Wadau nifanyeje wanipe mafao yangu?

cosa nostra

JF-Expert Member
Sep 17, 2010
1,773
1,805
Wadau nifanye nini?

Huu ni mwaka unakatika sina kazi, kipindi mkataba wangu wakazi unaisha nilikua na matumaini ya kupata pesa zangu kutoka mfuko wa hifadhi ya jamii ila naona suala hili limegonga mwamba ndio lilikua tegemo langu sikopesheki nina watoto na mke wananitegemea.

Hivi huu mchakato wa fao la kujitoa ndio forever au wataanza kututoa soon.

Jamani pesa zangu zinaniuma sana.
 
Pole sana kaka sisi viongozi wetu ndio wameamua iwe hivyo yaani wametumaliza kabisa tufe pamoja vizazi vyetu.
 
Pole sana mkuu,jaribu kuwa unaenda kwenye mfuko husika usikie wanasemaje juu ya mafao usichoke ukiona hawaeleweki nenda mpk ssra ukajue nn hatma
 
Hili fao la kijitoa ni bomu litalolipuka mda si mrefu Just wait and see yaani PESA yangu mwenyewe bado figisu nilitewe mara ooh mpaka sijui miaka 55 ifike ndio upewe kwani serikali inauhakika nitafikisha hiyo miaka, hv wanajua uchungu tunaoupitia tukiwa makazini ? Leo mtu kaamua kuacha kazi ili achukue mafao yake ajiajiri mwenyewe nyie mnaanza kumbania wakati hela za makato ni jasho Lake mwenyewe. Patachimbika
 
Pole sana mkuu,jaribu kuwa unaenda kwenye mfuko husika usikie wanasemaje juu ya mafao usichoke ukiona hawaeleweki nenda mpk ssra ukajue nn hatma
nimefuatilia wana sema eti niendelee kuchangia sijui from kipato gani,eti nitapata tena kazi kama wananitafutia vile

kijumla siwaelewi
 
Hili fao la kijitoa ni bomu litalolipuka mda si mrefu Just wait and see yaani PESA yangu mwenyewe bado figisu nilitewe mara ooh mpaka sijui miaka 55 ifike ndio upewe kwani serikali inauhakika nitafikisha hiyo miaka, hv wanajua uchungu tunaoupitia tukiwa makazini ? Leo mtu kaamua kuacha kazi ili achukue mafao yake ajiajiri mwenyewe nyie mnaanza kumbania wakati hela za makato ni jasho Lake mwenyewe. Patachimbika
wakati huu una nguvu hata ya kufanya biashara wao wanakaonayo mpaka uzeeni, then ukiangalia upande mwingine wa ajira ndo hivo utasota sana
 
Hili fao la kijitoa ni bomu litalolipuka mda si mrefu Just wait and see yaani PESA yangu mwenyewe bado figisu nilitewe mara ooh mpaka sijui miaka 55 ifike ndio upewe kwani serikali inauhakika nitafikisha hiyo miaka, hv wanajua uchungu tunaoupitia tukiwa makazini ? Leo mtu kaamua kuacha kazi ili achukue mafao yake ajiajiri mwenyewe nyie mnaanza kumbania wakati hela za makato ni jasho Lake mwenyewe. Patachimbika
kama mimi nimechoka sana mkuu
 
Wadau nifanye nini

Huu ni mwaka unakatika sina kazi

Kipindi mkataba wangu wakazi unaisha nilikua na matumaini ya kupata pesa zangu kutoka mfuko wa hifadhi ya jamii ila naona suala hili limegonga mwamba

ndio lilikua tegemo langu sikopesheki nina watoto na mke wananitegemea

hivi huu mchakato wa fao la kujitoa ndio forever au wataanza kututoa soon

jamani pesa zangu zinaniuma sana
Watakuwa pp....hawa mm mwaka wa Pili sasa mkuu cna hamu niliambiwa wanadili na watu waliofikisha miaka 15 kazini Na kuendelea na mambo mengi kama hayo yako...ila cc wa miaka miwili mi3 tusubiri tamko la sirikali hii sasa cjui mpaka lini,..

Eeeeee unikumbukee
 
Nssf noma! Ni mfuko mkubwa kuliko mifuko yote! Lakini walikuwa wanatoa mafao kiduchu kuliko pspf na Lapf japo hii ni mifuko michanga! Uzoefu unaonyesha wastaafu wengi hufa ndani ya miaka 5! Sasa hizo pesa zinakusaidiaje?
 
  • Thanks
Reactions: ari
Moja kati ya maamuzi ya ajabu kuwahi kufanywa na kuwaathiri watu wengi hili la kuzuia makato yetu walala hoi ni mojawapo.

Vikampuni vingi vya mjini havina mikataba mirefu na wafanyakazi wake baada ya miaka miwili ama mitatu unatimuliwa. Vingine vina-exist ndani ya muda mfupi vinakufa.

Imagine una miaka 30, mke na watoto,naishi nyumba ya kupanga then kutokana na kuyumba kwa uchumi kampuni imekupunguza kazini,na kutafuta kazi nyingine hupati kozi kila mahala hali ni tete.

Tegemeo kubwa na pekee mtu uchukue mafao yako ukalime hata viheka vya alizeti na mahindi ili kusukuma maisha mbele hala unaambiwa subiri miaka 25 ijayo ndio uje.....! Nije nikiwa maiti? ama nije vipi? nitaishije mimi na familia yangu? mbona serikali hii inaitesa mioyo yetu? watoto wanalia njaa chakula hakuna matokeo yake nini nini?

Pesa yako ulikuwa unakatwa kila mwezi leo hii unapangiwa umri wa kwenda kuichukua kweli?
Huu ni use.nge.rema ambao unapaswa kuachwa.
 
Binafsi sioni haja ya kuendelea kuwachangia hawa wezi,cha msingi ni kuacha kazi na kudeal na ujasiriamali tuu.
Pengine nitayumba kidogo mwanzoni lakini ni bora zaidi kuliko kukatwa pesa kila mwezi halafu mwishowe hupewi kwa wakati.
 
Wakati mwingine sipendi kuziona au kuchangia hizi mada Kwa sababu hakuna mwenye uthubutu wa kuchukua action... Tutaishia kupiga kilele wee... Bora tuziache hizi mada..
 
nimefuatilia wana sema eti niendelee kuchangia sijui from kipato gani,eti nitapata tena kazi kama wananitafutia vile

kijumla siwaelewi
Nyambaff zao wanajibu kana kwamba wao ndo wanakusaidia kutuma applications ....nchi.imeshakua ya kinyambaff sana....
 
Back
Top Bottom