WADOGO ZANGU NJOONI TUSHAURIANE.

Nyarubhangara

Member
Aug 4, 2019
36
25
Amani iwe kwenu wana if.
Mimi ni mgeni humu jf japo nimekuwa mfuatiliaji wake kwa muda sasa, nashukuru kwamba panaelimisha na kuburudisha si haba.
Niende kwenye pointi ;Kuna tabia ambayo wadogo zangu vijana huwa wanayo ambayo si nzuri kwa kweli, sijui Kama Mimi ndo nitakuwa tofauti lakini ni tabia ambayo hainifurahishi hasa.Utakuta kijana anamtongoza binti/mwanamke kwa sura ya hekima na adabu lakini binti/mwanamke atakapo ingia nae kwenye mahusiano chochote watakacho kifanya falaghani atakipeleka kijiweni kwa wenzie na kuhadithi yote yaliyojili a-z wengine mpaka picha wanachukuana,na ikitokea mwanamama akapita maeneo hayo basi utawakuta wakimsonta vidole wengine wanapiga mpaka miruzi. Sasa wadogo zangu huwa mnafanya hivo kwa kutaka nini hasa?!humuoni kifanya hivo Kama ni kujidhalilisha na wewe pia mbali na kumdhalilisha mwenzio? Karibuni tusemezane
 
Jaribu upande wa wazee maana wao hawatumii Simu janja wala mitandao ya kijamii. Nafikiri huko mtapata amani ya kutosha
 
Huo ni utoto na ni watoto pekee ndio hushiriki mambo hayo ili kujipatia sifa. Matured man hawezi kujitafutia sifa kupitia Mambo hayo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom