Waenda kufunga ndoa kwa gharama ndogo

Waenda kufunga ndoa kwa gharama ndogo

bwafo

Senior Member
Joined
Mar 18, 2011
Posts
103
Reaction score
70

Na Dustan Shekidele, Morogoro
WANANDOA Charles Kanyema (29) na Bi. Onoratha Pascal (28) hivi karubuni waliwashangaza wakazi wa Manispaa ya Morogoro baada ya kwenda kufunga ndoa wakiwa wamepanda bodaboda na kurejea nyumbani kwa kutembea kwa miguu.
Ndoa hiyo iliyofungwa katika Kanisa Katoliki Jimbo la Morogoro Mjini na kufungishwa na Paroko Msaidizi, Padri Phidelisi Mwesongo iligharimu shilingi 45,000 tu.
"Gharama hizo ni pamoja na picha 5 kwa ajili ya kumbukumbu yetu na nyumbani tumenunua mchele na nyama kwa ajili ya sherehe ndogo," alisema bwana harusi Kanyema.
Alisema fedha hizo zilitokana na michango waliyochangiwa na wana jumuiya wenzao na hawakutaka mambo makubwa katika sherehe yao.
Mara baada ya kuwafungisha ndoa, Padri Mwesongo aliwataka wanandoa hao kutambua kwamba maisha ya ndoa ni magumu na yanahitaji uvumilivu ili ndoa yao iweze kudumu.
Baadhi ya watu waliohudhuria sherehe hiyo waliwasifu wanandoa hao kwa kutotumia gharama kubwa wakidai kwamba mara nyingi ndoa zilizojaa kila aina ya mbwembwe huwa hazidumu.



MWANZO MZURI!
Source
WAENDA KUFUNGA NDOA KWA BODABODA, WARUDI KWA MIGUU - Global Publishers
 
Mungu awabariki katika ndoa yao, wazae watoto wakike na wakiume
 
Kumbe umaskini nao ni Ufahari?
 
very impressive am looking forward for the similar kind of wedding
 
Nimeipenda. ..mengine tunajitakia migharama ya bure, kwasababu hiyo nilishapiga marufuku kadi za mchango wa harusi.
 
Tena wamefunga ndoa mchana ?? bado ni gharama, wangefunga usiku kuepuka vitoto vya uwahilini ....wange sevu 30,000/= inatosha kuanzia maisha wiki nzima bodaboda 2,000/= mshkaki buku 3 soda wangebaki na 10 ya pilau
 
Safiiii, lakini sometime inabidi tutumie gharama sbb ni siku moja tu ktk maisha ya mwanadamu,ni sikukuu kubwa ya mwanadamu ndo maana watu hupenda kujifua wawezavyo, lkn ndo hivyo kila mtu hula kwa urefu wa kamba yake, km zipo we jilipue tu, km hamna hata chai na mandaz yatosha.
 
Huu ni mfano wa kuigwa!funga ndoa ya gharama kubwa kama unaweza kuigharamia mwenyewe..Hizi habari za watu kufunga ndoa kwa bajeti ya milioni kumi wakati wao wana shilingi laki mbili sio fair..Natamani siku moja ifike Tanzania kila mtu agharamie harusi yake mwenyewe na sio kusumbua watu..Mimi nitakua mfano,kama sina hela za kufanya sherehe nitaenda kanisani na mwenzangu baada ya hapo tunaendelea na ratiba zetu tulizopanga wenyewe.Big up kwa hao wanandoa. Nimeipenda hiyo
 
Back
Top Bottom