kwa sababu yanaonekana dhahiri kukwamisha jitihada zinazofanywa na DC huyo.
Alisema jitihada za kiongozi huyo zimeanza kuonekana toka alipoingia wilayani hapo kwa kutembelea soko hilo na kutatua kero mbalimbali, ikiwamo kuhakikisha linakuwa katika hali ya usafi.
Alisema baada ya DC huyo kufanya ziara ya kutembelea soko hilo aliweza kuelezwa mgogoro uliokuwapo kwa muda mrefu kati ya halmashauri na wafanyabiashara sokoni hapo, ambapo aliamua kuwaita pande zote na kufanya kikao cha Kamati ya Ulinzi na Usalama.
Aidha, alisema katika kikao hicho kulifanyika makubaliano pande zote kwamba wafanyabiashara katika soko hilo walipe kodi kwa halmashauri hiyo kama ilivyokuwa hapo awali.
Alisema baada ya makubaliano hayo waliondoka na mwanasheria naye aliondoka na walipofika mahali walikoafikiana kukutana waliamua kumpigia simu na aliwaambia wakutane mahakamani, kitu ambacho kiliwashangaza wafanyabiashara hao.
Alisema walipofika mahakamani mwanasheria aliyekuwa upande wa soko alishindwa kuzungumza, hali iliyowapa wakati mgumu na kushindwa kueleza wafanye nini kama mwanasheria huyo aliamua kufanya hivyo.
Alisema mgogoro ulikuwapo tokea Julai, mwaka huu baada ya wafanyabiashara hao kupandishiwa kodi kinyemela na kuamua kwenda mahakamani kwa ajili ya kupata ufumbuzi wa suala hilo.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Stendi ya Mabasi ya Korogwe, Wilfred Tesha, alisifu jitahada za DC huyo na kusikitishwa na hatua ya baadhi ya vikundi vya watu vinavyotaka kumchafua.
Kiukweli jitihada za Gambo zinaleta mafanikio na kuna baadhi ya vikundi vinatengenezwa kupunguza kasi yake, hivyo tunamuomba Rais Kikwete aendelee kumlinda na kumbakiza hapa hapa, alisema Tesha.
Alisema kesi iliyokuwapo baina ya wafanyabiashara hao na Halmashauri ya Mji ilidumu kwa kipindi cha miaka miwili na kusababisha DC huyo kuamua kuingilia kati na hatimaye wafanyabiashara hao wakapata haki yao.
Sisi kama wafanyabiashara wa Soko la Manundu hatutakubali Mrisho Gambo kuondoka Korogwe, tutaandamana na ikiwezekana kumwaga damu kwa sababu kiongozi huyo ni mtu mwenye kupenda maendeleo, lakini baadhi ya watu wanataka kumchafua, kwa hali hiyo hatutakubali, alisema Tesha.