Wafanyabiashara jihadharini na siasa kipindi hiki

Wafanyabiashara jihadharini na siasa kipindi hiki

East African Eagle

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2013
Posts
3,759
Reaction score
2,209
Kipindi hiki hadi kufikia october wakati wa uchaguzi wafanyabiashara wanatakiwa kuwa makini nani wanamchangia.

Ni vizuri kuwa na wataalamu wa kuwashauri vizuri kuwa je wanakoegemea kuko salama kwa biashara zao kwa kipindi hiki hadi october na baada ya october uchaguzi ukishafanyika?

Huu ni wakati ambao kile kitu kinaitwa political risk kinakuwa juu sana.Chaweza sababisha biashara kuharibika sasa hadi october au hata baada ya october.

Nawaomba wafanyabiashara wote waliangalie vizuri eneo la political risk kwenye biashara zao kabla ya kuwa na mihemko ya kisiasa na kujitosa kichwa kichwa kuunga mkono wagombea na kumwaga pesa zao.

Katika ushabiki wa kisiasa ni vizuri kuwa makini.Hii ni pamoja na magazeti na vyombo vyote vya habari political risk yaweza geuka ikawa business risk wafanyabiashara wasipokuwa makini.

Ni wakati wenye vyombo vya habari kutoachia tu wahariri ni vizuri wawe karibu na vyombo vyao maana biashara ikibuma mhariri ataenda tafuta kibarua sehemu nyingine akiacha biashara iliyobuma kwa mwenyewe.
 
Don't worry. I, Richard Mugizi aka Nyani Ngabu halisi will take care of it.
 
Halafu wewe ni mjiinga sana. Yaani CCM haitegemei kuomba hela Kwa wafanya biashara. Ina hela za kutosha. Ila jamaa katahadharisha kuwa timu ya Edo inaweza kudanganya watu kama ilivyo wadanganya wafanya biashara akina karamagi, rostam, mengi kumchangia eti atakuwa rais awape dili na akadondokea pua. Sasa mtoa maada anawapa tahadhari wafanya biashara kuepuka kundi la kina edo kwani Magufuli hahitaji ujinga wa hivyo, Yule ni Ngosha!!

haya ya magufuli yalikuwemo au umeyaweka wewe ?
 
Ushauri mzuri. Maamuzi yatabaki kuwa kwao.
 
Mlivyowanyima gesi na kumpa Mchina mlitegemea nini??

Mnaumia kuona Mengi na Bahressa wanawakimbia sio??
 
Back
Top Bottom