Wadau naombeni ushauri

Sukari Yenu

JF-Expert Member
Dec 8, 2014
1,698
1,255
Umuofia kwenu wakuu wa humu,

Naamini humu kuna watu tofauti wenye mawazo yatakayosaidia kufanya maamuzi sahihi, ikizingatiwa wengi wenu mmeshapitia hali kama hizi katika maisha au kushuhudia kwa mtu unayemfahamu na ukaona alichofanya.

Suala liko hivi, nina ndugu yangu amemaliza masomo (chuo kikuu) mwaka 2014. Akayaanza maisha ya mtaani na Mungu si athumani akapata ajira ya kujikimu Januari mwaka 2015, kwa mkataba wa mwaka 1 ambapo malipo yake ni kwa mfumo wa commission. Basically anapokea 400,000 before deductions ila kuna nyongeza ya commission endapo atafikisha percentage fulani ya target zao.

Kwa mwaka mzima hali imekua ngumu kazini na kufikisha hizo percent ili apate bonus imekua shughuli pevu hata kwa wenzake pia hali ni hiyo hiyo. Kwa hiyo mara nyingi alikua anavuta 400,000 deal ikiwa fresh anapata zaidi pia.

Sasa mkataba umeisha 31st Dec 2015 na wamefanya review ya performance amedai wamemwongeza miezi 3 waangalie utendaji huenda wakamchukua moja kwa moja na kupata atleast malipo yenye uafadhali au waachane nae for good.

Juzi kati hapo kapata deal ya kufanya kazi mahali kwingine. Malipo ni 450,000 per month before statutory deductions na hamna cha zaidi, mikataba ya miezi mitatu mitatu to the infinity (coz haijulikani kama kuna chance ya kuwa permanent employee), au kutoongezwa baada ya muda fulani.

Sasa je, aache huko aliko sasa hivi afanye maamuzi magumu kama Lowassa au akomae hapo alipo mpaka kieleweke. Mimi binafsi nimemwambia bora shetani unayemfahamu kuliko malaika usiyemjua, hivyo akomae hapo alipo huenda deal ikakaa sawa.

Magreat thinkers mnamshauri vipi ndugu yangu, best yangu tangu primary school? Afanyeje?
 
Back
Top Bottom