Wafahamu legends wa bongofleva

Wafahamu legends wa bongofleva

Mlaleo Kuwa wa kwanza kwenye game haimaanishi kwamba we ndo mkali kuliko waliokuja baada yako, kinachomata ni wewe umeifanyia nini game. Hao wakina Nigga One wangapi wanawajua? Maana huwezi kusema mtu ni legend wa muziki wakati ni underground. Sugu alijitengenezea himaya yake, na kwa michano aliyokuwa anasupply kijana wa wakati huo lazima umjue japo redio ya FM ilikuwa moja tu.

Halafu HBC nimeitaja hapo kwenye maelezo ya Jay. Profesa Jay ndo alikuwa kichwa HBC, na hilo unahitaji kubishana? CHEMSHA BONGO, wimbo ulioitambulisha HBC verse zote kachana Jay. Then akaja kuprove zaid kwamba ye ndo kichwa cha kundi baada ya kutoa Album yake ya kwanza kama solo artist 'MACHOZI JASHO NA DAMU' na kukimbiza ile mbaya kwa mapini ya kihistoria humo ndani. Hebu niambie baada ya kundi kuseparate wakina Terry(Fanani) walifanya nini?

Unaikimbia Mada yako wewe mwenyewe... Unaposema yeye ndie alikuwa kichwa ina maana hao wenzake si lolote si chochote?
 
profesa
inspector
afande
mwanafa
duly
kikosi
blu
tid
ngwea
noorah
jide
jay mo
gk
ay
fa
nk nk
 
Hawa ni watu ambao kwa mtazamo wangu wana impact kubwa sana kwenye huu mziki wa kizazi kipya "Bongofleva", yaani wameacha alama ambayo haitakuja kufutika vizazi na vizazi, wametoa hamasa kubwa kwa wasanii wengine wa miaka ya kuanzia 2000 na kuendelea;

1. JOSEPH MBILINYI (SUGU)---Huyu ndo msanii aliyeanza kurap siriaz kwa kutumia Lugha ya kiswahili na kukubalika na vijana wengi katikati ya miaka ya 90, akafanikiwa kurelease albam nyingi na kuwafanya wasanii kibao kupata confidence ya kufanya alichokuwa anafanya.

2. JOSEPH HAULE (PROF JAY)----Huyu aliendeleza alipoishia Sugu, kupitia huyu Bongofleva ilitanua fanbase kwa kiasi kikubwa, alifanikiwa kuondoa ile zana kwamba mziki (esp Hiphop) ni uhuni, watu wa rika tofauti wakaanza kusikiliza Bongofleva na kuachana na muziki wa kikongo na taarabu vilivyokuwa vimetawala sana enzi hizo.Wasanii pia walistuka, wakaanza kutunga vitu vya maana. Wimbo wake wa alioufanya akiwa na HBC "CHEMSHA BONGO" ulileta mapinduzi makubwa kwenye muziki huu


3. JUDITH WAMBURA 'LADY JAYDEE'----Alianza game kwa kusuasua, alitoa nyimbo mbili tatu ambazo hazikupata attention ya kutosha kabla ya kuachia 'BOMU' wimbo unaoitwa MACHOZI ambao ulikuwa kama wimbo wa taifa enzi hizo, ukiukosa redioni unaukuta kideoni. Naweza kusema video ya MACHOZI ndio video bora ya kwanza kuachiwa na msanii wa bongofleva, kwa wakati huo ilikuwa inaonekana video babkubwa na ndipo wasanii wakaanza kustuka kwamba na Bongo tunaweza kufanya video kali.Wimbo huo ulimpa mafanikio makubwa ndio maana neno 'Machozi' hadi leo hii bado analitumia kwenye biznes zake. Hata hivyo Jide hauishia hapo, aliendelea kutoa nyimbo n' album nyingi zilizofanya vizuri sokoni. Hadi leo hii haijatokea msanii wa kike aliyeweza kuwa consistent kwenye game kama yeye, ndio maana hadi leo hii zikiandaliwa tuzo, msanii bora wa kike anakuwa yeye hata asipokuwa na single inayobamba hewani.


# Tupia jina la msanii ambaye sijamtaja hapa ambaye unadhan anastahili kuitwa LEGEND

Hii list kama haina Jay Mo, Juma Nature, Crazy GK, basi ni feki!!
 
Unaikimbia Mada yako wewe mwenyewe... Unaposema yeye ndie alikuwa kichwa ina maana hao wenzake si lolote si chochote?

walikuwa na uwezo wa kawaida, Prof Jay alikuwa exceptional
 
Back
Top Bottom