Wafanyabiashara wataka DC Korogwe apewe ulinzi; Ni juu ya Ugomvi na Mwanasheria Ms. Nujum Tekka | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wafanyabiashara wataka DC Korogwe apewe ulinzi; Ni juu ya Ugomvi na Mwanasheria Ms. Nujum Tekka

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by nngu007, Sep 4, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Sep 4, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  [h=2][/h]JUMAMOSI, SEPTEMBA 01, 2012 06:25 NA OSCAR ASSENGA, KOROGWE

  WAFANYABIASHARA wa Soko la Manundu lililopo wilayani Korogwe, wameiomba Serikali kumuwekea ulinzi wa kutosha Mkuu wa Wilaya hiyo, Mrisho Gambo, kutokana na uchapakazi wake unaotaka kukwamishwa na baadhi ya watendaji katika Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe.

  Kauli hiyo ilitolewa na wafanyabiashara wa soko hilo kwa nyakati tofauti, baada ya kuona taarifa zikieleza kuwa Mwanasheria wa Halmashauri ya Wilaya hiyo, Nujum Tekka, anakusudia kumburuza mahakamani baada ya kuwatetea wafanyabiashara hao na kumaliza mgogoro uliokuwapo kwa kipindi cha muda mrefu.

  Mwenyekiti wa soko hilo, Mussa Hussein, alilieleza MTANZANIA kuwa maneno ya mwanasheria huyo aliyoyatoa hivi karibuni kuwa kadhalilishwa si kweli, kwa sababu yanaonekana dhahiri kukwamisha jitihada zinazofanywa na DC huyo.

  Alisema jitihada za kiongozi huyo zimeanza kuonekana toka alipoingia wilayani hapo kwa kutembelea soko hilo na kutatua kero mbalimbali, ikiwamo kuhakikisha linakuwa katika hali ya usafi.

  Alisema baada ya DC huyo kufanya ziara ya kutembelea soko hilo aliweza kuelezwa mgogoro uliokuwapo kwa muda mrefu kati ya halmashauri na wafanyabiashara sokoni hapo, ambapo aliamua kuwaita pande zote na kufanya kikao cha Kamati ya Ulinzi na Usalama.

  Aidha, alisema katika kikao hicho kulifanyika makubaliano pande zote kwamba wafanyabiashara katika soko hilo walipe kodi kwa halmashauri hiyo kama ilivyokuwa hapo awali.

  Alisema baada ya makubaliano hayo waliondoka na mwanasheria naye aliondoka na walipofika mahali walikoafikiana kukutana waliamua kumpigia simu na aliwaambia wakutane mahakamani, kitu ambacho kiliwashangaza wafanyabiashara hao.

  Alisema walipofika mahakamani mwanasheria aliyekuwa upande wa soko alishindwa kuzungumza, hali iliyowapa wakati mgumu na kushindwa kueleza wafanye nini kama mwanasheria huyo aliamua kufanya hivyo.

  Alisema mgogoro ulikuwapo tokea Julai, mwaka huu baada ya wafanyabiashara hao kupandishiwa kodi kinyemela na kuamua kwenda mahakamani kwa ajili ya kupata ufumbuzi wa suala hilo.

  Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Stendi ya Mabasi ya Korogwe, Wilfred Tesha, alisifu jitahada za DC huyo na kusikitishwa na hatua ya baadhi ya vikundi vya watu vinavyotaka kumchafua.

  “Kiukweli jitihada za Gambo zinaleta mafanikio na kuna baadhi ya vikundi vinatengenezwa kupunguza kasi yake, hivyo tunamuomba Rais Kikwete aendelee kumlinda na kumbakiza hapa hapa,” alisema Tesha.

  Alisema kesi iliyokuwapo baina ya wafanyabiashara hao na Halmashauri ya Mji ilidumu kwa kipindi cha miaka miwili na kusababisha DC huyo kuamua kuingilia kati na hatimaye wafanyabiashara hao wakapata haki yao.

  “Sisi kama wafanyabiashara wa Soko la Manundu hatutakubali Mrisho Gambo kuondoka Korogwe, tutaandamana na ikiwezekana kumwaga damu kwa sababu kiongozi huyo ni mtu mwenye kupenda maendeleo, lakini baadhi ya watu wanataka kumchafua, kwa hali hiyo hatutakubali,” alisema Tesha.

   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Sep 4, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Kweli sisi Wanaume tuna Issue... Tumetumia lugha chafu dhidi ya MWANAMKE na bado tunaendelea kumdhalilisha kwa kuunga

  Mkono hizo kauli...
   
 3. m

  malaka JF-Expert Member

  #3
  Sep 4, 2012
  Joined: Apr 5, 2012
  Messages: 1,323
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Kuna midemu mingine mijeuri na inanyodo sana.
   
 4. Narubongo

  Narubongo JF-Expert Member

  #4
  Sep 4, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,922
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 135
  Ni kwanini nisiamini waandishi wamenunuliwa kumsafisha gambo?
   
 5. U

  Ubungo JF-Expert Member

  #5
  Sep 4, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 1,239
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Suala ni kumdhalilisha huyo dada, hizi nyingine ni porojo za wapambe.
   
 6. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #6
  Sep 4, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,329
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Huyu si Gambo aliyewahi kutimuliwa uvccm Arusha!? Katulizwa na ukuu wa wilaya ndio anawadhalilisha nao akina mama! Upuuzi mtupu!
   
 7. Wamunzengo

  Wamunzengo JF-Expert Member

  #7
  Sep 4, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 810
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 60
  Hata kama demu ana nyodo, kidume hutakiwi kuwa mropokaji, si unamwita tu halafu unamtongoza kistaarabu??? akichomoa poa, akikubali si ndio ma-ushindi hayo??? kwa nini umtukane??? mi naona hili li-dc lina matatizo ya kujiamini hasa linapokutakana na mademu wakali. Demu hadhalilishwi bhana, demu unamsoma halafu unajua nini anataka, then unampatia ile kitu anataka, yaani saaaaafi kabisa. hili li-dc domo zito ndo maana lili-ropoka likidhani ndo ma-ujanja, kumbe linajimaliza. Li-shamba sana hili li-dc.
   
 8. KOKUTONA

  KOKUTONA JF-Expert Member

  #8
  Sep 4, 2012
  Joined: Jan 29, 2011
  Messages: 8,344
  Likes Received: 391
  Trophy Points: 180
  Nakubaliana na wewe kabisa.

  Wafanyabiashara wanayo sababu ya kumtetea GAMBO simply because yuko upande wao kuhusu mustakabali mzima wa vibanda vya biashara, umiliki na ushuru/kodi.

  Nina uhakika kabisa km GAMBO angekuwa upande wa mamlaka ya mji katika mustakabali huo hakuna mfanyabiashara angalimtetea.

  Ukweli kuhusu GAMBO, ktk utendaji wake, sawa ana kasi yake yakutaka sifa aiyemteua aonekane kuwa anafanya kazi sana but kutakitu kina kiasi chake kkizidi ni taabu.

  Amezidi ubabe, jeuri, kiburi lugha chafu na kadhalika nyiingi as if aliambiwa hicho kiti n cha milele, kwamba ana uwezo wa kufanya lolote na hakuna yoyote atakaemtoa hata akiharibu.

  As bado yuko Kor tutasikia mengi na hata hao wafanyabiashara watakuja kereka tu.
   
 9. KOKUTONA

  KOKUTONA JF-Expert Member

  #9
  Sep 4, 2012
  Joined: Jan 29, 2011
  Messages: 8,344
  Likes Received: 391
  Trophy Points: 180
  Km alishawahi kutimuliwa huyu mkuu wa kaya alifikiri nini hadi kumpa u DC km alishashindikana chamani?
   
 10. v

  viking JF-Expert Member

  #10
  Sep 4, 2012
  Joined: Aug 23, 2012
  Messages: 984
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 45
  Kudhalilisha mtu atende yeye ,halafu unaomba apewe ulinzi ,wewe umetumwa akili yako sio nzuri
   
 11. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #11
  Sep 4, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 160
  huyu keshazoea siasa chafu, basi atamchafua huyu dada wee ambaye hana uzoefu wa siasa.

  Wazee wengine tushaona, Miss Tekka, kaza uzi kama umesimamia haki.
   
 12. Narubongo

  Narubongo JF-Expert Member

  #12
  Sep 4, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,922
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 135
  bei ya waandishi wetu ipo chini sana, kitendo cha gambo hakivumiliki na iwapo tungekuwa na tabia ya kuwajibishana leo hii asingekuwa ofisini
   
 13. b

  bdo JF-Expert Member

  #13
  Sep 4, 2012
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,712
  Likes Received: 1,611
  Trophy Points: 280
  Tena nakumbuka tulipokuwa shule, darasa zima tulikuwa tunakula fimbo na kupiga magoti iwapo kuna mwl amempenda demu ila hawezi kumwambia, DC Gumbo na wananchi wa Korogwe hauwezi kumlinda mtu dhidi ya sheria, go mwanasheria mpaka kieleweke, kwanza inaonekana kabisa DC ameingilia uhuru wa Mahakama
   
 14. KOKUTONA

  KOKUTONA JF-Expert Member

  #14
  Sep 4, 2012
  Joined: Jan 29, 2011
  Messages: 8,344
  Likes Received: 391
  Trophy Points: 180
  You see, nchi hii kulindana kwingi, watu wamelewa madaraka wamesahau wajibu na majukumu yao.

  Lakini ukombozi uko njiani, wote wanaonunuliwa na kutumiwa kuwabeba viongozi wasio na tija na maslah kwa taifa wataisoma namba.
   
 15. Obama wa Bongo

  Obama wa Bongo JF-Expert Member

  #15
  Sep 5, 2012
  Joined: May 10, 2012
  Messages: 4,767
  Likes Received: 2,494
  Trophy Points: 280
  huyu gambo sindio yule kilaza ya manispaa arusha na uvccm, ukuu wa wilaya kaupata lini! dah ,mkuu wa kaya appontment zake bwana! ndo maana alichagua judge mahakama kuu asiye na degree! alafu sasa hivi ndo anasoma open university sasa hivi
   
Loading...