Wafanyabiashara waomba kununua korosho

Wafanyabiashara waomba kununua korosho

Kila kitu kipo sawa.magufuli amepiga hesabu ameona asiangalie maslahi ya watu wasiofika hata 10000 Ni heri aangalie maslahi ya wakulima wanaozidi 1000000
Bado niko siti ya mbele na popcorn zangu nacheki tu hii movie! Kuna kitu hakiko sawa but time will tell!
 
Wafanyabiashara ni yale makampuni 35 yaliyopewa hadi j3 ila hawakujitokeza na hawajajitokeza
Hao wengine ni machinga
 
Bado niko siti ya mbele na popcorn zangu nacheki tu hii movie! Kuna kitu hakiko sawa but time will tell!
HATUA ya serikali ya kununua korosho kwa bei kubwa na kuwaweka pembeni wafanyabiashara waliokuwa na nia ya kuwadhulumu wakulima, inaweza kuelezewa kuwa ni ushindi na mafanikio kwa wakulima wote wa Tanzania.

Tunasema kuwa ni ushindi kwa kila mkulima kwa kuwa kama imewezekana kudhibiti dhuluma kwenye korosho hata kwenye mazao mengine itawezekana.

Kwa wakulima wa korosho huu ni ushindi ambao unadhihirisha kuwa serikali imedhamiria kuwatetea wakulima kutokana na changamoto mbalimbali zilizokuwa zinawakatisha tamaa kwa miongo mingi.

Madhila ya wakulima hawa ni pamoja na ukosefu wa soko la zao hilo na bei ndogo inayotolewa kwa wakulima bila kujali gharama kubwa walizopata kuanzia kuhudumia hadi kuvuna mazao hayo.

Wakulima wa korosho wamekuwa waathirika wa bei ndogo kwa miaka mingi tangu kufungwa kwa viwanda vya korosho zaidi ya miaka 20 sasa.

Kwa ujumla changamoto zote za kilimo cha zao hilo zikijumuisha gharama kubwa za pembejeo zilirudi kwenye mifuko ya wakulima ambayo inatoboka zaidi kwa kuwa hawana fedha za kulipia gharama za uzalishaji, wala kujikimu kwani hata kile walichozalisha hakuna mnunuzi na hata akijitokeza ni kupunjwa.

Katika sakata la sasa la kutaka kuwaumiza wakulima licha ya korosha kuwa na bei kubwa kwenye soko la dunia, Rais John Magufuli, alionyesha msimamo kuwa hayuko tayari kuona uuzaji wa zao hilo ukichezewa tena kwa kuwapunja wakulima, kwa wafanyabiashara kununua kilo moja ya korosho kwa Shilingi 1,500 badala ya zaidi ya Sh. 3,000 kama serikali ilivyoelekeza.

Tunaunga mkono hatua ya serikali ya kuhakikisha kuwa wajanja wachache hawapewi nafasi ya kuwahujumu wakulima na taifa zima.

Ni wazi kuwa korosho ni zao la thamani kubwa ambalo kwa jinsi lilivyo na umuhimu wa kipekee kila kinachozalishwa kuanzia maganda, mafuta na mbegu huongezewa thamani na kuzalisha bidhaa nyingine nyingi zenye thamani kubwa. Kwa hiyo korosho ni mali.

Kwa upande wa afya zinatajwa kuwa na umuhimu wa kipekee na ni chakula cha watu mashuhuri wakiwamo wafalme na matajiri duniani, kwa hiyo si zao la kupuuzwa na wanunuzi kufanya vile watakavyo.

Hatua ya serikali ya kununua zao hilo na kuwalipa wakulima fedha zao kwa wakati linastahili pongezi na pia inafaa kuwa endelevu kwa kumulika uuzaji wa mazao mengine kwa hila na mbinu za kuwapunja wakulima.

Tunaipongeza serikali kwa kudhihirisha kuwa hizi si zama za kuwapunja wakulima kama ilivyokuwa imezoeleka . Kwani kuna wakati wakulima walipunjwa mno na kufikia hatua ya kukasirika wakifikia maamuzi ya kukata mazao na kufuga wanyama.

