BekaNurdin
JF-Expert Member
- Dec 21, 2012
- 2,267
- 2,041
Heshima kwenu wana JF!
Jana nimeenda Kariakoo kununua kifaa cha computer. Baada ya kulipa pesa nilipodai risiti nikapewa ya kuandikwa na kalamu, nikaikataa. Nilipoikataa wakaanza kukonyezana wao kwa wao, wakaniona nuksi! Nikawaambia isiwe taabu, nirudishieni pesa yangu na kifaa chenu chukueni. Nao bila kusita wakanirejeshea pesa yangu.
Nikaanza kuzunguka maduka mengine nipate kifaa hicho pamoja na risiti halali, duka la pili hola! Duka la tatu hola! Kifaa kipo ila risiti ya kimagumashi. Ile mvua iliyonyesha jana Kariakoo haikuniacha kunitwanga nikijitahidi kuwa mzalendo wa ukweli ili kuiwezesha serikali ipate kodi yake.
Style hii ya ukwepaji kodi inayofanywa na wafanya biashara pale Kariakoo imeandikwa mara nyingi sana hapa JF lakini TRA hawaonekani kuchukua hatua. Kwa nini wasitume maskauti wajifanye wateja kisha wawakamate hao manyang'au? Sasa natambua majipu hapo TRA bado hayajatumbuliwa yote. Mtumbuaji kazi kwako! Nawasilisha hoja!