Wadoeaji muwe na heshima

marrykate

JF-Expert Member
Joined
Mar 4, 2012
Posts
733
Reaction score
444
Bwana we si nikatokea kumpenda mkaka mmoja hapa ofisini, muda mrefu tu umepita, sema kila nikijipendekeza alikuwa haelewei somo, basi nikaamua kuacha na hizo mambo za kumuwinda winda kila mara, miaka miwili ikapita ghafla na yeye akaanza kujiweka karibu na mimi, kwa vile nampenda sana sikuweza kuresist basi nikarespond nikamchukulia kama rafiki wa karibu tu sio mpenzi.

Sasa katika mazoea haya ya urafiki mwenzangu sijui anahisi yupo na mke wake, kila siku anataka apate chakula cha jioni kwangu, basi nitajipikilisha wee jamaa anakuja anakula anasepa, huyu jamaa anapenda vyakula vya kuchemsha tu, visiungwe hata, na mimi napenda kukaanga ile mbaya,akaanza visa akikuta tumepika chakula asichopenda matusi yatamtoka huyo utafikiri alitoa hela halafu nikanunua vitu vingine.

Kujifanya kuimiliki nyumba utafikiri anajua hata kodi ya nyumba ni sh ngapi, akifika home basi itabidi muangalie vipindi anavyotaka yeye tu, maongezi yawe anayotaka yeye tu, feni izimwe.

Nimemwambia mara kadhaa kuwa yupo selfish sana anaona kama namtania vile nimfanyeje huyu mtu jamani?
 
mbunye kashaiona maana hujatuambia hapo
 

aisee......
 
Hebu timua aache kichefu chefu lol....



 
Umesema sio mpenzi wako anakupaje commands za kumpikia anachotaka?? Aoe basi kwanza
 
Umempenda mwenyewe! Sasa amekuwa mdoeaji? I guess, uliyotarajia kwake hukuyapata, ni ustaarabu kujiondoa mwenyewe.
^^
 
wewe si mkweli, hakuna mwanume wa aina hiyo duniani,huyu ni mtu wako ila pengine umemchoka tu,unashindwa kumwambia sababu kuna vitu lazima ana ku support.
 
Ndo ushamjua alivyo amua kusuka au kunyoa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…