Kupitia hatua zilizochukuliwa kwenye korosho wafanyabiashara wameona kuwa hizi siyo enzi zile walizozoea za kununua kilo moja ya ufuta kwa senti 50 au alizeti kwa Sh 100.

Ni wazi kuwa serikali imekuwa mkombozi mkubwa kwa wakulima hao ambao hutumia gharama kubwa kuzalisha lakini huambulia kiasi kidogo kwa kuwa wamekuwa ni watu wa kupunjwa na wafanyabiashara ambao hawana lengo la kuwaendeleza bali kuwadumaza.

Ndiyo maana tunaipongeza serikali kwa maamuzi hayo na kusimamia ule msimamo kuwa inawezekana bora kila mmoja atimize wajibu na hatua zilizochukuliwa na Rais zinaonyesha wazi kuwa wakulima hawatakuwa tayari kuonewa.

Tunaipongeza serikali kwani kama isingechukua hatua hizo ina maanisha kuwa wakulima wetu wangerudi nyuma tena kwenye zama za kupunjwa na kulalamikia bei ndogo. Hongera Rais kwa kuwapa wakulima kile wanataka.
 
Ninaunga mkono juhudi za serikali! Lakini ikumbukwe kuwa wakulima wanaopitia madhila ya jinsi ile si wa korosho peke yake. Serikali ina kazi kubwa ya kufanya baada ya mwanzo huu mzuri!
 
Hii inamaana gani? niko njiani naelekea huko ntarudi jukwaani

======

Mtwara. Wakati Serikali ikiendelea na mpango wake wa kununua korosho baadhi ya wafanyabiashara wameomba wanunue korosho hizo ili waendelee na ubanguaji katika viwanda vyao.

Maombi hayo yamekuja baada ya Waziri wa Kilimo na Umwagiliaji, Japhet Hasunga, Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Joseph Kakunda na mkuu wa mkoa wa Mtwara, Gelasius Byakanwa kutembelea viwanda hivyo pamoja na kukagua maghala.

Akiwa katika kiwanda cha Micronix mkini Mtwara mmoja wa watumishi wake, Catherine Julius alimwambia waziri ana ombi na kumweleza wanaomba kununua korosho hizo ili wanawake walioajiriwa katika kiwanda hicho waendelee na ajira zao.

“Mheshimiwa waziri tuna ombi, hiki ni kiwanda na zaidi kimeajiri wanawake ambao wana watoto na wengi wao hawana watoto, sasa tuna ombi tunaomba tuuziwe korosho ili tuweze kuendelea na shughuli za ubanguaji na ajira zetu,”amesema Julius.

Hata hivyo, Mkuu wa mkoa huo Gelasius Byakanwa amesema Rais alipoamua kuingilia kati na kununua korosho ilionekana kama ni kuwaonea wafanyabiashara na hawakusikilizwa lakini Serikali ilikuwa makini kuzinunua kwani inajua michezo inayochezwa na wafanyabiashara.

“Waandishi wa habari leo mmekuwa mashuhuda wafanyabiashara wenyewe wakiomba kuzinunua korosho, kwa soko lililopanda lini? Kwa bei ya lini ambayo inaweza kuwalipa? Kwa hiyo ni meseji tosha kulikuwa na mgomo, kwanini leo wanaomba wakanunue korosho kama soko la dunia haliwalipi?”Alihoji Byakanwa.

Aliendelea, “Wale wanaoathirika na ajira kwanza ni masuala ya mkataba na waliowaajiri, lakini Serikali itawahitaji wataalamu wa kubangua korosho ambao ni Watanzania watapata ajira kwenye viwanda vya Serikali ambavyo itavitumia, lakini niwaombe waandishi wa habari mfikishe ukweli walipoomba mlikuwepo na mmeona.”

Akizungumzia suala hilo, Waziri wa Kilimo, Hasunga amesema wakati wanaanza msimu wa ununuzi wafanyabiashara waliweka bei ndogo kwa madai bei katika Soko la Dunia imeshuka jambo ambalo ni kweli lakini si kwa kiwango wanachodai.

Amesema baada ya kuapishwa wametumwa Mtwara kuhakiki kwanza kama korosho zipo kwenye maghala na wamehakiki ziko nyingi lakini pia amekutana na wafanyakazi wengi ambao wanafanya shughuli zinazohusiana na korosho.

“Wakati Mheshimiwa Rais alipotangaza bei tulitangaza bei ya kumlipa mkulima, hatukujua kama kuna watu wengine huku ambao wanafanya hiyo kazi na wao wanastahili kulipa, sisi tukajua korosho si zipo.

“Tulipokuja jana nikajifunza kumbe Amcos zinakusanya korosho kwa wakulima na baada ya kukusanya kuna wafanyakazi wengine wanazipokea kutoka kwa wakulima na kuzipakia kwenye magari kuzipeleka kwenye maghala makubwa na wao wanatakiwa kulipwa,” alisema Hasunga.

Chanzo: Mwananchi
Huu ni upotoshaji wa kimkakati. Habari hii haisemi kama wafanyabiashara wameomba kununua korosho. Huyo ni mfanyakazi wa kiwandani anayehofia kuwa atakufa njaa kama viwanda vitakosa korosho za kubangua. Kwa namna habari hii ilivyowekwa ni kama Mwananchi nalo linajaribu kujihami ili lisikose kabisa matangazo!
 
Kwa hiyo unataka kusema mfanyakazi aliye omba wauziwe Korosho anauwezo wa kutoa hiyo shs 3,300 au zaidi au kumshawishi bosi wake atoe hiyo hela. Kama sio mkakati wa hao waliogoma kuwatumia hao wafanyakazi??? Akili Za kuambiwa changanya Na zako.
 
Kumbe na wewe umeelewa kwamba ni "mfanyakazi aliyeomba" na sio mfanyabiashara? Case closed!
 
Ni kweli case closed maana hakuna mfanyabiashara mwenye kuta kununua Kwa tshs 3,000 Na juu ya hapo Kwa kukosa Uwezo Na pia Kwa kuwa bei ya soko la dunia ni ndogo kuwawezesha hao wafanyabiashara kupata faida. Hivyo serakeli au huyo wakala wa Serekali atakaye nununua Kwa tafsiri yako atapata hasara wakati kuna wafanyabiashara 13 walimwandikia waziri mkuu kwamba wapo tayari kuinunua Kwa tshs 3,000 . Hivyo hawa wafanyabiashara walikuwa tayari kutengeneza hasara. Kwa tofauti ya bei Yao ya awali Na hii ya tshs 3,000.
Na hivyo wewe una akili saana ku liko hao wafanyabiashara walio mwambia waziri mkuu kwamba wapo tayari . Akili yako Kwa kweli imetukuka Na hivyo wafaa kuwa kiongozi wa akili ya kuambiwa changanya Na zako
 
Sijui kwanini kiwango cha kufikiri cha wengi kinashuka kwa kasi sana awamu hii. Haya unayoyaleta hapa kuninukuu, yana uhusiano gani na kile nilichokiandika? Kweli mmevurugwa.....
 
Ni kweli kiwango cha kufikiria na kuelewa kwa baadhi ya watu kipo chini ndio maana JK 2 alisema akili za kuambiwa changanya na za kwako sio unaenda kama gari lisilo na muendeshaji.
Maana mtu na akili zake anaambiwa "mfanyajazi" kaomba wauziwe korosho wasikose kazi kaona hilo jambo lina uzito juu ya haki ya bei nzuri kwa mkulima, pili mtu huyo huyo anaona ombi hilo la "nfanyakazi" lifanyiwe kazi na waziri wakati "mfanyakazi" huyo si muamuzi wala mtoa pesa wa hicho kiwanda
 
Back
Top Bottom